|
Yanga na Simba Hakuna Mbabe 3-3 |

|
Sunday, October 20, 2013 5:17 PM
Vijana wa Jangwani, Yanga wameshindwa kulinda magoli matatu waliyoyapata kipindi cha kwanza na kuwaruhusu Simba kusawazisha magoli yote kwenye kipindi cha pili. Mechi imeisha Simba 3 - Yanga 3. |
Yanga ilienda mapumziko ikiwa mbele 3-0 kufuatia magoli yaliyofungwa na Ngassa dakika ya 14 wakati Kiiza aliipatia Yanga magoli mawili kwenye dakika za 35, 45.
Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko na walitoka Abdulhalim Humud na Chanongo na kuingia William Lucian na Said Hamisi.
Mabadiliko hayo yalibadilisha upepo wa mchezo kwa Simba kuanza kuutawala mchezo na kuwapeleka spidi Yanga.
Simba ilipata magoli mawili ya haraka kupitia kwa Betram Mombeki dakika ya 55 na Joseph Owino dakika ya 57.
Dakika ya 83, Gilbert Kaze aliipatia Simba bao la tatu akiunganisha krosi safi ya faulo iliyopigwa na Chollo na kuifanya mechi hiyo imalize kwa Simba 3-3 Yanga. |
|
Nifahamishe.com
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
michael A
Sunday, October 20, 2013 20:44:09
|
|
Mtoa Maoni:
GRA HOPE
Monday, October 21, 2013 10:37:53
|
|
Mtoa Maoni:
www.rusumo.net
Monday, October 21, 2013 16:41:13
|
|
Mtoa Maoni:
Ubuguvu
Monday, October 21, 2013 17:54:18
|
|
Mtoa Maoni:
Rumao jackson
Tuesday, October 22, 2013 08:45:58
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (11), Soma maoni yote |
|
|
|
Habari zaidi za michezo |
...Habari Zaidi
|
|
|