Blogs
 
ARTICLES
Mwajabe Kizigina     Email : kizigina@nifahamishe.com     
JIBU KUHUSU CHUO CHA UZOEFU
             
Siku chache za zilizopita nilitoa mada moja kuhusu kuanzishwa kwa chuo cha uzoefu kwa ajili ya young proffessionlas wanaomaliza university. Sasa niliitoa mada hii na sikujua haswa nini kifanyike katika swala zima la kuwasaidia vijana ambao hawana uzoefu wa kazi ambao kwa kiasi kikubwa wanakutana na hili balaa la kutopata kazi kila sehemu wanazoenda kupeleka maombi yao…

Nilikaa chini na kujaribu kuwaza kwa makini haswa tunaweza kuwasaidia vipi vijana wetu. Katika kujaribu kupekua kurasa mbali mbali katika tovuti tofauti nikaja kuona jambo moja ambalo linavutia kwa kiasi fulani. Nikaona kuwa katika nchi zilizoendelea wanatoa kazi kwa vijana wapya waliomaliza Vyuo vikuu au Technical Schools ikiwa kama long term internship au pia wanaiita carrier training.

Hii inaweza kuwasaidia vijana ambao wamemaliza kwenda abroad for atleast two years ambayo ndio muda inayochukua the whole program. Na katika kuangalia angalia nikaona kuwa kuna baadhi ya nchi wanataka watu wenye atleast uzoefu wa mwaka au less but not fresh from the university na kuna baadhi ya nchi hawahitaji uzoefu wowote zaidi ya internship uliyoifanya wakati ukiwa mwanafunzi.

Sasa kutokana na mtazamo wangu nadhani hii ni moja ya solution kwa baadhi ya vijana ambao wanaweza kwenda abroad kutafuta ujuzi. Kwani unapokuwa na CV ya abroad ni rahisi zaidi kupata kazi nyumbani hata kama uzoefu wako ni wa mwaka mmoja au miwili. Hapa sitatoa details zozote za maana kuhusu process na upatikanaji wa hizo internships kwa sababu zipo nyingi mno ni kiasi cha mtu kuingia net na kutafuta kwa utulivu.

Bado naendelea kuumiza kichwa changu juu ya swala hili na wakati ukizidi kwenda nategemea nitapata ufumbuzi mwingine tofauti. Na kama kawaida ya nifahamishe ipo kwa ajili ya jamii kwa sababu hiyo tutaendelea kuwatafutia solutions za mada tofauti katika siku za usoni.


Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
JE NI SAWA BABA KUMUOMBA MSAMAHA MWANAE
JIBU KUHUSU CHUO CHA UZOEFU
Je kuzaliwa kwa mtoto kunapunguza mapenzi?
CHUO CHA UZOEFU.
JE NI SAWA KUMRUHUSU MTOTO WAKO KUWA NA BOYFR
Make Your Man Feel Appreciated
Msukosuko wa vyombo vya fedha duniani na madhara yake kwa Tanzania
Dating Your Coworker Or Boss, Is This A Good idea?
Should Tanzania worry about the credit crunch
Five Ways To Successfully Negotiate A Salary

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news