Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
BUNGE LA KATIBA LAIVA, JK ataja majina

NewsImages/7108538.jpg
Saturday, February 08, 2014 7:51 AM
RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201.


Uteuzi huo umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana, watu wazima na wazee, Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35, Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64 ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.

Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa wajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.

Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa.
Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.

Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.

Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na
Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.

Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-

(i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii) Taasisi za Kidini (20)
(iii)Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu
(iv) Taasisi za Elimu (20);
(v) Watu wenye Ulemavu (20);
(vi) Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix) Vyama vya Wakulima (20); na
(x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).

 
Na Mwandishi Maalum, Ikulu    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: richard    Tuesday, February 18, 2014 21:27:33   
 
Kiikweli raids kazingatia usawa wa jinsia na rika zote
 
 
Mtoa Maoni: jlmsenga    Wednesday, February 19, 2014 16:22:06   
 
Napendekeza serekali tatu serekali mbili sio Tanzania mpya tuamke
 
 
Mtoa Maoni: nasserelmasrawy    Wednesday, February 19, 2014 17:54:17   
 
asant mh kikwete
 
 
Mtoa Maoni: selestin peter    Thursday, April 24, 2014 01:28:57   
 
nawaomba wananchi wasikubali kushawishiwa kwa kukubaliana na mpango wa selikari tatu
 
 
Mtoa Maoni: 0688317264    Friday, April 25, 2014 11:35:59   
 
Selekali Tatu Ni Tanzania Kweli
 
 
       Jumla kuna maoni (9), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za Tanzania
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD
> Mwenyekiti wa CCM Dar aburuzwa mah akamani kwa kusambaza ARV bandia
> BUNGE LA KATIBA LAIVA, JK ataja majina
> Askari afariki dunia kwa kupigwa na jiwe kichwani na mahabusu- ARUSHA
> Serikali yatangaza neema vijijini kuunganisha umeme
> Mwanamke auawa,kichwa chake chakutwa uwanja wa mpira
> Tuna sifa za kukopa -Waziri
> Kila Mtanzania anadaiwa Sh.600,000/ deni la Taifa
> Askari watano wafariki katika ajali -DODOMA
> Hawa hawakuguswa katika mabadiliko mapya
> SURA MPYA
> Rais Kikwete awabwaga watano waliokuwa kwenye baraza la zamani
> Rais Kikwete awaapisha Mawaziri wapya aliowateua
> 13 wapoteza maisha katika ajali -Singida
> Akamatwa kwa kosa la kujifanya Koplo wa JWTZ
> 9 wapoteza maisha katika ajali ya basi -LINDI
> Mkapa achapisha vitabu vya hotuba zake
> 15 wapoteza maisha mgogoro wa ardhi Kiteto
> Wananchi wachoma moto basi lililouwa watoto watatu

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD