|
Drogba Aitosa Chelsea na Kujiunga na Galatasaray |

Didier Drogba ameingia mkataba wa miezi 18 kuichezea Galatasaray |
Tuesday, January 29, 2013 1:44 AM
Didier Drogba amelitosa dili la bilionea wa Chelsea, Roman Abramovich la kumrudisha tena Chelsea mwezi huu na badala yake ameamua kujiunga na wababe wa Uturuki, Galatasaray. |
Baada ya Chelsea kuendelea kuwakera washabiki wao kwa kutofanya vizuri na kutoka sare ya 2-2 na timu ya daraja la pili ya Brentford, bilionea Roman Abramovich alitoa ruhusa wiki iliyopita Chelsea waanze mazungumzo ya kumrudisha mkongwe Didier Drogba ili aipe nguvu safu ya ushambuliaji ya Chelsea ambayo inaonekana kupwaya.
Abramovich alitoa ruhusa Drogba asajiliwe kwa mkopo toka timu ya Shanghai Shenhua ya China kwa muda wa miezi sita ambapo mwisho wa msimu wangeweza kuuongeza mkataba wake kwa mwaka mmoja.
Taarifa za uhakika zilizotolewa zilisema kuwa mazungumzo ya kumrudisha Drogba, Chelsea yalishafikia mbali kiasi cha kuwapa matumaini Chelsea kuwa mfungaji wao mahiri atatua hapo kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Lakini mbali ya matumaini hayo leo jioni, Drogba ametangaza kujiunga na mabingwa wa Uturuki, Galatasaray.
Drogba ameingia mkataba wa muda wa miezi 18 ambapo atalipwa euro milioni 6 katika kipindi hicho na pia atakuwa akilipwa euro 15,000 kwa kila mechi atakayokuwa akicheza.
Katika mtandao wake wa Twitter, Drogba alisema "Nafasi ya kuichezea timu hii kubwa ya Galatasaray ni nzuri sana kiasi cha kwamba nisingeweza kuikataa".
"Nasubiri kwa hamu kucheza tena katika kombe la mabingwa wa ulaya dhidi ya timu bora za ulaya", aliongeza Drogba akielezea hamu yake ya kuichezea Galatasaray ambayo imefanikiwa kuingia kwenye hatua ya 16 bora katika kombe la mabingwa wa ulaya ambapo mbele yao wanakabiliwa na timu ya FC Schalke 04 ya Ujerumani.
Wiki iliyopita Galatasaray iliwapiku Liverpool na kumsaini nahodha wa Uholanzi, Wesley Sneijder aliyekuwa akiichezea timu ya Inter Milan ya Italia.
Sneijder alipewa mapokezi ya kifalme alipotua Istanbul. Haijulikani hali itakuwaje Drogba atakapotua Istanbul baada ya kumalizika kwa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini. |
|
Nifahamishe.com
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Dulla
Tuesday, January 29, 2013 10:14:29
|
|
Mtoa Maoni:
Mang
Tuesday, January 29, 2013 14:02:52
|
|
Mtoa Maoni:
EWkxonVJlRbcc
Monday, February 11, 2013 03:18:56
|
|
Mtoa Maoni:
wUepRNPJVbE
Wednesday, February 13, 2013 13:18:37
|
|
Mtoa Maoni:
SgvVJrYDILZOFb
Thursday, February 14, 2013 07:32:12
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (16), Soma maoni yote |
|
|
|
Habari zaidi za michezo |
...Habari Zaidi
|
|
|