|
MANJI atangaza kuachia ngazi Yanga |

|
Wednesday, December 11, 2013 10:21 AM
MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji ametangaza kutogombea tena nafasi hiyo ili kuweza kuwapisha wengine kuongoza klabu hiyo. |
Amesema atakuwa mwanachama wa kawaida na hatagombea kwani madarakani yake yataisha ifikapo Aprili, mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Manji alisema , ni wakati wa kupata viongozi wapya katikia uchaguzi mkuu utakaofanyika May mwakani.
“Ukomo wangu utaishia Aprili mwakani, nawaachia wanachama wengine wenye sifa kugombea”
"Na sitagombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya klabu zaidi ya kubaki kuwa mwanachama wa Yanga” alisema
Katika mkutano huo Manji pia alitumia nafasi hiyo kumtambulisha Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo, Beno Njovu atakayechukua nafasi ya Kaimu Katibu Mkuu, Lawrance Mwalusako. Hata hivyo Manji alisema licha ya kumtangaza Katibu huyo, Bado Mwalusako ataendelea kuitumika Yanga hadi Januari 19, mwakani.
|
|
Na Pilly Kigome, Dar
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
DeClarkes
Wednesday, December 11, 2013 12:14:51
|
|
Mtoa Maoni:
ALEXANDER GEODI
Saturday, January 11, 2014 14:48:21
|
|
Mtoa Maoni:
Heri Machaku
Monday, January 13, 2014 13:53:24
|
|
Mtoa Maoni:
ISAYA MWAIJELEGE
Sunday, April 06, 2014 16:02:38
|
|
Mtoa Maoni:
T7jOMkT4Z1
Tuesday, July 01, 2014 18:37:43
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Habari zaidi za michezo |
...Habari Zaidi
|
|
|