Blogs
 
ARTICLES
Iddy Mwanyoka     Email : mwanyoka@nifahamishe.com     
Jee EAC ni Dawa ya Matatizo ya Nchi Zetu
             
Kwa muda mrefu sasa mabishano kati ya Watanzania, Waganda na Wakenya kuhusu muungano wa nchi za Africa Mashari yamekuwa kugumzo katika vijiwe mbalimbali na katika mitandao na blogu mbalimbali.

Wakenya na Waganda wamekuwa wakiwalaamu Watanzania kwamba ndio chanzo cha kufanya maongezi ya muungano kuzorota. Baadhi ya Wakenya wamediriki hata kuwatusi Watanzania kwa kusema kwamba akili zetu ni za kijamaa hivyo tunawaogopa wao sababu wana akili za kikabaila.

Kuunganisha nchi sio swala la maamuzi ya masaa matu au manne, na sio swala la raisi Kikwete, Museveni, Kagame au Kabaki bali ni swala la wananchi wa nchi hizi za mashariki ya Africa. Ikumbukwe kwamba 1967 Mwalim Nyerere, Jummo Kenyetta na Obotte walijaribu ili swala la kuunganisha nchi za mashariki. Matokeo yake huo muungano ulipasuka mnamo mwaka 1977. Sidhani kama huu ni muda muafaka wa kujadili kwa nini muungano ulipasuka miaka hiyo ya sabini. Lakini ni muda muafaka wa kujadili jee kweli tunaitaji muungano kwa muda huu?

Kuanzia mwanzoni mwa miaka ya tisini baada ya kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin dunia imeingia katika mfumo mpya, mfumo wa utandawazi (globolization). Nchi nyingi duniani zimepunguza vikwazo vya kibiashara baina ya nchi na nchi, na nyingine zimetengeneza muungano wa kibiashara baina ya nchi na nchi, mfano NAFTA (North American Free Trade Agreement). Na nyingine zimeunda muungano wa nchi kama vile jumuia ya nchi za Ulaya.

Ijapokuwa dunia nzima inashabikia swala zima la kuungana, hiyo isiwe sababu ya sisi (Wafrica) kushabikia pia. Swala la kuunganisha nchi linaitaji uchambuzi yakinifu wa faida na hasara za muungano. Watanzania tunafahamu raha na karaha za muungano kushinda nchi yoyote ile Africa. Kwani Tanzania ndio nchi pekee ambayo ni muunganiko wa nchi mbili (Tanganyika na Zanzibar)

Kuna maswala machache ambayo nadhani kabla ya kuwaza kuunganisha nchi hizi za mashariki inabidi tujiulize.
Swali la kwanza, Jee Uganda watakubali kufuata mfumo wa demokrasia na kuachana na mfumo wa udikteta? Raisi Museveni amekuwa madarakani tangu miaka ya themanini na bado ataendelea kuwa madarakani mpaka siku atakapojisikia kuachia ngazi. Hili swala muhimu sana kwetu Watanzania kujiuliza.

Swala la Pili, Jee sheria ya kumiliki ardhi itatumika ya Tanzania au ya Kenya au ya Uganda? Nchi za Kenya na Uganda zimekuwa na mikwaruzo ya ardhi kwa miaka zaidi ya 50 sasa. Wakulima wakubwa wamekuwa ndio wamiliki wa ardhi kwa asilimia kubwa, na huku wakulima wadogo wakijikuta wao ni wakodishaji tuu.

Swala la tatu, Jee ni mbinu gani Kenya inajaribu kutumia kupunguza chuki za kikabila baina ya Waluo na Wakikuyu na wengineo? Juzi juzi tumeone jinsi wakenya walivyo katana vichwa badaa ya uchaguzi. Na kiini kabisa chake ni kwanini hawa Wakikuyu wameshindwa uraisi na wanakataa Wajaluo wasichukue uongozi.
Swala la nne, Jee Kagame ataacha kuwasaidia waasi wa msituni wanaochafua amani ya Congo? Juzi juzi tumeona jinsi jeshi hili la waasi lilivyo uwa watu kama kuku nchi Congo.

Maswali haya manne ni baina ya maswali mengi sana ambayo inabidi tuyajibu kabla hatujashabikia swala zima la muungano. Ileweke ya kwamba mimi sipingi muungano bali napinga muungano utakao kufa baada ya miaka michache kuanzishwa.

Ukiachana na matatizo ya Wakenya, Wanyaruwanda na Waganda, sisi wenyewe Watanzania tuna mambo mengi sana ya kufanya kabla hatujawaza kuungana na mtu yoyote yule. Tanzania bado hatuna huduma mahususi za Afya na Elimu. Leo hii malaria bado ni tishio la maisha ya watoto wengi nchini kwetu, vile vile Elimu yetu bado hawezi kuwaanda wananchi wetu wawe washindani katika muongo huu wa mtandawazi.

Ukiachana na Elimu na Afya, mfumo wetu wa uchumi bado ni duni sana. Watanzania wengi bado wanaishi katika hali duni sana. Nchi yetu imekuwa mkiani katika swala zima la kusafirisha bidhaa nje ya nchi, Tanzania imekuwa bingwa wa kupokea bidhaa za nje.

Hivyo basi, itakuwa ni swala la muhimu sana kama muungano ukasubiri mpaka tutakapotatua matatizo yetu ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Ikumbukwe ya kwamba nchi hizi zote tatu zinategemea misaada ili kuendesha serikali zake. Sasa naona ni swala la ajabu leo kuwaza kuunganisha serikali ambazo zinashindwa hata kujiendesha zenyewe.

Nadhani kwa muuda huu tuangalie uwezekano wa kuanzisha muungano wa kibiashara baina nchi hizi tatu. Muungano utakao ondoa au kupunguza sheria za usafirishaji na uchuuzi wa bidhaa baina ya nchi hizi za mashariki mwa Africa. Swala hilo litaongeza ajira na vile vile kuongeza ushindani wa kibiashara.

Nahitimisha kwa kusema kwamba EAC sio dawa ya matatizo tuliyonayo Africa Mashariki, bali ni chochezi ya matatizo mengine. Mwalimu alisema “ shona suti kutokana na ukubwa wa kitambaa, na kabla ujawaza kununua baiskeli kwanza jenga choo”. Hivyo basi kwanza kabla hatujawaza kuwa na nchi mmoja ya Africa mashariki basi tutatue matatizo yetu kwanza.

Comments / Maoni
No comment added
Post your Comments / Toa maoni yako
Heading
Comments


                  
My Other articles
Mkutano wa G-20 Unamuhusu vipi Kibwana?
Foreign Aid: glaucoma to Tanzania
WHY CAPITALISM FAILED IN AFRICA?
World Bank is Not a Solution
HOW IMF & WORLD BANK FAILED IN AFRICA
Mfumo Wetu Wa Elimu Ndio Chanzo Cha Umasikini
Jee EAC ni Dawa ya Matatizo ya Nchi Zetu
Macho Yote Kwa Obama
Mpasuko wa mfumo wa fedha duniani je ni mwisho wa dolla?
10 Jobs That Pay $30 An Hour

 
Photo Gallery

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream

 Huku si Kujitakia kifo?
Most viewed news