Blogs
 
ARTICLES
Iddy Mwanyoka     Email : mwanyoka@nifahamishe.com     
Mfumo Wetu Wa Elimu Ndio Chanzo Cha Umasikini
             
Tukiwa tunasherekea miaka 47 ya Uhuru nimeona ni muhimu kusimama kidogo na kutazama mfumo wetu wa elimu unamsaidiaje Mtanzania wa karne hii ya sayansi na tekinologia. Nadhani tutakubalia kwamba elimu ndio moyo wa maendeleo ya nchi yoyote.

Katika muongo huu wa utandawazi swali kubwa nililojiuliza ni jee mfumo wetu wa elimu unaweza kumjenga kijana wa Kitanzania kupambana na kijana wa Kihindi au Kimexican? Tanzania ya leo bado inatumia mfumo wa miaka 7 ya elimu ya msingi, miaka 4 ya sekondari na 2 ya sekondari ya juu. Hii ni jumla ya miaka 13 kabla mwanafunzi hajakanyaga chuo chochote ili kupata mafunzo ambao anaweza kuyatumia. Swali linakuja jee miaka hii 13 kijana huyu anakuwa amepatiwa ujuzi wa aina gani? Jee kijana huyu ameandaliwa vilivyo kushindana na vijana wenziwe kutoka nchi nyingine kama hatafanikiwa kuingia chuo kikuu chochote?

Katika karne hii ya 21 ambapo computer inaunganishwa katika nchi tano kabla ya kuuzwa ni muhimu tukatazama mfumo wetu wa elimu kama tunataka kushindana. La sivyo kila siku tutasema hatuwezi kuungana na Kenya sababu wanajua Kingereza au wana wasomi kushinda sisi.

Mfumo wetu wa Elimu ni wa karne ya 19, mfumo wa kuzalisha watoto wenye uwezo wa juu wa kukremu badala ya kuzalisha vijana wenye uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo. Nidhahiri ya kwamba kwa miaka yote 13 kijana wa Kitanzania anakuwa anaandaliwa ili afanye mtihani wa kidato cha sita.

Nadhani huu ni muda muafaka kwa serikali yetu kutazama kwa kina mfumo huu wa nadharia. Tunaitaji elimu ambayo itamuandaa kijana wa Kitanzania awe mshindani katika muongo huu wa utandawazi. Nadhani huo sio muda wa kushindanisha ni shule gani ina division one nyingi, bali ni muda wa kushindanisha shule zenye kuzalisha wanafunzi wenye uwezo wa juu wa kufanya utafiti.

Elimu ya Imla haina nafasi katika dunia ya leo. Kama viongozi wetu wanataka Tanzania siku mmoja iwe moja ya nchi bora, basi hawana budi kuliangalia upya swala la mfumo wetu wa elimu. Vingenevyo tutazidi kudhamini shahada kutoka ng’ambo na vijana wetu watazidi kuwa mkiani.

Madhara ya hii elimu tumeyaona baada ya ubinafsishaji kupiga hodi Tanzania. Tumeona jinsi wawekezaji wanavyo wathamini wafanyakazi walio soma ng’ambo kuliko wale walio soma Tanzania. Wengi wetu tumekuwa tukisema wanachofanya wawekezaji sio haki, japokuwa tumeshindwa kukubali ukweli kwamba wanafunzi wetu wana uwezo mkubwa wa kukremu kuliko kufanya uchambuzi.


Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
Mkutano wa G-20 Unamuhusu vipi Kibwana?
Foreign Aid: glaucoma to Tanzania
WHY CAPITALISM FAILED IN AFRICA?
World Bank is Not a Solution
HOW IMF & WORLD BANK FAILED IN AFRICA
Mfumo Wetu Wa Elimu Ndio Chanzo Cha Umasikini
Jee EAC ni Dawa ya Matatizo ya Nchi Zetu
Macho Yote Kwa Obama
Mpasuko wa mfumo wa fedha duniani je ni mwisho wa dolla?
10 Jobs That Pay $30 An Hour

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news