Blogs
 
ARTICLES
Iddy Mwanyoka     Email : mwanyoka@nifahamishe.com     
Mpasuko wa mfumo wa fedha duniani je ni mwisho wa dolla?
             
Marekani ni moja nchi maarufu sana hapa dunia kwa mfumo thabiti wa fedha (Financial Syestem). Mfumo wa huu ambao umesimama zaidi ya miaka mia moja, umekubwa na majanga mengi katika nyakati mbali mbali.

Mwishoni mwa mwaka wa 1920 kulitegwa bomu ambalo liliuwa zaidi ya watu 38 na kujerui wengine 300, lakini janga hili halikutetemesha mfumo wa fedha.

October 29, 1929 Marekani ilikubwa na pigo kubwa sana na kupelekea mfumo mzima wa fedha wa Marekani na duniani nzima kuanguka. Tukio hii ni maarufu sana kama Great Depression.

Marekani ikiwa chini ya rais wao Franklin D. Roosevelt maarufu kama FDR iliweza kuandaa mbinu mpya za kupambana na muanguko huu wa kifedha, mbinu hizo zilijulikana kama New Deal.

Tume nyingi zilianzishwa kwa kupitia mfumo huu wa New Deal na vile vile shughuli nyingi sana za kiuchumi zilianzishwa, moja kati ya shughuli hizo ni ile ya Tennessee Valley Authority (TVA) ambayo ni maarufu sana kwenye somo la jeografia nchini kwetu Tanzania.

Hivyo baada ya kuanzishwa kwa New Deal, Marekani iliweza kusimama na kuendelea kuwa kiongozi wa dunia kwenye swala zima la mfumo wa fedha. Sheria nyingi sana za kuongoza mabanki ziliwekwa, sheria maarufu ni ile ya Glass Steagall Act ya mwaka 1933.

Sheria hii ilizuia mabanki yote kujiusisha na kuwekeza kwenye biashara zenye risk kubwa. Mabanki yazuiliwa kabisa kuwekeza kwenye shea za kampuni yoyote.

Hii ilisababishwa kuanzishwa kwa banki zinazohusika na kuwekeza tuu (Investement Bank). Banki (commercial) zilibakia na biashara moja tuu nayo ni kukopesha.

Mfumo huu uliendelea mpaka miaka ya 1980, ambapo mabanki mengi ya marekani yaliendelea kulalamika kwamba Bunge la Marekani linawanyimwa uhuru wa kushindina kibishara.

Mwaka 1976 Marekani ilipata mlipuko wa watu kununua nyumba maarufu kama real estate boom. Hivyo banki nyingi zilizokuwa zinajishirikisha na kuweka na kukopa yaani Saving and Loan Bank zilijiusisha moja kwa moja na mlipuko huo wa nyumba.

Kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1980 mlipuko wa bei (Inflation) uliingia Marekani hivyo kupelekea kampuni hizi zilizojiusisha na kuweka na kupa kuanguka na kufa. Tatizo hilo ni maarufu kama S&L crisis. Hata hivyo Marekani ilisimama kidete na kulishinda janga hili.

Mwaka 2001 Marekani iliadhibiwa na ugaidi, na moja kati ya vitega uchumi vyake viliathiriwa na swala zima la ugaidi.

Serikali ya Marekani iliingilia kati na kufunga soko la shea Wall Street Market. Lakini siku chache baadae mfumo wa fedha wa Marekani uliamka na maisha ya kila siku yaliendelea.

Mwaka 1970 serikali ya Marekani ilianzisha shirika mfano wa shirka la nyumba (Federal Home Loan Mortgage Corporation) maarufu kama Feddie Mac, ambalo kazi yake ilikuwa ni kununua mikopo ya nyumba kutoka kwa ma banki, na kisha kuzitengeneza kama shea na kuziuza kama “ Mortagage-backed Security”.

Chombo hichi kazi yake kubwa ilikuwa ni kuongeza mzunguko wa fedha kwenye banki. Sababu mikopo mingi ya nyumba ni ya miaka 30, na riba yake huwa haoingezeki.

Hivyo bank nyingi haziwezi kushikilia deni kwa miaka 30, na ndio maana Feddie Mac ilianzishwa ili kununua madeni haya na kisha kuwauzia wawekezaji.

Mwishoni mwa miaka ya 1990, serikali ya Marekani ilipitisha sheria za kupunguza sheria za kuangalia banki, na moja kati ya sheria walio futa ni Glass Steagall Act ya 1933. Hili ilizipa nafasi banki za Marekani kuwekeza kwenye njia nyingi kasoro kwenye soko la shea.

Part II ya makala hii inakuja karibuni


Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
Mkutano wa G-20 Unamuhusu vipi Kibwana?
Foreign Aid: glaucoma to Tanzania
WHY CAPITALISM FAILED IN AFRICA?
World Bank is Not a Solution
HOW IMF & WORLD BANK FAILED IN AFRICA
Mfumo Wetu Wa Elimu Ndio Chanzo Cha Umasikini
Jee EAC ni Dawa ya Matatizo ya Nchi Zetu
Macho Yote Kwa Obama
Mpasuko wa mfumo wa fedha duniani je ni mwisho wa dolla?
10 Jobs That Pay $30 An Hour

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news