Blogs
 
ARTICLES
Kassim Baruani     Email : kasbaru@nifahamishe.com     
Safari ya kilomita 1000...
             
Ni suala linalofahamika kwamba kila kitu kina mwanzo.Na kama walivyosema wahenga,’mwanzo mgumu’.Watu wengi hukata tamaa na kuishia njiani pale wanapokutana na ugumu au vikwazo mbalimbali katika kujaribu kufanya jambo fulani.Matokeo yake ni kwamba wanaendelea kubaki pale pale walipokuwa,bila hata ya kupiga hatua yoyote mbele,na mara nyingi ukweli ni kwamba wanakuwa wamepiga hatua kurudi nyuma,hasa pale utakapojumuisha katika mahesabu muda na nguvu walizozitumia katika kujaribu jambo hilo.

Tukiangalia kwa makini tutaona kwamba karibu watu wote waliopata mafanikio makubwa katika mambo mbalimbali walifanya juhudi kubwa sana mpaka kuweza kufika hapo walipo,ikiwa ni pamoja na kukabiliana na vikwazo mbalimbali walivyokutana navyo njiani.Kama wao waliweza kwanini na sisi tusiweze?

Kitu cha muhimu ni kujiamini,kuwa na mipango madhubuti,adabu katika jambo unalolifanya na juhudi.Kitu chochote kizuri hakipatikani bila kukitolea jasho.Na pia mtu yeyote anaweza kufanikiwa katika kile anachokifanya kama atafanya juhudi kiasi cha kutosha.
Siku zote tukumbuke kwamba safari ya kilomita 1000 huanza na hatua moja.


Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
WAZAZI:WALIMU NA MARAFIKI WA KWANZA WA WATOTO
KITENDAWILI
DEMOKRASIA YA KWELI
Safari ya kilomita 1000...

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news