Blogs
 
ARTICLES
Mwajabe Kizigina     Email : kizigina@nifahamishe.com     
JE NI SAWA BABA KUMUOMBA MSAMAHA MWANAE
             
Kama kawaida yangu katika ukurasa huu huwa sina mada maalumu ambayo naileta kwenu wananchi ila huwa nakuwa na general view katika mambo yanayoihusu jamii.
Siku ya leo nimeamua kuja na hii mada kuhusu wazazi zaidi wazazi wa kiume.

Katika mazingira ambayo tunakulia sisi watanzania mara nyingi mama ndio anakuwa karibu na watoto zaidi kuliko baba. Ofcourse hii inaweza kubadilika kutegemea na familia husika. Ila kwa mtazamo wa ujumla naweza kusema hivi ndivo ilivyozoeleka. Sasa mara nyingi baba anakuwa mkali kwa watoto inafikia hatua mtoto akimuona baba amerudi kutoka kazini badala ya kufurahia ndio anasikitika. Anamsalimia then anatafuta sehemu ya kujificha. Well, hili si tatizo sana maana sometime inakuwa ni nature ya mtu kwamba anakuwa yupo hard kwa kila mtu hata kwa familia yake.

Sasa tatizo linakuja pale huyu baba ambaye hana ukaribu na wanae pale anapojikuta amemchapa mwanae kimakosa au kampiga kimakosa then kwa sababu yupo too superior anaona kuomba msamaha kwa mwanae ni udhaifu. Akijiangalia kwa jinsi anavyo behave then aseme samahani....anaona duh hii nitakuwa nimejishusha hadhi yangu. Anaamua kunyamaza tu na kuendelea na maisha kama kawaida.

Sasa ubaya wake ni kwamba mtoto nae anakulia katika mazingira kama hayo. Hajafundishwa kuomba msamaha na hajawahi kuombwa msamaha. Hali hii inakuwa inaendelea kutoka kizazi hadi kizazi. Mimi sidhani kama ni aibu au kujidhalilisha kama ukiamua kuomba msamaha pale unapofanya makosa hata ka wale waliokuzidi umri. Ndio inakuongezea heshima maana binadamu mara nyingi tunakumbukana kwa mabaya so watu wanapokuzungumzia pale ulipochemsha basi watasema pia kuwa uliomba msamaha. Mimi kwa mtazamo wangu nadhani ndio inaongeza utu wako mbele za watu.

Anyway point ya muhimu niliyotaka kuisema ni kwamba mara nyingi kuomba msamaha kwa mwanao inakauwa ni vigumu zaidi kama utatengeneza umbali kati yako na watoto wako. Ikishakuwa hivyo kama ukimfanyia makosa mwanao kuomba msamaha inakuwa ni kazi ngumu sana. Kuna familia moja naifahamu ambayo baba na mama huwa wanashindana kutengeneza ukaribu na watoto wao hali ilinivutia sana sio siri. Hope kwamba we can adopt some ways of living from other families. Hii haimaanishi kuwa upo dhaifu. Kwa sababu be sure kwamba zipo pia familia ambazo pia zina adopt some ways of life from you.


Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
JE NI SAWA BABA KUMUOMBA MSAMAHA MWANAE
JIBU KUHUSU CHUO CHA UZOEFU
Je kuzaliwa kwa mtoto kunapunguza mapenzi?
CHUO CHA UZOEFU.
JE NI SAWA KUMRUHUSU MTOTO WAKO KUWA NA BOYFR
Make Your Man Feel Appreciated
Msukosuko wa vyombo vya fedha duniani na madhara yake kwa Tanzania
Dating Your Coworker Or Boss, Is This A Good idea?
Should Tanzania worry about the credit crunch
Five Ways To Successfully Negotiate A Salary

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news