Blogs
 
ARTICLES
Mwajabe Kizigina     Email : kizigina@nifahamishe.com     
Je kuzaliwa kwa mtoto kunapunguza mapenzi?
             
Siku kadhaa zilizopita katika pita pita zangu mtaani nilikutana na rafiki yangu mmoja mkongwe akaniambia kuwa tangu waridi wake alipojifungua basi kila siku anakuwa na wasiwasi na mtoto wao tu. Akaniambia kuwa ni kweli kupata mtoto ilikuwa ni muhimu katika ndoa yao ila Mrs alikuwa yupo too busy na mtoto kiasi kwamba jamaa akahisi kuwa amesahaulika.

Nikakaa nakufikiria kama shemeji yangu yupo sawa au rafiki yangu dio mwenye makosa. Haikuwa rahisi kupata jibu ikabidi niulize ili nipate mawazo ya watu tofauti kutokana na swala hili. Kila mmoja alitoa mawazo ambayo yalilenga zaidi kujipa upendeleo yeye mwenyewe. Mwishowe nikaelewa kuwa shemeji yangu hakuwa na makosa…endapo mapenzi yale ambayo mama anamuonesha mtoto na baba pia angekuwa nayo wala kusingekuwa na kujisikia kuwa umesahaulika.

Nyingi ya familia zetu za kiafrika mtoto anakuwa anaangaliwa mara anapokuwa mchanga ila akishakua kidogo tu ukaribu wa mtoto na mzazi zaidi mzazi wa kiume unapongua siku hadi siku. Zaidi unabaki uhusiano kati ya mama na mtoto tu. Sasa swala hili la kuanza kujenga masafa kati ya baba na mtoto matokeo ni kwamba baba anakuwa hamjui mwanae na mara atakapohitaji kujua chochote anaenda kumuuliza mkewe. Hajui kuwa umbali alishaujenga tangu kitambo.

Mi nafikiria kwamba mapenzi mtoto anayoyapata kutoka kwa mama yawe sawa na yale atakayoyapata kutoka kwa baba. Si udhaifu kumpenda au kuonesha kama wampenda sana mwanao. Ila kuna kitu kimoja pia hapa. Mara nyingine mama anashika ujauzito bila ya kupanga na mumewe kisa marafiki zake wana watoto. Hii sasa si sawa. Na hii pia inachangia kujenga umbali kati ya baba na mtoto atakayezaliwa.

Namalizia kwa kusema kwamba watoto ndio wanaofanya ndo iweze kuwa imara. So si kila wakati mtu ujifikirie mwenyewe tu wakati familia ni zaidi ya wewe na mkeo. Familia ni pamoja na watoto.Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
JE NI SAWA BABA KUMUOMBA MSAMAHA MWANAE
JIBU KUHUSU CHUO CHA UZOEFU
Je kuzaliwa kwa mtoto kunapunguza mapenzi?
CHUO CHA UZOEFU.
JE NI SAWA KUMRUHUSU MTOTO WAKO KUWA NA BOYFR
Make Your Man Feel Appreciated
Msukosuko wa vyombo vya fedha duniani na madhara yake kwa Tanzania
Dating Your Coworker Or Boss, Is This A Good idea?
Should Tanzania worry about the credit crunch
Five Ways To Successfully Negotiate A Salary

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news