Kompyuta na Monitors, Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Serikali yatangaza neema vijijini kuunganisha umeme

NewsImages/7106610.jpg
Monday, February 03, 2014 6:08 AM

SERIKALI imeshusha gharama ya kuunganisha umeme vijijini ambapo kuanzia sasa wateja watalipia Shilingi 27,000 na wataweza kuungaishiwa umeme.
Vilevile imepunguza zaidi viwango vya kuunganishiwa umeme vitakavyolipwa na wananchi wa mikoa ya Kusini wanaoishi maeneo linapopita bomba la gesi.

Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alipokutana na uongozi wa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) na makandarasi waliopewa kazi ya kusambaza umeme kwenye vijiji vya mikoa mbalimbali.


Kuhusu mikoa ya bomba la gesi alisema serikali inatafakari namna ya kuendelea kuwapunguzia gharama wananchi wa mikoa ya Kusini, na kwamba wakati wowote itatangaza viwango vipya vya umeme itakayokuwa chini zaidi.

Profesa Muhongo, alisema wananchi watakaoanza kunufaika na punguzo ni wakazi wa mikoa ambayo kuna miradi ya umeme inayosimamiwa na Rea.

Alisema utekelezaji wa miradi hiyo ya Rea iliyoanza mwaka 2007 hadi 2015 itawawezesha wananchi kulipa Sh. 27 badala ya Sh 177,000 za hapo awali.

"Nawatangazia wananchi wote watakaohusika na miradi hii ya umeme watalipa kiasi hicho cha pesa kwani nia ya serikali ni kuona uchumi wa nchi unainuka,” alisema Profesa Muhongo.

Alisema miradi hiyo inagharimu Sh. bilioni 881, inatekelezwa katika awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza ilikamilika Desemba mwaka jana na awamu ya pili yenye miradi 35 imeaanza mwaka huu hadi Juni mwakani.

Hata hivyo, alionya makandarasi watakaokiuka mkataba wa kazi kwa kufanya kazi chini ya kiwango pamoja na kupokea rushwa kutoka kwa wananchi, watafukuzwa zabuni zao kupewa watu wengine.

Mwenyekiti wa Bodi ya Rea, Balozi Ami Mpungwe, alisema viongozi wataendelea kusimamia kazi za chombo hicho ambacho kina wajibu wa kutoa mwelekeo, kusimamia sera na mikakati mbalimbali na kuitekeleza.

 
Na MWandishi Wetu, DAr    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: nuhu baraza    Wednesday, February 05, 2014 18:24:59   
 
hiyo safi sana itapunguza au kumaliza kabisa munkari nahasira ambazo wananchi walikuanazo.
 
 
Mtoa Maoni: Tumain v Temba    Friday, February 07, 2014 13:41:33   
 
Nivizuri ikawa kwa vitendo isiwe tena siasa,Na swala la bei ya umeme ni bora lika tizamwa tena upya kuokoa mazingira'Gesi ya kwetu wenyewe shida ni nini?
 
 
Mtoa Maoni: Moses masokola    Sunday, February 16, 2014 21:05:42   
 
Chalumba mtemi sana duuuu
 
 
Mtoa Maoni: Erickson Mbabe!    Thursday, March 06, 2014 13:28:46   
 
Cyo Siasa Bali Matendo Sasa!!Na Ukwel Utumike.
 
 
Mtoa Maoni: Mchungaji Nuhu Ami Axwesso    Thursday, March 06, 2014 13:35:53   
 
Basi Ni Wakati Wa Kumkumbuka Mungu Jaman Watanzania Wenzangu Maana Pasipo Mungu Hakuna Ki2 Twafanya Basi Tuiombe Nchi Yetu Pamoja Na Serikali.
 
 
       Jumla kuna maoni (11), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za Tanzania
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD
> Mwenyekiti wa CCM Dar aburuzwa mah akamani kwa kusambaza ARV bandia
> BUNGE LA KATIBA LAIVA, JK ataja majina
> Askari afariki dunia kwa kupigwa na jiwe kichwani na mahabusu- ARUSHA
> Serikali yatangaza neema vijijini kuunganisha umeme
> Mwanamke auawa,kichwa chake chakutwa uwanja wa mpira
> Tuna sifa za kukopa -Waziri
> Kila Mtanzania anadaiwa Sh.600,000/ deni la Taifa
> Askari watano wafariki katika ajali -DODOMA
> Hawa hawakuguswa katika mabadiliko mapya
> SURA MPYA
> Rais Kikwete awabwaga watano waliokuwa kwenye baraza la zamani
> Rais Kikwete awaapisha Mawaziri wapya aliowateua
> 13 wapoteza maisha katika ajali -Singida
> Akamatwa kwa kosa la kujifanya Koplo wa JWTZ
> 9 wapoteza maisha katika ajali ya basi -LINDI
> Mkapa achapisha vitabu vya hotuba zake
> 15 wapoteza maisha mgogoro wa ardhi Kiteto
> Wananchi wachoma moto basi lililouwa watoto watatu

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD