Blogs
 
ARTICLES
Mwajabe Kizigina     Email : kizigina@nifahamishe.com     
CHUO CHA UZOEFU.
             
Wiki hii nakuja na mada tofauti kidogo inayohusu new graduates. Kutokana na matatizo yaliyokumba soko la dunia kila sehemu utakayoenda kuomba kazi utakuta wanataka mtu mwenye atleast uzoefu wa miaka miwili.

Tukijaribu kuziangalia nchi zilizopo bara la Afrika, matatizo ya uchumi yapo tangu enzi na enzi. Of course si kila nchi ya Afrika ina matatizo ya kiuchumi ila nyingi hali yake ya kiuchumi si nzuri. Sasa hali imezidi kuwa mbaya kwa sababu hata nchi zinazotoa misaada Afrika na zenyewe masoko yao ya nje yameathirika kwa kiasi kikubwa. Kwa sababu hii makampuni mengi badala ya kuajiri wafanyakazi yanapunguza wafanyakazi kutoka kazini. Yapo baadhi ya makampuni machache ambayo still hali yao haijabadilika sana almost ipo the same.

Mbaya ni kwamba kama ni new graduate na ukaenda kuomba kazi wanasema uwe na uzoefu usiopungua miaka 2 au labda uwe na refa atakaye kuunganishia kazi. Sasa kama kila sehemu inahitaji uzoefu, je, itakuwaje kwa vijana wetu ambao ndio wamemaliza na wanataka kuanza kazi??

Wakati nilipokuwa naumiza kichwa changu kuhusu nini cha kufanya nikapata mdau mmoja ambaye na yeye ameshapoteza muda wake mwingi kutafuta kazi kila sehemu na kuniambia kuwa cha moto anakiona. Hivyo akaniambia kuwa angalau vingeazishwa vyuo au makampuni maalumu kwa ajili ya kuwapa new graduates experience. Ni vigumu kupata organization au company katikati ya tatizo hili la uchumi likachukua new graduates na kuanza kumtrain na kumlipa for 6 months for free. Ndio maana kupunguza unnecessary expenses wanachukua mtu mwenye experience ili aingie straight kazini.

Nini kifanyike? Hatuwezi kuwaacha vijana bila kazi, na hatuna marefa wa kuwasaidia vijana wetu waingie kazini. Na economic crisis hatujui itaisha lini. Kama super power zinaathirika basi sisi waafrika ndo tunaumia zaidi. Nini kifanyike?


Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
JE NI SAWA BABA KUMUOMBA MSAMAHA MWANAE
JIBU KUHUSU CHUO CHA UZOEFU
Je kuzaliwa kwa mtoto kunapunguza mapenzi?
CHUO CHA UZOEFU.
JE NI SAWA KUMRUHUSU MTOTO WAKO KUWA NA BOYFR
Make Your Man Feel Appreciated
Msukosuko wa vyombo vya fedha duniani na madhara yake kwa Tanzania
Dating Your Coworker Or Boss, Is This A Good idea?
Should Tanzania worry about the credit crunch
Five Ways To Successfully Negotiate A Salary

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news