Blogs
 
ARTICLES
Iddy Mwanyoka     Email : mwanyoka@nifahamishe.com     
Mkutano wa G-20 Unamuhusu vipi Kibwana?
             
Mpasuko wa uchimi unazidi kutishia nchi zilizo endelea na zile zinazoendelea. Wachumi mbali mbali duniani wamekuwa mstari wa mbele kutoa njia mbadala zitakazo weza kuponya chumi kuu za dunia. Marekani na Uingereza wakiwa mstari wa mbele kushauri nchi nyingine tajiri kukopesha benki binafsi ambazo zimekubwa na mtikisiko. Huku Ufarasa na Ujerumani zimekuwa zikipingana na njia kumwaga pesa kwa mabenki, na kupendekeza sheria kali zipitishwe dhidi ili kuepusha swala kama ili kutokujirudia. Haya yote ni kutoka kwa nchi kubwa dunia, swala linakuja jee Kibwana au Mwaipopo mkutano wa G-20 unamuhusu nini?

Katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka Mh. Jakaya Kikwete ameendelea kuwapasha Watanzania kuhusu swala zima la mpasuko wa uchumi wa dunia. Swali kubwa ambalo Watanzania wengi wanajiuliza ni kwamba jee uchumi wa duniani unaniusu nini mimi Kibwana? Pato langu la kila siku linategemea samaki kutoka bahari ya hindi, mvua toka kwa mungu na mbegu ambazo nimetunza tangu msimu uliopita. Ukweli ni kwamba nchi za Africa hazijajiunga moja kwa moja na mfumo wa fedha wa nchi za Magharibi na Asia, hata hivyo haziwezi kuepuka mpasuko huu wa fedha kwa sababu zifuatazo.

Serikali nyingi za Africa zinajiendesha kwa kutumia misaada kutoka kwa nchi zilizoendealea. Mfano Tanzania inategemea wadhamani kwa zaidi ya asilimia 40 ili kuendesha bajeti yake ya kila mwaka. Hivyo basi kama wadhamani wapo katika shida ya kifedha ni dhahili kabisa moja ya matumizi watakayo punguza ni misaada kwenda kwa nchi zinazoendela. Kutoweza kupata misaada hii kutapunguza uwezo wa serikali kudhamini baadhi ya huduma za msingi kama Afya, ujenzi wa barabara na huduma nyingine za msingi ambazo Kibwana anazitumia kila siku.

Pili, serikali nyingi za Africa zinategemea utalii kama moja ya chanzo cha kuingiza pato kwa nchi husika. Utalii ni sekta kubwa sana kwa nchi nyingi za Africa, kwa Tanzania utalii unachingia 10% katika pato la taifa. Kutokana na kuyumba huku kwa uchumi watalii kutoka nchi za Marekani na Ulaya wamepungua kwa kiasi kikubwa. Swala hilo linatishia kuiathiri sekta hii ya utalii, ambayo inamchango mkubwa sana wa maendeleo katika mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

Tatu, serikali nyingi za Africa zinaetemea uchumi unaondeshwa na usafirishaji wa malighafi nje ya nchi. Malighafi hizi ni pamoja na dhahabu, tanzanite na mazao mengi ya biashara. Kuyumba kwa uchumi katika nchi za magahari kutanasababisha matakwa (demand) malaghafi hizi kupungua na matokeo yake pei ya malighafi hizi kushuka (Kutokana na mfumo wa demand and supply). Madhara ya kushuka kwa bei za malighafi ni pamoja na kupunguza pato kwa taifa. Na mwisho wa siku ni nchi kupunguza matumizi katika huduma mbali mbali.

Mambo haya matatu yanamuathiri Kibwana na Mwaipopo moja kwa moja. Ukweli ni kwamba tatizo hili la uchumi halijapatiwa dawa mpaka sasa. Raisi mpya wa Marekani, Barack Obama ameshatumia takribani $2 trillion kujaribu kuponya uchumi wa Marekani, lakini wataalamu wa uchumi wanasema kwamba swala hili bado halijafika hata nusu. Ni mategemeo yangu kwamba nchi kama Tanzania itapunguza matumizi yake katika sekta ambazo hazina umuhimu sana, na kuhifadhi kiasi itakacho save kwa baadae. Ukweli ni kwamba mpasuko wa uchumi unatisha, na hakuna dawa mpaka sasa. Macho yote ni kwa G-20.


Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
Mkutano wa G-20 Unamuhusu vipi Kibwana?
Foreign Aid: glaucoma to Tanzania
WHY CAPITALISM FAILED IN AFRICA?
World Bank is Not a Solution
HOW IMF & WORLD BANK FAILED IN AFRICA
Mfumo Wetu Wa Elimu Ndio Chanzo Cha Umasikini
Jee EAC ni Dawa ya Matatizo ya Nchi Zetu
Macho Yote Kwa Obama
Mpasuko wa mfumo wa fedha duniani je ni mwisho wa dolla?
10 Jobs That Pay $30 An Hour

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news