Kompyuta na Monitors, Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo

NewsImages/7119142.jpg
Mwandishi wa Marekani aliyeuawa na kundi la ISIS
Thursday, August 21, 2014 6:11 PM
Majeshi ya Marekani yameendelea kuwashambulia wapiganaji wa Islamic State huko Iraq licha ya vitisho kutoka kwa kundi hilo kuwa watawaua mateka wengine wamarekani iwapo Obama angeendelea kuishambulia himaya hiyo kaskazini mwa Iraq.
Majeshi ya Marekani kwa ushirikiano na ndege zisizikuwa na marubani zilifanya mashambulizi 14 usiku wa kuamkia leo.
Mashambulizi kumi na manne ya angani yamefanyika katika eneo karibu na bwawa la Mosul na yalilenga kuwasaidia wanajeshi wa Iraq na wa kikurdi.

Bwawa la Mosul lililotekwa kutoka kwa wapiganaji wa IS
Maafisa wajeshi la Marekani wamesema kuwa walifaulu kulipua magari ya kijeshi na vitu vingine vilivyokuwa vikitumiwa na wapiganaji wa IS .
Tarifa kutoka kwa wakurdi zinasema kuwa ndege ambazo hazina rubani zilikuwa angani kuwalinda wanajeshi Wakurdi wakati wapiganaji wa Pesh Merga wakisukumwa katika milima, kusini mashariki mwa bwawa kubwa la Mosul, ambalo lilitwaliwa tena kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu wiki hii.
Pentagon imethibitisha kuwa mashambulizi kumi na manne ya angani yalifanywa katika sehemu hiyo kuliko bwawa na kuyalenga magari kadhaa ya kijeshi na vitu vingine.
Televisheni ya taifa ya Iraq imesema kuwa ndege hizo za vita za Marekani zilikuwa pia zimetekeleza mashambulizi katika kambi za magaidi mkoani al-Anbar hadi magharibi mwa Baghdad, na zilikuwa zimetoa ulinzi wa angani kwa vikosi vya serikali vilivyokuwa vikielekea kuwakabili waasi wa kisuni.

Majeshi ya Iraq yakielekea kukabiliana na wanamgambo wa Islamic State
Awali makao kuu ya Jeshi la Marekani limesema kuwa wanajeshi la kitengo maalum walijaribu kumuokoa mwanahabari James Foley na waamerika wengine walioshikwa mateka nchini Syria.
Habari hii imetolewa baada ya video ya aliyetekwa nyara novemba 2012 nchini Syria kuonyeshwa akiuawa kikatili na wanamgambo wa Kiislamu kutokea jumapili .
Wanamgambo hao walisema mauaji yake ilikuwa kulipiza kisasi dhidi ya Marekani kwa sababu ya kuwashambulia wapiganaji wao hewani Iraq.

Rais wa Marekani Barack Obama alikashifu mauaji hayo na kuwalinganisha wanamgambo hao na ugonjwa wa saratani na kuwa itikadi zao hazikuwa na mwelekeo aliendelea kuwa kusema tendo hilo lilishtua ulimwengu mzima

Umoja wa kitaifa ,uingereza na wengine pia wameeleza huzuni yao kutokana na video hiyo.
Mamake Bwana Foley Diane alisema kuwa mwanawe aliaga dunia kwa niaba ya watu wa Syria.
Kamati inayolinda wanahabari ilisema ina wasi wasi kwa wanahabari wote waliozuiliwa na wanamgambo hawa na kusema wanahabari wajiepushe na Syria.

 
Source: BBC    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: ISLAMU    Thursday, August 28, 2014 17:39:10   
 
Habari za kuaminika zinasema kuwa, watuhumiwa wa kiislamu (zingatia hapa, ni watuhumiwa bado uhalifu wao hauja thibitika)wanapata mateso ya kutisha na ya kinyama ambayo dunia ikisikia na uadilifu kufanywa, wahusika wataishia pabaya.

Je nifahamishe habari hizi sio muhimu?

 
 
Mtoa Maoni: MARK WA ITALY.    Friday, August 29, 2014 18:17:00   
 
MARK.MUSHI WA ITALY NIMERUDI RASIMI NDANI YA MTANDAO WA NIFAHAMISHE,BAADA YA KUPOTEA KWA MUDA MREFU.HAWA WA IRAQ,IRAN,PALESTINA.ISRAELI AWA2MII AKILI,NA WANA2MIA DINI YAO KAMA KIGEZO CHA...ILA SIKU YA SIKU WATAZIDI KUPATA HASARA WAO TU.MAANA MAREKANI ATAWA2NGUA KWA MABOMU YA NDEGE HADI WAKOME ADABU YAO,VP TORRES ANAKUJA AC MILAN?DESTRO AJE CHELSEA BHANA.KAMA IMEKUTOUCH NICHEKI KWA NAMBA HII,+393336989592.
 
 
Mtoa Maoni: MARK WA ITALY.    Friday, August 29, 2014 18:17:01   
 
MARK.MUSHI WA ITALY NIMERUDI RASIMI NDANI YA MTANDAO WA NIFAHAMISHE,BAADA YA KUPOTEA KWA MUDA MREFU.HAWA WA IRAQ,IRAN,PALESTINA.ISRAELI AWA2MII AKILI,NA WANA2MIA DINI YAO KAMA KIGEZO CHA...ILA SIKU YA SIKU WATAZIDI KUPATA HASARA WAO TU.MAANA MAREKANI ATAWA2NGUA KWA MABOMU YA NDEGE HADI WAKOME ADABU YAO,VP TORRES ANAKUJA AC MILAN?DESTRO AJE CHELSEA BHANA.KAMA IMEKUTOUCH NICHEKI KWA NAMBA HII,+393336989592.
 
 
Mtoa Maoni: Witnes Gamasa    Tuesday, October 14, 2014 14:33:19   
 
Mwenyezi MUNGU Ailaze Roho Ya Maremu James Foley Pema Peponi Amina. Raha Ya Milele Umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie Apumzike Kwa Amani.
 
 
Mtoa Maoni: DANNY MWALASA    Thursday, October 16, 2014 21:21:38   
 
ISIS KAMWE HAWATAKUJA KUWEZA ETI KUITAWALA DUNIA KWA HILA ZAO.
WATAISHIA HUKOHUKO ARABUN

 
 
       Jumla kuna maoni (15), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za dunia
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Mbakaji Azimia Baada ya Kuambiwa Mwanamke Aliyembaka ni Muathirika
> Wanawake Waislamu Waowana Ndoa Ya Jinsia Moja.
> Wanawake Waislamu Waowana Ndoa Ya Jinsia Moja.
> Wazuiwa Chuo Kwa Nguo Waliyovaa
> 'Waislamu ni Waovu Waueni Wote'
> Jela Au Faini Kwa Kucheka Kwa Sauti Kubwa.
> Kijasho Chembamba Chamtoka Waziri Mkuu
> Wakulima Wapewa Mikopo Kupunguza Ujane
> Binti Wa Miaka 15 Atoroka kwa Mume kisa Mzee
> Gangnam Style Ina Asili ya Afrika
> Apiga picha za uchi kupinga katiba ya kiislam
> Mwanamke mnene washindwa kumpandisha kwenye Gari la wagonjwa
> Wafufua maiti na kuitembeza mitaani
> Mbunge wa bunge la ulaya ashitakiwa kwa kuwatukana waislamu
> Ajiua kwa Matamanio ya ngono ya mara kwa mara
> Wanawake waitisha mgomo wa ngono Italy
> Mwanafunzi azuiwa kwenda chooni afariki darasani
> Cobra ailazimisha ndege kutua Misri
> Obama Achaguliwa Tena Kuwa Rais wa Marekani
> Wamarekani Kumchagua Rais Wao Leo
> Mlinzi wa Obama Ajiua
> Aliyetangazwa Amekufa, Ahudhuria Mazishi Yake Mwenyewe
> VIDEO - Ukisikia Pombe si Maji....

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD