Blogs
 
ARTICLES
Mwajabe Kizigina     Email : kizigina@nifahamishe.com     
JE NI SAWA KUMRUHUSU MTOTO WAKO KUWA NA BOYFR
             
Wakati nilipokuwa na umri mdogo kila nikijiuliza swali hili sipati jibu la moja kwa moja au ninakuwa na majibu tofauti kuhusu mada hii. Kutokana na uzoefu wangu mdogo niliokuwa nao wa kuishi sehemu tofauti na watu tofauti wenye tamaduni tofauti, nikaona kuwa labda jamii nyingi za kiafrika zaidi za nyumbani Tanzania hatupo wazi kueleza hali halisi kwa watoto wetu.

Tanzania mtoto anapokuwa amefika umri wa teenager, zaidi watoto wa kike anakatazwa asiwe karibu na wavulana lakini haambiwi sababu haswa akiwa karibu nao tatizo gani linaweza kutokea. Sasa mtoto anaanza kujiuliza tatizo haswa ni nini na ndipo hapo anapoanza kuutafuta ukweli yeye mwenyewe. Akiwa katika makundi na marafiki zake wanamchambulia ni nini kinaendelea kama akiwa na mvulana na wanaweza kumshawishi na yeye ajaribu kuingia katika mahusiano ya kimapenzi. Na kwa sababu mzazi hakumfafanulia haswa sababu za kumkataza kwake mtoto anakuwa anasikiliza ushauri wa marafiki zake na kwa kiasi kikubwa atawaamini zaidi kuliko atakavyomuamini mzazi wake. Kwa sababu hao ndio wanamfafanulia kuanzia A to Z. Na ndipo hapo mtoto anaanza mahusiano na kuingia mzima mzima si nusu nusu.

Kama tukiangaia nchi za Ulaya na Amerika, watoto wanaanza kuingia katika mahusiano wakiwa na miaka 16. Unaweza kuona kuwa ni mapema kumruhusu mwanao awe na rafiki wa kiume au wa kike katika umri huo. Ila ukweli ni kwamba wenzetu wanajua wanachokifanya na wao si wajinga kuwaruhusu watoto wao kuingia katika mahusiano. Wanachofanya ni kuwaelezea haswa mahusiano ni kitu gani, wanapokuwa katika mahusiano kuna mambo gani yanaweza kutokea na kama yakitokea athari zake ni nini. Na cha muhimu zaidi mzazi anatakiwa amwambie mtoto wake mipaka ambayo uhusiano wa kimpenzi ya mtoto wake uishie wapi. Kwani unaweza ukamkataza ukawa ni mkali kwa mwanao huku humwambii ukweli then siku akipata chance ‘ONE MISTAKE ONE GOAL.’ Hatuna uwezo wa kumfuatilia mtoto kila anachokifanya ila kama tukimpa moyo kuwa tunategemea mambo makubwa kutoka kwake na kwamba she/he can make it happen kwa maana hiyo asiharakishe mambo fulani fulani. Na pia mzazi anatakiwa kumuonesha mapenzi kama mtoto nadhani watoto wetu hawatavuka mipaka tutakayowawekea. Kutokana na nchi mbili tatu nilizowahi kutembelea swala hili nimeona kwamba linawezekana si kwamba sisi waafrika hatuna akili kiasi kwamba watoto wetu tutakachowaambia hawataelewa ila hatufanyi kama wenzetu wa ughaibuni wanavyofanya.

Kwa hiyo tunaweza kuwaruhusu watoto wetu kuwa katika relationships ila lazima kuwe na mipaka na mipaka hiyo mtoto mwenyewe lazima ahakikishe haivukwi. Nakubali kwamba watoto wapo tofauti na tabia tofauti ila bado naamini kuwa bora mtoto ajue mapema kinachoendelea.Comments / Maoni
 Posted By: rashidy              Fri 30 January 09
 Mi naona utamaduni wetu hauturuhusu
 Sasa mzee unataka wazazi tuwafundishe watoto zetu ngono? Hii nadhani ni kinyume cha utamaduni wetu
       

Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
JE NI SAWA BABA KUMUOMBA MSAMAHA MWANAE
JIBU KUHUSU CHUO CHA UZOEFU
Je kuzaliwa kwa mtoto kunapunguza mapenzi?
CHUO CHA UZOEFU.
JE NI SAWA KUMRUHUSU MTOTO WAKO KUWA NA BOYFR
Make Your Man Feel Appreciated
Msukosuko wa vyombo vya fedha duniani na madhara yake kwa Tanzania
Dating Your Coworker Or Boss, Is This A Good idea?
Should Tanzania worry about the credit crunch
Five Ways To Successfully Negotiate A Salary

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news