Blogs
 
ARTICLES
Yona Maro     Email : yona_maro@nifahamishe.com     
Jamii Ijihadhari na Soko Huria
             
Mfumo wa biashara ya soko huria tunaojaribu kuujenga unahitaji uangalifu na umakini wa hali ya juu sana. Uhai wa biashara yoyote inayotegemea nguvu ya soko ni masoko yake (wateja) . Baadhi ya’vigogo’ wanaitumia dhana ya soko huria kucheza rafu. Wanaigeuza jamii yetu kuwa soko la biashara za hovyo wanazobuni. Matokeo yake wanaiangamiza jamii nzima kwa manufaa yao binafsi.

Tangu sheria ya vyombo vya habari irekebishwe na watu binafsi waliporuhusiwa kushiriki katika sekta hii muhimu ya habari, tumeshuhudia utitiri wa magazeti, radio binafsi, na vituo vya Televisheni.

Vyombo hivyo vya habari viliingizwa kwa kasi nchini kwa malengo ya kibiashara zaidi ya kutoa huduma kwa jamii. Ndiyo maana habari zinazoandikwa au kutangazwa na vyombo hivyo ni zile zenye kusisimua na zinazokidhi haja ya masoko tu jamii itanufaikaje na habari zinazoandikwa au makala siyo jambo muhimu.

Kuna baadhi ya magazeti hapa nchini ni maalumu kwa masuala ya ngono na ukahaba. Na jamii yetu imefikishwa mahala kukubali kashfa hii kama jambo la kawaida. Magazeti hayauziki bila ya kuandika kashfa za ngono! Hayapendwi sharti kuwepo mikasa ya machangudoa na wateja wao! Hayafurahishi mpaka kuwe na michoro ya vikatuni vizinifu! Hivi jamii inapolishwa uchafu huu nini matarajio ya baadaye? Tunataka kujenga taifa la wazinzi? Magazeti kama chombo cha habari yanatabia ya kudhibiti fikra za wasomaji.

Ukisoma mambo ya kihuni mara kwa mara akili yako nayo inahamia huko huko. Inaogopesha kuona kuwa magazeti yanayoandika habari za uzinzi (sensetional) yanakumba wasomaji wengi. Tafsiri yake jamii inasoma kwa bidii sana mambo ya kihuni na yasiyokuwa na maana.

Jamii imegeuzwa soko la habari za kihuni na kijinga bila ya kutambua.

Janga la ukimwi linalotishia maisha ya Watanzani walio wengi limetumiwa kama chachu ya biashara haramu ya kondomu. Viongozi wa ngazi ya juu wa taifa wamekuwa wakiwahamasisha wananchi watumie kondomu kujikinga na ukimwi.

Jamii ya Watanzania imeingizwa kwenye ‘mkenge’ na viongozi wao wa taifa kuhusu matumizi ya kondomu; na hivi sasa wananchi wako katika hatari ya kuambukizwa.

Viongozi wanatamba kwamba kampeni ya kudhibiti ukimwi imefanikiwa kwa sababu mamilioni ya kondomu yameshauzwa nchini! Mauzo ya kondomu ndiyo kipimo cha kudhibiti ukimwi! Jamani! Hiki ni kigezo biashara ya kondomu ina soko kiasi gani na wala siyo mafanikio ya kudhibiti ukimwi. Watanzania tunageuzwa soko la kondomu wala hatugutuki! Wataalamu wa ukimwi wameshaongea mara nyingi sana kwamba kondomu siyo kinga ya ukimwi. Ukimwi hauna kinga wala tiba. Lakini viongozi wetu, vyombo vya habari, na jamii nzima ya Watanzania hatuna utamaduni wa kuzingatia mambo ya kitaalamu. Tumekuwa hodari wa kusoma ‘songombingo’ tu bila ya kupitia makala zinazoandikwa na wataalamu. ‘Vigogo’ wanaisaliti jamii kwa kutosema kweli kuhusu udhaifu wa kondomu. Wanaogopa kupoteza masoko ya mradi huu.Tusipoachana na uasherati; hata tukivaa ‘tube ya baiskeli’ wachilia mbali kondomu, ukimwi utatumaliza tu!

Ulipoanzishwa mradi wa ‘Speed-governor’ hoja ilijengwa kwamba lengo lilikuwa kudhibiti ajali za barabarani. Debe lilipigwa na viongozi wa taifa mpaka wananchi wakakubali kuwa ufumbuzi wa ajali za barabarani umeshapatikana.

Wenye mabasi na magari mengine ya abiria walishinikizwa kununua ‘speed-governor’ kwa gharama kubwa la sivyo magari yao hayataruhusiwa kufanya shughuli. Bada ya magari kufungwa ‘Speed-governor’ ajali zilipungua au kwisha ? tunaomba ripoti ya jeshi la polisi pamoja na wadau wa usafirishaji . Kila siku tunashuhudia ajali mbaya na za kutisha . Wenye mabasi na wananchi walifanywa soko la miradi ya watu! Mbaya zaidi vyombo hivi vilinunuliwa kwa gharama kubwa na nisharti ufunge katika gari lako. Nani anayefaidika?.

Siku za karibuni katika barabara za mkoa wa Dar es salaam barabara zilipanuliwa na kuwekwa njia tatu , watu wakazidi kugongwa na ajali kuongezea waliohusika na mradi huu mpaka leo hatujapata ripoti ya maandishi kuhusu kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa mradi huu toka uanze

Katika miaka ya nyuma tulikuwa hatujui kama kuna biashara ya madawa ya kulevya ulimwenguni. Kwa kawaida biashara hii hufanywa na watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha na wenye nyadhifa mbalimbali. Tujiulize hawa ‘vigogo’ wanaofanya biashara hii haramu wamepataje soko la biashara hii katika jamii yetu? Wako tayari kuliachia soko lao hili? Soko limebuniwa kwa kumomonyoa maadili mema ya jamii na kuingiza ya ajabu ajabu . Soko lao linapanuka zaidi kadri tunavyoendelea kukumbatia mila na desturi mbovu. Vita dhidi ya madawa ya kulevya haitafanikiwa iwapo maadili mema ya jamii yataachiwa yatoweke.
Kuna lingine hili jipya la kuruhusu watu binafsi waendeshe biashara ya silaha nchini. Hoja inayojengwa ni kwamba; "Serikali inajitoa katika biashara na kuiachia sekta binafsi.


Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
Je unajua jinsi ya kujilinda unapotembelea tovuti kama Facebook au hi5?
Usiingie kichwa kichwa, Hii ni kwa usalama wako
Tutumie Runinga Kuleta Mapinduzi Katika Utoaji Wa Elimu
Jamii Ijihadhari na Soko Huria
Hakuna Mtetezi wa mapambano ya Wananchi
MAPINDUZI BILA KUMWAGA DAMU

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news