|
Aliyetangazwa Amekufa, Ahudhuria Mazishi Yake Mwenyewe |

Gilberto Araujo |
Thursday, October 25, 2012 1:55 AM
Mwanaume aliyehudhuria mazishi yake alisababisha kizaa zaa nchini Brazili na kupelekea baadhi ya ndugu zake kuzimia na wengine kumkimbia kwa hofu. |
Muosha magari katika mji wa Alagoinhas nchini Brazili, Gilberto Araujo mwenye umri wa miaka 41, alisababisha mtafaruku mkubwa pale alipohudhuria mazishi ambayo yalikuwa kwaajili yake.
Mtafaruku huo ulitokea pale kaka yake Gilberto, Jose Marcos, alipotakiwa na polisi aende hospitali kuutambua mwili wa ndugu yake ambaye alitajwa kuwa ameuliwa kwa kupigwa risasi.
Jose aliutambua mwili huo na kusema ni kweli wa mdogo wake Gilberto na kuruhusiwa kuuchukua mwili huo kwaajili ya taratibu za mazishi.
Wakati taratibu za mazishi zikielekea ukingoni, Gilberto aliwahi nyumbani kwao baada ya kukutana na mtu aliyempa taarifa kuwa nyumbani kwao wanajua amefariki dunia na hivyo mazishi yanafanyika.
Baadhi ya watu kwenye mazishi walizimia na wengine walikimbia baada ya kumshuhudia aliyetajwa kuwa ni marehemu ametokea mbele yao akiwafuata.
Shemeji yake Gilberto akilielezea tukio hilo alisema kuwa mtafaruku ulianza pale habari zilipoanza kusambaa mtaani kuwa muosha magari ameuliwa kwa kupigwa risasi.
"Polisi walimuita mume wangu na kumuambia kuwa kaka yake ameuliwa kwa kupigwa risasi na mwili wake uko monchwari hivyo alitakiwa aende kuutambua", alisema mke huyo wa kaka yake.
Iligundulika baadae kuwa mtu halisi aliyeuliwa katika tukio hilo alikuwa ni Genivaldo Santos Gama.
"Kwa jinsi walivyokuwa wakifanana na wote walikuwa waosha magari ndio maana watu walidhani ni Gilberto ameuliwa", alisema mama yake Gilberto.
"Nina furaha sana, kitu gani ambacho mama anaweza kusema baada ya kuambiwa kuwa mtoto wake amefariki halafu baadae anamuona yuko hai", alisema mama yake Gilberto, bi Marina Santana. |
|
Nifahamishe.com
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Faraja McHarris
Thursday, October 25, 2012 06:54:20
|
|
Mtoa Maoni:
kadwame
Thursday, October 25, 2012 18:38:47
|
|
Mtoa Maoni:
alobadilijina
Friday, October 26, 2012 20:45:39
|
|
Mtoa Maoni:
MR. GROOM FOONG
Friday, November 02, 2012 08:57:50
|
|
Mtoa Maoni:
j . j mpingo
Saturday, November 03, 2012 14:29:35
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (9), Soma maoni yote |
|
|
|
Habari zaidi za dunia |
...Habari Zaidi
|
|
|