|
Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan |

|
Saturday, June 28, 2014 10:51 PM
Waislamu duniani leo wanaanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan huku wengine wakitarajiwa kuanza kufunga kesho jumapili |
Waislamu wanauanza mwezi wa tisa wa kalenda ya kiislamu ambao hujulikana zaidi kama mwezi wa Ramadhan kwa kujizuia kula na kunywa kuanzia alfajiri ya kweli inapochomoza hadi jioni jua linapozama. Kufunga ni moja ya nguzo tano za Uislamu.
Kuanza na kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan hutegemea na kuandama kwa mwezi lakini kumekuwa na mgongano juu ya njia za kuona kuandama kwa mwezi. Baadhi ya nchi hutaka mwezi lazima uonekane kwa macho na hukataa kutambua kuandama kwa mwezi kwa kutumia njia za kisayansi.
Nchini Yemen,Viongozi wa dini ya kiislam jana ijumaa wamethibitisha kuandama kwa mwezi wametangaza kuwa jumamosi ndio mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Hata hivyo nchi ya Saudi Arabia majirani wa Yemen imetangaza kuwa wao wataanza kufunga jumapili kwakuwa hawajauona mwezi nchi humo.
NIFAHAMISHE.COM inawatakia waislamu wote duniani mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
|
|
Nifahamishe.com
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Remmy
Monday, June 30, 2014 23:11:41
|
|
Mtoa Maoni:
Mwalimu
Tuesday, July 08, 2014 00:22:43
|
|
Mtoa Maoni:
FATMA MOH'D
Tuesday, July 15, 2014 12:58:34
|
|
Mtoa Maoni:
ubuguvu
Sunday, July 27, 2014 07:58:01
|
|
Mtoa Maoni:
MUISLAM
Saturday, August 09, 2014 15:27:05
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (10), Soma maoni yote |
|
|
|
Habari zaidi za Tanzania |
...Habari Zaidi
|
|
|