Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Watoto wafariki kwa kutumbukia katika shimo la choo

NewsImages/7089258.jpg
Sunday, January 05, 2014 12:59 PM
WATOTO wawili ndugu moja wamefariki dunia juzi baada ya kutumbukia kwenye shimo la choo ambalo lilikuwa wazi halijafunikwa likiwa halijamalizika ujenzi.

Watoto hao ambao walikuwa wakicheza na watoto wenzao wenyeji karibu na shimo hilo na hatimaye walitumbukia humo na kupoteza maisha kwa kuwa lilikuwa na maji.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea huko maeneo ya Yombo Machimbo
na kuleta huzuni na simanzi kubwa kwa wakazi wa maeneno hayo.

Ilidaiwa na mmoja wa jirani wa aliyepoteza watoto hao kuwa, watoto wao walikuja kutembea kwa ndugu yao huyo na baadae kujichanganya na watoto wenzao wa maeneo hayo katika michezo ya kawaida ya watoto

Imedaiwa baadae mama huyo alianzakuwatafuta watoto hao baada ya kuona muda mwingi hakuwaona kurudi na ndipo alipoanza kuuliza kwa majirani iwapo wamewaona watoto hao na kila alipogonga nyumba ya jirani kuwaulizia wamekuwa wakijibu hawajawaona.

Ndipo kwa ushirikiano wa majirani walianza kuwasaka watoto hao huku na huko na kijana mmoja akatoa wazo waangalie visimani na walipoanza kuangalia visimani cha kwanza waligonga mwamba na walipoenda kuangalia katika shimo hilo walifanikiwa kuona mtoto mmoja akiwa anaelea juu ya maji ya shimo hilo.

Baada ya kuona mwili mmoja walikwenda kuripoti kituo cha polisi kwa uthibitisho na polisi ilipofika walitoa amri ya kujaribu kuingia ndani yashimo hilo huenda huyo mmoja likuwa chini

Ndipo kijana mmoja alijitolea na ngazi ikashushwa akaingia chini ya shimo hilo na aliukuta mwili huo ukiwa chini kabisa ya matope na aliutoa ukiwa na tope

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Englibet Kiondo, alithibitisha kutokea kwa tukio hili

Watoto hao wametajwa kuwa ni Abubakari Mohamed (3) mkazi wa Vingunguti na Abdulmalick (3) mkazi wa Machimbo.


 
Na Pilly Kigome, DAr    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Remyy    Sunday, January 05, 2014 16:41:57   
 
Tatizo la TZ ni kua hakuna utamaduni wa kuweka viashiria au vizuizi kwenye mashimo,hasa huko mijini. Simo likichimbwa baada ya kazi nilazma liwekwe uzio hata kama kesho uchimbaji utaendelea. Barabarani mashimo kila mahali na hakuna vizuizi wala viashiria vya kuonyesha hatari. Kwahio iwekwe sheria, mtu kuacha shimo wazi iwe ni mijini au vijijini achukuliwe hatua kali na hata barabara zenye mashimo manispaa husika ichkuliwe hatua kali nasiokungoja mpka mtu anguke humo,hii niaibu hasakwawagen
 
 
Mtoa Maoni: SEEKER-OF-TRUTH    Sunday, January 05, 2014 17:33:35   
 
Kila nafsi itaonja umauti, na kila mmoja atalipwa alicho tenda siku ya Kiama. Mimi kama mzazi, habari hii imenigusa sana, natamani ningewajua wafiwa nishirikiane nao kwa hali na mali.

Hadithi sahihi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Salla-lahu alaihi wasallam)inasema kua mtu yeyote atakaefiwa na watoto wadogo wawili, Mola atampooza kwa kumuingiza peponi.

Namuomba Allah awarehemu watoto hao, na awape subira wazazi, amin.

 
 
Mtoa Maoni: neem    Sunday, January 05, 2014 18:10:57   
 
Poleni sana wafiwa,inasikitisha sana,watoto wawili kupoteza maisha
namna hiyo,walikwenda kucheza kama
wenzao hawakurudi nyumbani wazima
wanarudi maiti.Sikitisho na simanzi.Na poleni mwenye hilo shimo sijui atasema nini,watoto wawili.Tunajua nibahati mbaya lakini watu wajue mtu yeyote akichimba shimo lazima aweke kitu
cha kuzuia mtu yeyote au mnyama hasipite hapo nihatari, uku wenzetu
wanaweka taa inawaka au utepe mwekundu hatari usikaribie,anaogopa kubamwa na sheria.Mwaka umewanzia vibaya .

 
 
Mtoa Maoni: Uncle D    Wednesday, January 08, 2014 10:49:39   
 
Nimeumia sana kwa kweli.Ila nchi yetu kuna kitu ambacho tumekikosa kama Remyy alivosema.Huwa tunakosa mafunzo ya vihatarishi katika maeneo ya kazi na makazi.Migodini hili tatizo halipo lakini sio kwa migodi ya wachimbaji wadogo wadogo.Nikweli mwenye shimo amefanya uzembe lakini kumshitakitutakuwa tumemuonea hii ni bahati mbaya maana hilo kosa liko kwetu wote serikali na sisi wenyewe.Na mkumbuke serikali ni mimi na wewe.Ila wakuu waserikali muangalie hili jambo muliongelee kwenye bunge
 
 
Mtoa Maoni: sokwe    Friday, January 10, 2014 07:37:21   
 
habari zako ni zilezile toka weeeeeeeeeeee
 
 
       Jumla kuna maoni (9), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za Tanzania
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD
> Mwenyekiti wa CCM Dar aburuzwa mah akamani kwa kusambaza ARV bandia
> BUNGE LA KATIBA LAIVA, JK ataja majina
> Askari afariki dunia kwa kupigwa na jiwe kichwani na mahabusu- ARUSHA
> Serikali yatangaza neema vijijini kuunganisha umeme
> Mwanamke auawa,kichwa chake chakutwa uwanja wa mpira
> Tuna sifa za kukopa -Waziri
> Kila Mtanzania anadaiwa Sh.600,000/ deni la Taifa
> Askari watano wafariki katika ajali -DODOMA
> Hawa hawakuguswa katika mabadiliko mapya
> SURA MPYA
> Rais Kikwete awabwaga watano waliokuwa kwenye baraza la zamani
> Rais Kikwete awaapisha Mawaziri wapya aliowateua
> 13 wapoteza maisha katika ajali -Singida
> Akamatwa kwa kosa la kujifanya Koplo wa JWTZ
> 9 wapoteza maisha katika ajali ya basi -LINDI
> Mkapa achapisha vitabu vya hotuba zake
> 15 wapoteza maisha mgogoro wa ardhi Kiteto
> Wananchi wachoma moto basi lililouwa watoto watatu

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD