Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Ewura yashtua wabunge kwa kuwa na matumizi makubwa
Advertisement


Wednesday, June 03, 2009 5:06 PM
KAMATI ya Bunge ya Mashirika ya Umma,imeshtushwa na matumizi makubwa yanayofanywa na Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji(EWURA) kwa wafanyakazi wake.
Gharama hizo ni pamoja na zile zinazotumika kwa ajili ya matibabu ambapo kwa mwaka zinafika milioni 150,vikao vya bodi milioni 225,mafuta milioni 90 kwa ajili ya magari yao.

Wakati gharama kwa ajili ya mawasilinao ni shilingi milioni 66 kwa mwaka ambapo kila mfanyakazi huwekewa muda wa maongezi kutokana na Idara anayoifanyia kazi ikifika.

Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti mara baada ya kupokea taarifa ya Mkaguzi wa hesabu za Serikali(CIG),wabunge hao walisema gharama hizo ni kubwa sana ukilinganisha na uchanga wa Mamlaka hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo,Halima Mdee,alisema kitendo cha Mamlaka hiyo kugharamia matibabu ya mfanyakazi mmoja mmoja kuna hatari kubwa ya kughushiwa kwa risiti kwa matibabau ambayo mfanyakazi hajayapata jambo amablo litaitia Mamlaka hasara.

“Mimi kwa ningeshauri katika hili ili kupunguza gharama hizi ni vyema Ewura mkajinga na Mfuko wa Bima ya Afya,ambapo mfuko huo una uwezo wa kugharamia matibabu ndani na nje ya nchi kwa magonjwa takribani 999 bila kujali kiwango cha mshahara anachopata mfanayakazi.

“Kwa staili mnayoitumia kutoa fedha za matibabu ipo siku atakuja Mkurugenzi yoyte katika Mamlaka hiyo,asiyekuwa na huruma na fedha za walipa kodi,kwenda kutibiwa mafua nje kwa sababu tu fedha hizo zinatolewa na ofisi,”alitahadharisha Mdee.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Kabwe Zitto,alisema haoni haja ya wafanyakazi kuwekewa muda wa maongezi kwenye simu zao na badala yake wanagetumia ‘rediocal’ ili kupunguza gharama zisizo za lazima.

“Katika taarifa yenu inaonyesha kwamba kwa mwaka kiasi cha shilingi milioni 66 zinatumika kwa ajili ya kuwekea wafanyakazi muda wa maongezi,hii ni pesa nyingi sana inatumika,na mna uhakika gani kama muda huo wa maongezi unatumiwa kwa ajili ya shughuli za kazini tu na si vinginevyo,?”alihoji Zitto.

Akijibu hoja hizo,Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka hiyo,Simon Sayore,alisema sula la mafuta walipendekeza kutoa mkopo wa magari kwa wafanyakazi na kuwakata kidogokidogo kwenye mishahara yao baada ya kuona endapo wangetumia magari ya ofisi gharama ingekuwa kubwa zaidi ya ilivyo sasa.

Wakati kuwawekea muda wa maongezi,Sayore alisema kunatokana na aina za kazi ambazo wamekuwa wakifanya kwa masaa kwamba sio kazi za kukaa ofisini bali ni kazi za kwenda mitaani.

Akifafanua zaidi alisema kwa upande wao utumiaji wa ,redio call’ wanaona sio mawasiliano salama kwao ukilinganisha na kazi ambazo wanazifanya.

Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,Huruna Masebu alisema suala la kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya watakutana na kulijadili kwa unadani ili kuona ni jinsi gani wataweza kujiunga.


 
Na Zainabu Rashid    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Chioky    Saturday, July 11, 2009 16:27:14   
 
Hizi pesa ni zile 1% tunazokatwa wateja katika bili za Tanesco. Sisi wananchi tunaumia EWURA wanastarehe na pesa zetu. Hivi kuna maana gani kutoza hiyo 1% katika bill ya Tanesco wakati matumizi ni hayo? Wabunge, kwanini msipeleke hoja bungeni hiyo 1% tunayotozwa wananchi ikafutwa maaana EWURA wanazo pesa nyingi za kuchezea wakati sisi wanachi tunabebeshwa mzigo huo usiokuwa na sababu wala tija.
 
 
Mtoa Maoni: moms016    Sunday, August 09, 2009 01:28:35   
 
nilikuwa na swala (suali) hivi kwa nini haijawahi kutokezea wabunge kuandamana na kudai waongezewe mishahala yao kama ilivyo kwa sekta ya walimu na udaktari na vitengo vyengine?
UBUGUVU- KAKA-MAMA K-haya mazee..

 
 
Mtoa Maoni: Mtata dot com    Monday, August 24, 2009 11:19:47   
 
Nchi hii inaliwa na wapuuzi wachache hebu cheki hilo swala la umeme mzigo unatuelemea sisi kumbe mavitu kibao yamekua associated na hizi gharama vitu kama richmond na hawa jamaa wa ewura wanaokula waziwazi lakini wanaachwa tu....Imefika wakati sasa tuonyeshe mfano hata kwa kunyonga Fisadi hata mmoja hadharani iwe fundisho kwa wale waliosalia.Kikwete sasa inabidi awe makini na watu wake anaowapa dhamana ya kuliongoza taifa hili isiwe kwa kulipa fadhila lasivyo tutakuja kuuana kama kuku..
 
 
Mtoa Maoni: haruna    Tuesday, December 08, 2009 14:25:54   
 
sioni haja yakujadili EWURA,mafisadi wangapi wameiingizia serikali hasara na imekuwa siasa tu.je wabunge wanalipwa kiasi gani na kwa kazi ipi waifanyayo?kwanini tuoe dagaa wakati Sangara yu hai?
 
 
Mtoa Maoni: Hamrabi    Saturday, December 12, 2009 18:13:04   
 
Unaona ulaji huo,punda afe mzigo ufike.Huo ndio ulaji ndg zangu.Mimi na wewe ndio punda lazima tufe na abdalah afike.Upuuzi mtupu.
 
 
       Jumla kuna maoni (12), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za biashara na uchumi
> Benki ya Vijana kuzinduliwa
> Jishindie Milioni 3 Kila Siku na Vodacom
> Precision Air yaanza safari za Bukoba
> Precision Air yazindua nauli maalumu ya Sunrise
> Zain sasa ni Airtel
> Nokia Yatoa Simu Zinazochajiwa na Baiskeli
> TBL yapigwa faini kuvuruga ushindani wa kibiashara
> Gharama za huduma za simu zazidi kupungua
> Uzalishaji wa Bia Mpya TBL Wasimama Baada ya Mitambo Kuungua
> Ewura yashtua wabunge kwa kuwa na matumizi makubwa
> Zain yaja na Balckberry Pre Paid
> Wakulima wa embe wasaidiwa milioni 126/-
> BOT, NMB ijiunge na umoja switch kuondoa kero
> Soko la samaki laingiza bilioni mbili
> Serengeti Breweries yatunzwa tunzo ya dhahabu
> VIDEO - Dhahabu Zatumika Kununulia Mkate Zimbabwe
> ATM 'Yapagawa' na Kuwajaza Watu Mapesa Italia
> Wafanyabiashara Watakiwa Kujitangaza
> BET Yatoa Elimu Kwa Wajasiliamali Nchini
> Wengi hawajui kama simu za zamani zinaweza kutumika kutengeneza vitu vingine
> Mmea wa Mbuyu Unatakiwa Kuzalishwa Kwa Wingi- Wizara
> Arusha Thomson Safaris named among 2009 Best Adventure Travel Companies on Earth
> Mifuko ya Rambo kupigwa marufuku Tanzania
> Uuzaji wa Pamba Nje Marufuku
> Uzalishaji Korosho Utashuka

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD