Blogs
 
ARTICLES
Iddy Mwanyoka     Email : mwanyoka@nifahamishe.com     
Macho Yote Kwa Obama
             
Takribani siku 14 tangu Marekani ichague raisi wao wa arubaini na nne. Matumani bado ni makubwa sana ndani na nje ya Marekani.

Jee nini Raisi huyu kijana atafanya ili kubadili mfumo mzima wa Uchumi wa Marekani, kubadili mfumo mzima wa sheria za America kwa nchi nyingine (US foreign policy)?. Kwa upande mwingine pia nchi za Africa nazo zinatazama jee mtoto wao nini atafanya kusaidia bara la giza.

Ukweli ni kwamba raisi Obama ana mengi ya kufanya ndani ya Marekani kabla hajawaza lolote kuhusu nje ya Marekani. Kwa kuanzia tuu siku 100 za kwanza ndani ya serikali yake Mh. Obama atatazama kwa karibu kabisa maswala makuu mawili nayo ni Usalama na Ulinzi wa Marekani na lapili ni hali ya Uchumi wa Marekani.

Kwenye swala zima la Ulinzi na Usalama wa Marekani Mh. Obama ana kazi kubwa ya kufanya. Moja raisi Obama anakabiliwa na swala zima la uzalishaji nuclear wa nchi ya Iran. Hili ni swala zito na lenye kutishia ulinzi na usalama wa Marekani na marafiki zake kama Israel. Swala hili ni zito sana sababu Amerika haiwezi kuruhusu Iran kumiliki nuclear. Swala la pili ambalo linamkabili raisi Obama ni kufunga jela la Guantanamo ambayo imeshikilia wafungwa wa kivita. Swala hili ni zito sababu jela hii ina wafungwa takribani ya 250, ambao badhi yao wanaweza kukutwa walikuwa na makosa madogo hivyo wanapaswa kuachiliwa. Swali kubwa ni jee unawapeleka nchi gani? Swala latatu ni vita ya Iraq, jee raisi Obama atarudisha wanajeshi wote wa Marekani walioko ndani ya Iraq ifikapo mwishoni 2010? Swala kubwa la kuangalia ni jee kwa kufanya hivyo atakuwa analinda maslai ya Marekani? Ukweli ni kwamba Marekani imewauzia vifaa vingi sana vya kijeshi nchi ya Iraq, na kuwaacha tuu wawe na silaa zote hizi huko mfumo wao mzima wa siasa bado haujatengemaa ni swala gumu sana linalomakabili raisi Obama. Swala la nne ni Afrighanstan, jee ni mfumo gani Serikali ya raisi Obama itatumia kupambana na wahasi wa Taliban ambao wanapata nguvu kila siku zinapopita. Jee raisi Obama atatumia nguvu kuingia kwenye mpaka wa Afrighanstan na Pakistani?

Kwenye swala zima la uchumi hapa ndipo kila mtu anamtazama kwa macho mawili. Ukuaji waUchumi wa duniani unaonekana kupungua, na labda unaweza kusimama kwa muda mrefu (baadhi ya wachumi wanakadiria ni miezi 14). Makampuni mengi yanapunguza idadi ya wafanyakazi, hivyo kuongeza idadi ya Wamarekani wasio na kazi. Uchumi wa Marekani unandeshwa na wafanyakazi, hivyo kuongezeka kwa idadi ya watu wasio na kazi ni swala linalitishia uongozi wa Obama. Vile vile macho yanatazama kuhusu swala zima la kuyasaidia makampuni ya matatu Kimarekani yanayo tengeneza magari. Jee raisi Obama atazuia kampuni hizi kubwa tatu zisife? Na la mwisho ni mchakato mzima wa mikopo ya nyumba ambao ni chanzo cha mlipuko huu mzima unaotishia uchumi wa dunia. Jee raisi Obama atatengeneza mfumo wa mpito utakao saidia watu wanaoshindwa kulipa kodi zao za nyumba wasinyang’anywe nyumba zao na mabank?

Haya ni mambo machache yanayo mkabili raisi Obama katika siku 100 za kwanza za uongozi wake. Hata hivyo zaidi ya asilimia 70 ya Wamarekani wanaamini kwamba raisi Obama anaweza kuirudisha Marekani katika njia njema. Katika hatua za mwanzo tumeona jinsi Obama anavyo tumia njia alizotumia raisi wa kumi na sita wa Marekani Abraham Lincoln ambae anatokea jimbo mmoja na raisi Obama. Moja njia hizo ni kuchanganya watu mbali mbali kwenye baraza lake la mawaziri pasipo kujali itikadi zao za kisiasa. Tumeona uwezekano wa kumpanga mama Clinton kama waziri wake wa mambo ya nje. Mama ambae alimchezea rafu mbaya sana wakati wa awali wa kampeni za uchaguzi. Hivyo japokuwa njia ya kwenda kwenye ardhi ya ahadi ni mbovu, lakini bado Wamarekani wana imani kubwa sana na kiongozi wao.


Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
Mkutano wa G-20 Unamuhusu vipi Kibwana?
Foreign Aid: glaucoma to Tanzania
WHY CAPITALISM FAILED IN AFRICA?
World Bank is Not a Solution
HOW IMF & WORLD BANK FAILED IN AFRICA
Mfumo Wetu Wa Elimu Ndio Chanzo Cha Umasikini
Jee EAC ni Dawa ya Matatizo ya Nchi Zetu
Macho Yote Kwa Obama
Mpasuko wa mfumo wa fedha duniani je ni mwisho wa dolla?
10 Jobs That Pay $30 An Hour

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news