|
Apiga picha za uchi kupinga katiba ya kiislam |

Alia akiwa amenyanyua juu bendera ya Misri, akiwa na marafiki zaki |
Friday, December 21, 2012 12:36 AM
Mwanamke mmoja anayejihusisha na harakati za kutetea haki za wanawake mwenye uraia wa Misri, amepiga picha za uchi na kuzitupia kwenye blog yake kupinga katiba mpya ya Misri, iliyoandikwa na wanasiasa wa kiislam
|
Mwanaharakati huyo anayeitwa Alia Mahdi ambaye kwa sasa ameweka makazi yake nchini Sweden, alipiga picha hizo akiwa yeye na marafiki zake wa wili wa kike, wote kwa pamoja wakiwa wamesimama uchi mbele ya jengo la ubalozi wa Misri, uliyopo katika mji wa Stockholm, Sweden.
Alia akiwa uchi wa mnyama ulionekana mwili wake ukiwa umepambwa na maaandishi yasemayo “Sheria ya kiislam si Katiba" mwengine aliandika "hapana Waislam, ndiyo kidunia" akionyesha kupinga vyama vya kiislam na kuviunga mkono vyama visivyo vya kisilamu, wa mwisho aliandika" kuwa pamoja na Mors ni mwisho wa dunia".
Alia akiwa amenyanyua juu bendera ya Misri, huku rafiki zake wakiwa wameshika mabango yalioziba sehemu zao nyeti moja likisema "Hakuna dini" na lengine likisomeka "dini ni utumwa", Alia alifanya hivyo akiunga mkono wapinzani wa katiba iliyotangazwa na Rais wa Misri Mohamed Morsi hivi karibu.
Alia hii ni mara ya pili sasa kupiga picha za uchi na kuzitupia kwenye mitandao, mara ya kwanza ilikuwa tarehe 23 Oktoba 2011 alipiga picha za uchi na kuziposti kwenye blog yake akipinga kile ailichokiita ni ubaguzi wa rangi katika jamii kwa kutumia nguvu.
Rais Mohamed Morsi amekuwa akikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa vyama na makundi yasiokua ya dini yanayopinga katiba hio mpya, baada ya kujitoa kujitoa katika mchakato wa kuandaa katiba hiyo katika hatua za mwisho, wakipinga vifungu kadhaa kama vile uislam ndiyo dini ya Taifa na vinginevyo vinavyo husu uislam. |
|
Nifahamishe.com
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Dulla
Friday, December 21, 2012 08:22:12
|
|
Mtoa Maoni:
God will provid
Friday, December 21, 2012 08:24:04
|
|
Mtoa Maoni:
Sheikh Haniwezi
Friday, December 21, 2012 10:19:38
|
|
Mtoa Maoni:
Mugole
Friday, December 21, 2012 13:57:21
|
|
Mtoa Maoni:
SAA-IL
Friday, December 21, 2012 15:11:21
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (64), Soma maoni yote |
|
|
|
Habari zaidi za dunia |
...Habari Zaidi
|
|
|