Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Mwenyekiti wa CCM Dar aburuzwa mah akamani kwa kusambaza ARV bandia

NewsImages/7109502.jpg
Madabida kulia na wenzake wakifikishwa mahakamani
Tuesday, February 11, 2014 6:48 AM
MWENYEKITI wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Ltd cha Dar es Salaam (TPI), Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na ma

Wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TPI, Seif Shamte, Meneja Masoko, Simon Msofe, Mhasibu Msaidizi, Fatma Shango pamoja na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), Sadick Materu na Evans Mwemezi.

Jana washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo na mashitaka yao yalisomwa na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Nyigulile Mwaseba.

Shitaka la kwanza, Aprili 5, mwaka 2011, washitakwia hao kwa kutumia nyadhifa zao walisambaza makopo 7,776 ya dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARV) aina ya Antirectroviral.

Washtakiwa hao, walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 76 (1)(2) cha Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2003, wakijaribu kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa halali na kwamba zimetengenezwa Machi, 2011 na muda wake wa kutumika unakwisha 2013 wakati wakijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa, Aprili 11, 2011, Madabida, Shamte, Msofe na Shango walisambaza na kuuza makopo 4,476 ya dawa bandia aina ya Antiretroviral walizokuwa wakijaribu kuonyesha kuwa zilikuwa na viambatanisho vya Starudine 30mg, Nevirapine 200mg, Lamivudine 150mg pamoja na fungu namba OC 01.85 kumbe si kweli

Katika shtaka la tatu wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kinyume na Kifungu cha 302 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 walijipatia Dola za Marekani 98,506 sawa na Sh148,350,156.48 fedha walizopata Aprili 12 2011

Katika shtaka la nne, Materu na Mwemezi wakiwa ni Meneja wa Udhibiti Viwango na Ofisa Udhibiti Viwango wa MSD, kati ya Aprili 2 na 13, 2011 huku wakijua nia ya kutendeka kwa makosa hayo ya usambazwaji wa dawa bandia, walishindwa kuzuia kinyume na Kifungu cha Sheria namba 383 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Katika shtaka la tano, wakili huyo wa Serikali alidai kuwa kati ya Aprili 5 na 30, 2011, washtakiwa Madabida, Shamte, Msofe, Shango pamoja na Materu na Mwemezi, kinyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi, walishindwa kutekeleza majukumu yao wakiwa watendaji.

Alidai kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa hao kwa pamoja walishindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kusambaza makopo 12,252 ya dawa bandia wakijaribu kuonyesha kuwa zilitengenezwa Machi 2011 na kwamba zitakwisha muda wake wa kutumika Februari 2013.

 
Na MWandishi Wetu, DAr    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: neem    Wednesday, February 12, 2014 17:20:26   
 
Izo dawa bandia na dawa zilizo kwisha muda wake ni sumu 100% huo
ni kuua kwa makusudi.Kama ni nchi
ya CHINA unanyongwa ni kama hile ya maziwa ya watoto,wakubwa wa hiyo kampuni wengine walinyongwa.
Kwanini watu wanapenda sana fedha
kuliko kupenda wenzao?Hizi ndizo
siku zamwisho tulizo kuwa tunaambiwa?kuwa siku zamwisho watu
watapendasana fedha,ndugu kwa ndugu watauana,nchikwa nchi,vita
etc.dawa zilizokwisha muda zinafutwa tarehe tayari ni sumu.Hogopa MUNGU Tamaa ya hela
inakuponza sasaSHAME.

 
 
Mtoa Maoni: neem    Wednesday, February 12, 2014 17:36:30   
 
Mchezo kama huu wa kufuta tarehe
na kuwekwa tarehe mpya nausikia
sana nchi za west Afrika.Wako very
sharp kwa mchezo huo na watu wengi
wamepoteza maisha kwa kununua dawa
za bandia na za kuisha muda wake
huku wanaonyesha sana kwenye TV
kuhusu AFYA ya watu wa Afrika,kuwa
hatarini na dawa za bandia etc
Wanao adhirika sana ni watoto na
watu wadhaifu kiafya.Kumbe ni sisi
wafrika kwa Afrika tunauana kwa
tamaha za kupenda sana hela.Hela
hatutakwenda nazo tutaziacha hapa
duniani navyote tuvipendao

 
 
Mtoa Maoni: Uncle D    Saturday, February 15, 2014 18:41:02   
 
Nashauri bunge la katiba mpya lipitishe sheria kuwa mtu akikamatwa na kosa kama hili ameua kwa kukusudia hivo anyongwe mpaka afe.Tujiulize ni watu wangapi wamekufa kutokana na utapeli huu wakidhani wanakunywa dawa za kupunguza makali ya dawa.Kumbe ndio maana kuna ndugu zetu wameadhirika unakuta anakufa ghafla wakati asubuhi ulikuwa unongea naye.Tuige mfano wa china Tanzania siasa zimetuharibu sana hadi viongozi wetu tu mizaha na mamboa ya msingi

 
 
Mtoa Maoni: Dr Noel Mmolle    Monday, April 14, 2014 16:23:20   
 
Hawa ni wauwaji wa makusudi,hawastahili hata huruma ya Mtanzania ye yote,siasa kwa kweli inatumika vibaya na inatuletea maafa haya. Inabidi Watanzania tubadilike, kwenye kazi tufanye kazi,kwenye sayansi tusiiweke siasa,naomba mahakama itoe adhabu kali kwa wauwaji hawa wa kukusudia,ili iwe mfano kwa watu wenye tabia kama hiyo.
 
 
Mtoa Maoni: Tumaini    Friday, May 16, 2014 17:28:22   
 
Minaona wanyongwe tu iliiwefundisho kwa wengine kama hawa wanaoathir afya za wenzao kwasababu yatamaa ya pesa!
 
 
       Jumla kuna maoni (8), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za Tanzania
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD
> Mwenyekiti wa CCM Dar aburuzwa mah akamani kwa kusambaza ARV bandia
> BUNGE LA KATIBA LAIVA, JK ataja majina
> Askari afariki dunia kwa kupigwa na jiwe kichwani na mahabusu- ARUSHA
> Serikali yatangaza neema vijijini kuunganisha umeme
> Mwanamke auawa,kichwa chake chakutwa uwanja wa mpira
> Tuna sifa za kukopa -Waziri
> Kila Mtanzania anadaiwa Sh.600,000/ deni la Taifa
> Askari watano wafariki katika ajali -DODOMA
> Hawa hawakuguswa katika mabadiliko mapya
> SURA MPYA
> Rais Kikwete awabwaga watano waliokuwa kwenye baraza la zamani
> Rais Kikwete awaapisha Mawaziri wapya aliowateua
> 13 wapoteza maisha katika ajali -Singida
> Akamatwa kwa kosa la kujifanya Koplo wa JWTZ
> 9 wapoteza maisha katika ajali ya basi -LINDI
> Mkapa achapisha vitabu vya hotuba zake
> 15 wapoteza maisha mgogoro wa ardhi Kiteto
> Wananchi wachoma moto basi lililouwa watoto watatu

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD