Blogs
 
ARTICLES
Yona Maro     Email : yona_maro@nifahamishe.com     
Je unajua jinsi ya kujilinda unapotembelea tovuti kama Facebook au hi5?
             
Kama wewe ni mtembeleaji wa Tovuti kama Facebook pamoja na Hi5 utakuwa umeona baadhi ya vijimambo vinavyoendelea katika tovuti hivyo, mfano unapojiunga na tovuti hizo inakuwa na sehemu maalumu ambayo inakuwezesha wewe kujiunga na account yako ya yahoo au google ili uweze kualika marafiki zako wengine waliokuwa katika contacts zako za
hiyo yahoo mail au google unapojiunga pale na kweli rafiki zako hao wote watapata hiyo mialiko yako na wengi watakuja kujiunga na wewe kama ni facebook au hi5 au tanged huu ndio ulimwengu wa sasa ambapo
kumtafuta mtu wakati mwingine ni rahisi zaidi kuliko anavyofikiria
ukiingia katika tovuti hizo za kijamii unaweza kumtafuta mtu huyo kama ameweka taarifa zake sahihi .

Wakati ambapo mashirika mengi ya kijasusi duniani yakitumia mitandao hii ya kijamii kwa ajili ya taarifa zao za kila siku , kama kujua Fulani anayetumia jina Fulani yuko wapi na anafanya nini au anawasiliana na nani ameweka tarifa gani katika account yake ya facebook au hi5 na ndio magenge mengi ya kihalifu pia yanatafuta watu
wa kushirikiana nao katika uhalifu wao katika nchi kadhaa duniani, wengi wanatumika bila wao kujua au kwa kujua ingawa takwimu zinaonyesha wengi wanaingizwa bila wao kujua kama wanatumika katika uhalifu wa aina Fulani.

Unapopata barua pepe kutoka facebook ambayo inatakiwa kuja kwako moja kwa moja inaingia katika sanduku la barua pepe yako kama ni yahoo au hotmail , unapotaka kuangalia ujumbe huo inakufungulia katika window
nyingine au tab nyingine inategemea wewe unavyotaka lakini mara nyingi huwa zinafungua moja kwa moja pamoja na password yako , hii ina
maanisha kama ulikuwa sehemu ambayo mtandao unaenda taratibu ukaamua kuondoka zako ukaacha kazi zako hapo mwingine anaweza kuja kukaa katika computer hiyo na kufungua kile ulichotaka kufungua wewe na kufanya kazi zake au na kufanya uharibifu hata kwenye profile yako kama alikuwa na nia hiyo mbaya .

Katika makala yangu mmoja kuhusu usalama wa mitandao ya mawasiliano haya niliwahi kusema vyombo vyetu vya usalama viwe na watu maalumu ambao wanawaweka katika mitandao hii kwa ajili ya kufanya kazi maalumu nayo ni kujiunga katika vikundi mbali mbali katika mitandao hii kwa
ajili ya kupata taarifa na kujua watu wengi zaidi katika dira mbali mbali za kujenga au za kubomoa jamii mbalimbali.

Kuna jambo ambalo niliwahi kuhisi huko nyuma kwamba inawezekana kabisa huu wizi katika ATM inawezekana mawasiliano kati ya wahalifu hawa yanafanyika kwa njia ya mitandao hii jamii na sio kwa njia ya barua pepe za kawaida ambazo watu wamezoea , mimi sio mtaalamu sana katika mawasiliano ya Barua pepe lakini unapotumia barua pepe ni rahisi zaidi
mtu kuweza kukubamba kuliko unavyofanya mawasiliano kwa njia ya mitandao jamii kama facebook au hi5 .

Mwaka jana katika moja ya Somo langu niliwahi kufanya utafiti kuhusu watu na tabia zao wanapotumia mitandao hii , imeonyesha kwamba unapojiingiza katika mitandao jamii hii ni rahisi sana kuweza kujua tabia za watu haswa zilizojificha na hata kujua vitu anavyopenda yeye haswa kama unatumia jinsia bandia haswa za kike wahalifu wengi wa Nigeria wanatumia jinsia za kike ingawa wao ni midume na kwa njia hiyo wamefanikiwa kulaghai wengi sana haswa wanaopenda mijimama ya kizungu au wale wanaopenda safari za ulaya ua njia rahisi za kujipatia kipato

Ukiacha facebook na hi5 kwa sasa kuna mwingine umekuja kwa kasi sana nao ni twiter , mitandao hii haswa twiter inaonyesha inaweza kufunika kabisa shuguli za blogu na forums zingine huko mbeleni kama forum hizi na blogu hizi hazijajiimarisha zaidi kibiashara na kuwa na vitu vya kibunifu zaidi kuliko ilivyo sasa hivi , nafikiri kinachoweza
kufanyika zaidi ni kwa kampuni kubwa katika google kununua zinazochipukia kama twitter , au tanged pamoja na tovuti zingine zinazotoa huduma za mawasiliano na vikundi vya kijamii .

Ni hilo tu kwa leo , kwahiyo ndugu unapotumia hizi browser za mitandao haswa katika internet café uwe makini sana uangalie kama unaacha chochote kama reference katika browser catch za computer hizo, uhalifu mwingi sana katika mitandao siku hizi unafanyika kwa watu kuacha reference hizo ambazo wengine wanaweza kuzitumia kushambulia
sehemu zingine au hata kuweza kukushambulia wewe binafsi

Kwahiyo huko makazini mwetu tunapofanya kazi pia hakikisha huachi reference ukiacha mashambulizi hayo , hata documents nyingi nyeti zinaibiwa kwa njia hii au ambazo zinahusiana na hizi , kama unavyoona hapo uhusiano wa mtu anapotumia mitandao hiyo jamii halafu mwisho inavyokuja kujihifadhi katika catch ya browser yake ya chrome hapo
anakuwa amepatikana kwa kiasi kikubwa

Naamini kwa kiasi kikubwa watengenezaji wa browser sasa wanafanya jitihada za dhati kuimarisha usalama wa mitandao hii.

Kuna mengi ya kuandika ila kwa leo nitaishia hapa.


Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
Je unajua jinsi ya kujilinda unapotembelea tovuti kama Facebook au hi5?
Usiingie kichwa kichwa, Hii ni kwa usalama wako
Tutumie Runinga Kuleta Mapinduzi Katika Utoaji Wa Elimu
Jamii Ijihadhari na Soko Huria
Hakuna Mtetezi wa mapambano ya Wananchi
MAPINDUZI BILA KUMWAGA DAMU

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news