Kompyuta na Monitors, Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Rais Kikwete awaapisha Mawaziri wapya aliowateua

NewsImages/7098898.jpg
Rais Kikwete pichani
Monday, January 20, 2014 11:38 PM
RAIS wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania leo amewaapisha mawaziri na manaibu wake Ikulu kufuatia uteuzi wake alioufanya jana.

Rais Jakaya Kikwete jana alifanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa kujaza nafasi tano zilizokuwa wazi huku wizara nyingine amezibadilisha na wizara nyingine hakuzigusa katika mabadiliko hayo.

Rais amejaza nafasi za wizara zilizoachwa wazi baada ya mawaziri wake kujiuzulu na wengine kutakiwa kujiuzulu.


Mawaziri hao walitakiwa kujiuzulu baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kubaini uozo katika operesheni Tokomeza Ujangili

Ikiwemo kusababisha watu wasio na hatia kuuawa, kuteswa, kujeruhiwa, kudhalilishwa, kubakwa na vitendo vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na upotevu wa fedha na mali hususani mifugo.

Ambapo waliotakiwa kujizulu kutokana na sakata hilo akiwemo aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David Mathayo na Balozi Khamisi Kagasheki [Maliasili] alijiuzulu mwenyewe baada ya kutolewa kwa ripoti hiyo.

Na aliyekuwa waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, alifariki dunia Januari Mosi mwaka huu huko nchini Afrika Kusini, hivyo kufikisha mapengo ya wizara tano ambapo tayari zimeshateuliwa wahusika wengine wapya.

Katika kuziba nafasi hizo Rais Kikwete, amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwa Waziri kamili wa Wizara hiyo na Naibu wake akiwa ni Mahmoud Hassan Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini (CCM).

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa amepewa Dk. Hussein Ali Mwinyi ambapo awali kabla ya mabadiliko alikuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Wizara ya Mambo ya Ndani amepewa Mathias Chikawe ambaye kabla ya mabadiliko alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria huku Naibu wake akibaki kuwa Pereira Silima.

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, amepewa Dk. Titus Kamani, ambaye ni Mbunge wa Busega wilayani Magu mkoani Mwanza huku naibu wake ameteuliwa kuwa Kaika Ole Telele ambaye ni Mbunge wa Ngorongoro.

Mabadiliko hayo ni kwa nafasi ambazo mawaziri wake walitakiwa kujiuzulu.


 
Na Mwandishi Maalum, Ikulu    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: neem    Wednesday, January 22, 2014 02:12:49   
 
Mawaziri wapya ,ni uteuzi mzuri mimi nimeupenda hawsa kwa wakina
Mama nimefurai sana ,hapo mr.president umefanya vizuri,kwa
upande wangu sijui kwa wengine.
Zaidi kuona waziri waFEDHA ni mwanamke safikabisa kazi itakuwa nzuri,afanye bidii kama yule wa Nigeria Mrs Ngozi anasifiwa sana
kwa kuinua uchumi wa nchi yake bila kumsahau aliyekuwa waziri wa fedha wa Msumbiji alikuwa mwamke
alifanya vizuri mpaka hela zao zikawa za thamani,naona na TZ
tunaitaji hivyo,sio sh.1 kwa sh18
19shTZ shame.


 
 
Mtoa Maoni: FWyOxKAv    Tuesday, July 01, 2014 14:09:31   
 
Whoever edits and puelbshis these articles really knows what they're doing.
 
 
Mtoa Maoni: A wonderful job. Super helpful intaomofirn.     Monday, November 23, 2015 18:52:11   
 
A wonderful job. Super helpful intaomofirn.
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za Tanzania
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD
> Mwenyekiti wa CCM Dar aburuzwa mah akamani kwa kusambaza ARV bandia
> BUNGE LA KATIBA LAIVA, JK ataja majina
> Askari afariki dunia kwa kupigwa na jiwe kichwani na mahabusu- ARUSHA
> Serikali yatangaza neema vijijini kuunganisha umeme
> Mwanamke auawa,kichwa chake chakutwa uwanja wa mpira
> Tuna sifa za kukopa -Waziri
> Kila Mtanzania anadaiwa Sh.600,000/ deni la Taifa
> Askari watano wafariki katika ajali -DODOMA
> Hawa hawakuguswa katika mabadiliko mapya
> SURA MPYA
> Rais Kikwete awabwaga watano waliokuwa kwenye baraza la zamani
> Rais Kikwete awaapisha Mawaziri wapya aliowateua
> 13 wapoteza maisha katika ajali -Singida
> Akamatwa kwa kosa la kujifanya Koplo wa JWTZ
> 9 wapoteza maisha katika ajali ya basi -LINDI
> Mkapa achapisha vitabu vya hotuba zake
> 15 wapoteza maisha mgogoro wa ardhi Kiteto
> Wananchi wachoma moto basi lililouwa watoto watatu

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD