|
SURA MPYA |

AshaRose Moja ya mawaziri wapya walioteuliwa jana |
Monday, January 20, 2014 11:58 PM
Katika uteuzi huo mpya wa Rais sura mpya nazo zimeingia ambapo awali hazikuwepo katika baraza teule.
|
Wapya waliyoingia katika baraza jipya akiwemo Dk. Asha-Rose Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Kamani Ole Telele na Mgimwa .
Mwingine ni Mwigulu Nchemba ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara.
Sura zingine mpya ni Jenista Mhagama[Mbunge Peramiho CCM] ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Dk. Pindi Chana [Mbunge wa Viti Maalum], ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,.
Godfrey Zambi[Mbunge Mbozi], anakuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.
Mwingine ni Juma Nkamia [Mbunge wa Kondoa Kusini], anakuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Nkamia kabla ya kuwa mbunge aliwahi kuwa Mwanahabari wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), lakini pia amefanya kazi Voice of America Marekani.
Dk. Kebwe Stephen Kebwe anakuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
|
|
Na MWandishi Wetu, Dar
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Bernard Maira
Tuesday, January 21, 2014 19:52:22
|
|
Mtoa Maoni:
Uncle D
Friday, January 24, 2014 18:02:04
|
|
Mtoa Maoni:
Shukuru basana
Saturday, February 01, 2014 10:58:59
|
|
Mtoa Maoni:
HiSugbsBZ
Tuesday, July 01, 2014 11:54:47
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Habari zaidi za Tanzania |
...Habari Zaidi
|
|
|