|
Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0 |

Hispania wamekuwa mabingwa wa mataifa ya ulaya kwa mara nyingine tena |
Monday, July 02, 2012 2:03 AM
Hispania imekuwa nchi ya kwanza kutwaa makombe matatu makubwa duniani kwa mpigo baada kuibugiza Italia mabao 4-0 na kulitwaa tena kombe la mataifa ya ulaya. |
Mabingwa wa ulaya na mabingwa wa dunia, Hispania au maarufu kwa jina la "La Roja" wamejiongezea taji jingine kwa kutwaa tena kombe la euro 2012.
Katika mechi hiyo ya fainali iliyochezwa nchini Ukraine, Hispania waliwafundisha soka Italia kwa pasi zao fupi fupi wakitawala sehemu kubwa ya mechi hiyo.
Licha ya vyombo vya habari kumbeza kocha wa Hispania kwa staili yake ya kuchezesha viungo sita bila ya mshambuliaji, staili yake hiyo ilisaidia kumzima nyota wa Italia, Andrea Pirlo na kumfanya Mario Balotelli kuwa msindikizaji uwanjani.
Magoli mawili ya Hispania kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa David Silva kwenye dakika ya 14 na beki Jordi Alba kwenye dakika ya 41 yalisaidia kuivunja nguvu Italia kabla ya Fernando Torres na Juan Mata kulipigilia jeneza la Italia misumari ya mwisho kwenye dakika za mwisho za kipindi cha pili.
Kwa ushindi huu Hispania imefanikiwa kuvunja rekodi nyingi za mashindano ya soka ya kimataifa.
Hispania imekuwa nchi ya kwanza kuweza kufanikiwa kuutetea ubingwa wake wa kombe la mataifa ya ulaya. Hispania pia imeweka historia ya kutwaa kombe la mataifa ya ulaya kwa idadi kubwa ya magoli kuliko mechi zote za fainali za Euro zilizowahi kuchezwa.
Hispania imekuwa nchi ya kwanza kutwaa makombe matatu makubwa kwa mfululizo baada ya kutwaa Euro 2008 na kombe la dunia 2010.
Fernando Torres amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli katika mechi mbili tofauti za fainali za kombe la mataifa ya ulaya. |
|
Nifahamishe.com
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
(Nundaa)
Monday, July 02, 2012 08:06:42
|
|
Mtoa Maoni:
zungut
Monday, July 02, 2012 13:00:13
|
|
Mtoa Maoni:
(Nundaa)
Monday, July 02, 2012 14:18:51
|
|
Mtoa Maoni:
Misha
Monday, July 02, 2012 15:45:34
|
|
Mtoa Maoni:
(Nundaa)
Tuesday, July 03, 2012 07:22:35
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (9), Soma maoni yote |
|
|
|
Habari zaidi za michezo |
...Habari Zaidi
|
|
|