Kompyuta na Monitors, Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika

NewsImages/7116250.jpg
wasanii wakijumuika katika picha
Thursday, April 17, 2014 6:59 PM
Siri ya Mtungi iliwania vipengele saba: Tuzo ya Mwigizaji Bora kwenye Drama, ikiwakilishwa na Juma Rajabu, Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Filamu za Vichekesho, Filamu Bora iliyotumia lugha kiufasaha (Kiswahili) na Mwandaaji Bora Mwenye Kipaji (Kyle Quint)
USIKU wa kuamkia March 9 Jumapili, haukuwa mzuri kwa tamthilia ya Siri ya Mtungi kwani ilichemka kwenye halfa ya tuzo za Africa Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA) 2014 zilizofanyika Nigeria.

Siri ya Mtungi tamthilia inayotengenezwa na Media for Development International (MFDI) Tanzania, ni tamthilia ilikuwa tishio kubwa katika tuzo hizo, kwani iliteuliwa kuwania vipengele saba tofauti kati ya vipengele 28 vilivyowaniwa.

Siri ya Mtungi iliwania vipengele saba: Tuzo ya Mwigizaji Bora kwenye Drama, ikiwakilishwa na Juma Rajabu, Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Filamu za Vichekesho, Filamu Bora iliyotumia lugha kiufasaha (Kiswahili) na Mwandaaji Bora Mwenye Kipaji (Kyle Quint).

Pia ilijitokeza kuwania Tuzo ya Mhariri Bora wa Sauti ikiwakilishwa na Jordan Riber, Tuzo ya Mbunifu Bora wa Mavazi (Doreen Estanzia Noni) na Tuzo ya Mpambaji Bora ikiwakilishwa na Rehema Samo.

Kwa bahati mbaya haikufurukuta hata kwenye kipengele kimoja, kutokana na kile kilichoelezwa na waandaaji kwamba Siri ya Mtungi ni kati ya washiriki waliopata kura chache katika kuwania tuzo hizo ambazo mshindi wake anategemea zaidi kura za watazamaji.

Tamthilia ya Siri ya Mtungi imeambulia patupu katika tuzo hizo zilizotolewa usiku wa kumkia jana Jumapili, katika Hoteli ya Eko and Suites Victoria Island, Lagos nchini Nigeria.

Akizungumza kwa njia ya barua pepe na gazeti hili jana, John Riber ambaye ni Prodyuza na Mkurugenzi Mkuu wa MFDI Tanzania, alisema: “Siri Ya Mtungi inawashukuru kwa kutuunga mkono, kwa nguvu kubwa na sasa tunajitayarisha kwa ajili ya tuzo nyingine mwakani. Tunatoa pongezi kwa wengine wote waliokuwa wamechaguliwa pamoja na washindi wote.”

Katika tuzo hizo ambazo hutolewa kila mwaka, Kenya imefanikiwa kutamba huku Nigeria ikiongoza kwa kutwaa tuzo nyingi zaidi. Waigizaji kutoka Nigeria waliotamba kwenye tuzo hizo ni pamoja na Osita Iheme, Rita Dominic na Desmond Eliot.

Vikwazo vilivyoiponza Siri ya Mtungi

Hakuna cha kuficha, Watanzania hatuna utamaduni wa kupiga kura. Tunaweza kuinuka na kusifia wenzetu pindi wanapofanikiwa, lakini kwa upande wetu hatuna utamaduni wa kuwafanya watu wetu wang’are.

Hata hivyo timu ya Siri ya Mtungi yenyewe haikuwa na nguvu kubwa kwenye kushawishi wadau, katika upigaji kura. Yote kwa yote timu hii ipo vizuri na tunaamini mapungufu haya yakirekebishwa, hakutakuwa na matatizo kama haya miaka ijayo.

Ni kweli kwamba penye ushindani daima kunakushinda na kushindwa, hivyo haina budi kukaza buti na kuanza kujipanga upya ili pindi tunapoanza tuwe washindi.
Hapana shaka wala wasiwasi, tuzo si kigezo pekee cha kupima ubora wa kazi. Hata wao wa mataifa mengine wamejifunza mengi, tayari elimu imewafikia ikiwa ndiyo lengo kuu la Siri ya Mtungi.

Watanzania wapo nyuma katika ushirikiano maana unakuta kazi nzuri na watu wanaikubali ila ikifika kwenye kupiga kura au kutoa maoni tunakuwa wazito.

Kiukweli tunapitwa na mambo mengi wakati tupo kwenye nafasi nzuri ya kushinda au kujitangaza. Siri ya Mtungi ni tamthilia nzuri kwa watazamaji wa kawaida na hata wale wageni wasioijua vyema lugha ya Kiswahili. Umoja ni nguvu daima.

Baadhi ya washindi wa AMVCAs kwa mwaka huu na kazi zao kwenye mabano ni pamoja na Shirley Frimpong (Manso), Yvonne Okoro & Ken Attoh (Contract), Frank Rajah Arase (The Groom’s Bride), Elvis Chucks ( A Wish), Bikiya Graham (Douglas) Flower Girl, Desmond Elliot ( Finding Mercy), Funke Akindele ( Return of Sheri Koko), Osita Iheme (The Hero), Walter Waltbanger Taylaur (The Wages), New Era Award Movie Rita Dominic (The Meeting) na wengineo.

Kuhusu Siri ya Mtungi

Ni tamthilia ya televisheni inayofurahisha, inayoonyesha maisha ya Cheche, mpigapicha mwenye bashasha na mmiliki wa studio ya kupiga picha ya Mtungi. Ana mke mrembo, Cheusi, aliyemzalia watoto wawili wenye afya huku akiwa na ujauzito wa mtoto wa tatu,’ hii ni sehemu ya kwanza ya tamthilia hiyo.

Ushiriki wa tamthilia hii katika tuzo hizi za kimataifa pia ni ishara ya kutambulika na kukua kwa sanaa na wasanii wa maigizo kutoka Tanzania. Sehemu ya pili ya tamthilia hii iliyojizolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania ipo katika matengenezo na inatarajiwa kuanza kuonyeshwa tena ifikapo Mei mwaka huu.

John Riber Prodyuza na Mkurugenzi Mkuu wa MFDI Tanzania, anasema uamuzi wa kutayarisha tamthilia ya Siri ya Mtungi ya kiwango cha juu inayoongea moja kwa moja na watu wa Tanzania na Afrika Mashariki ni mwanzo wa kuleta mapinduzi ya mtandao wa mawasiliano.

Ndugu zangu tuchangie wasanii wetu.

 
Master,Mwanaspoti    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: SEEKER-OF-TRUTH    Thursday, April 17, 2014 23:56:34   
 
Nilijua tu iko siku Nifahamishe pia itageuza muelekeo, itafuata mkondo wa maji, halafu itakosa wapenzi na kudoda kama blog zingine.

Story kama hizi zinapatikana maelfu ya mitandao, na sikutegemea nifahamishe wataleta habari duni kama hizi.

KWAHERI NIFAHAMISHE.

 
 
Mtoa Maoni: marthinya    Friday, April 18, 2014 08:52:25   
 
nawapa pole wanasiri ya mtungi,wasikate tamaa wajipange upya.
 
 
Mtoa Maoni: jovin wamineso    Wednesday, April 23, 2014 13:31:15   
 
watanzania tuna kasumba ya kuwasifia wasanii wakiwa kwa jukwaa ktk michango kama kura tunakaa pembeni so vzr tizama nigeria
 
 
Mtoa Maoni: Umassm shija    Friday, May 02, 2014 10:39:58   
 
Nijambo la heri wanamtungi paka ampo mlipo.lakin watanzania hawana mapenz na sanaa...! tuamke.. mimi ni mwandishi wa hadithi,mchoraji wa katuni naitaji mfadhili namba yangu ni 0766633527. ilemela, mwanza.
 
 
Mtoa Maoni: Uncle D    Tuesday, May 06, 2014 07:06:56   
 
Nifahamishe siku hizi mmechuja sana kwa kutoa habari.Jitahidini jamani habari za idadi ya wabunge wa katiba 201 mmeiweka huu mwezi wa tatu sasa ndio ikaja hii ya Mtungi.Wakati mwingine naona uvivu kuifungua tena Nifahamishe maana najua sitakuta kituu
 
 
       Jumla kuna maoni (10), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za Tanzania
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD
> Mwenyekiti wa CCM Dar aburuzwa mah akamani kwa kusambaza ARV bandia
> BUNGE LA KATIBA LAIVA, JK ataja majina
> Askari afariki dunia kwa kupigwa na jiwe kichwani na mahabusu- ARUSHA
> Serikali yatangaza neema vijijini kuunganisha umeme
> Mwanamke auawa,kichwa chake chakutwa uwanja wa mpira
> Tuna sifa za kukopa -Waziri
> Kila Mtanzania anadaiwa Sh.600,000/ deni la Taifa
> Askari watano wafariki katika ajali -DODOMA
> Hawa hawakuguswa katika mabadiliko mapya
> SURA MPYA
> Rais Kikwete awabwaga watano waliokuwa kwenye baraza la zamani
> Rais Kikwete awaapisha Mawaziri wapya aliowateua
> 13 wapoteza maisha katika ajali -Singida
> Akamatwa kwa kosa la kujifanya Koplo wa JWTZ
> 9 wapoteza maisha katika ajali ya basi -LINDI
> Mkapa achapisha vitabu vya hotuba zake
> 15 wapoteza maisha mgogoro wa ardhi Kiteto
> Wananchi wachoma moto basi lililouwa watoto watatu

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD