Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Yanga Yawabamiza Wasauzi 3-2

NewsImages/6767282.jpg
Sunday, January 20, 2013 3:42 AM
Mabingwa wa kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati almaarufu kombe la Kagame, timu ya Young Africans Sports Club imeifunga timu ya Black Leopard ya Afrika Kusini mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Young Africans iliyokuwa nje ya nchi kwa kambi ya mafunzo takribani wiki ilikuwa ikicheza mbele ya washabiki wake, iliweza kucheza soka safi na la kuvutia kipindi chote cha mchezo huku Black Leopard ikipata wakati mgumu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Didider Kavumbagu alikosa bao la wazi dakika ya 21 ya mchezo akiwa yeye na mlinda mlango wa Black Leopard Ayanda Mtshali, lakini shuti alilopiga lilipaa juu ya lango la timu hiyo.

Yanga iliednelea kuutawala mchezo kwa wachezaji wake kupigiana migongeo mizuri na kuutawala mchezo hasa eneo la kiungo, Kabange Twite alishindwa pi akuipatia Yanga bao katika dakika ya 25 baada ya kushinda kumalizia pasi safi ya Mbuyu Twite.

Dakika ya 32 Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa Balck Leopard Harry Nyirenda kumuangusha Haruna Niyonzima katika eneo la hatari, amabpo mwamuzi Hashim aliamuru upigwe mkwaju wa penati na Jerson Tegete kuukwamisha mpira huo wavuni.

Yanga iliongeza kasi ya kusaka bao la pili lakini shambulizi liliofanywa na Mbuyu Twite liliokolewa na mlinda mlango wa Black Leopard Matshal kabla ya Mbuyu tena kupiga kichwa kilichopaa mita chahce juu ya lango la timu ya Black Leopard.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Young Africans 1 - 0 Black Leopard.

Kipindi cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo kocha Brandts aliwatoa Kabange Twite, Mbuyu Twite na golikipa Ally Mustafa 'Barthez' nafasi zao zikachukuliwa na Juma Abdul, Saimon Msuva na golikipa Said Mohamed.

Dakika ya 47, Humphrey Khoza aliipatia Black Leopard bao la kusawazisha kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Edagr Manaka kufutia kutokuwepo kwa mawasilaino kati ya mlinzi Nadir Haroub na mkinda mlango wake Said Mohamed.

Kiungo chipukizi Frank Domayo aliipatia Young Africans bao la pili dakika ya 63 ya mchezo, akimaliza pasi safi iliyopigwa na kiungo Haruna Niyonzima na mpira huo kumkuta Domayo ambaye alimchambua mlinda mlango wa Black Leopard Mtishal na kuhesabu bao la pili.

Dakika 10 baadaye mshambuliaji Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la tatu kwa umakini akimalizia pasi ya kungo mshambuliaji Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa timu ya Black Leopard na kumpasia mfungaji aliyeukwamisha mpira huo wavuni.

Jerson Tegete nusra angeipatia Young Africans bao la nne, kufuatia lakini krosi iliyopigwa na Saimon Msuva kuokolewa na mlinzi wa Black Leopard sentimeta chache pemebeni mwa lango huku Tegete tayari akiwa tayari kwa kuukwamisha mpira huo.

Dakika ya 89, Black Leopard ilijipatia bao la pili kwa mkwaju wa penati kupitia kwa mshambuliaji wake Rodney Magalela kufuatia mlinzi wa kulia wa Young Africans kumcheza madhambi mshambuliaji huyo katika eneo la hatari.

Mpaka mpira unamalizika Young Africans 3- 2 Black Leopard.

Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake kwa kupata ushindi huo wa leo, kwani timu ya Black Leopard ni timu nzuri, imecheza vizuri lakini mwisho wa siku vijana wangu walikuwa ni bora zaidi ndio maana wameibuk ana ushindi huo.

Kambi yetu ya mafunzo nchini Uturuki imetusaidia sana, wachezaji wanacheza kwa kujiamini wametulia hawana presha ya mchezo, hali inayopelekea kucheza migongeano kwa uhakika na hii ni dalili tosha kuwa tupo tayari kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom alisema 'Brandts'

Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez'/Said Mohamed, 2.Mbuyu Twite/Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Kabange Twite/Saimon Msuva, 8.Frank Domayo, 9.Didier Kavumbagu/Said Bahanuzi, 10.Jerson Tegete/George, 11.Haruna Niyonzima

Black Leopard: 1.Ayanda Mtshali, 2.Ernort Dzaga, 3.Nkosiyabo Xakane, 4.Harry Nyirenda, 5.Humphrey Khosa, 6.Munganga Djunga Jean, 7.Mongezi Bobe, 8.Thomas Madimba, 9.Abbas Amidm, 10.Edagr Manaka 11.Rodney Ramagalela

 
Source: Tovuti ya Yanga    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: RAJAB CHRISTIAN    Monday, January 21, 2013 06:05:38   
 
HOW'S Hanifa Salum Hassan DOIN? Mtoto yule anapona katika Jina lipitalo majina yooooooooooote
THE
LORD JESUS CHRIST
THE SON OF
THE LIVING GOD
HALLELUJAH!!! YEAH!!!

 
 
Mtoa Maoni: MARK.MUSHI WA I    Monday, January 21, 2013 18:34:28   
 
MARK.MUSHI WA ITALY SHABIKI NAMBA 1 WA SIMBA NA CHELSEA,ILA NAWAPA PONGEZI YANGA KWA USHINDI,AYA NILIKUWA TANZANIA NILIENDA KUFUNGA HARUSI ILA KWA SASA NIMERUDI ITALY.NAPATIKANA KWA NAMBA YANGUILEILE YA MKONONI NA PICHA ZA HARUSI NA VIDEO MTAZIONA HAPAHAPA,CM NIILEILE,+393336989592.UBUGUVU UKO KAKA?CKU NJEMAA...
 
 
Mtoa Maoni: zsILQrrVQqCXorK    Monday, February 11, 2013 20:12:07   
 
January 30, 2011 11:16 pm by Hi Yolanda,Great post about diaspora folks in Mexico. I just moved to Mexico City (TODAY) and would love to cocennt with people here. I do corporate partnerships for an international agriculture institute based here. It would be great to share knowledge maybe over coffee.Thanks!
 
 
Mtoa Maoni: eeaEKtGcVeogjmX    Thursday, February 14, 2013 07:32:53   
 
KOfwSv , [url=http://jfkrmnilojlh.com/]jfkrmnilojlh[/url], [link=http://qxhewxrppdjy.com/]qxhewxrppdjy[/link], http://qrkoijozhver.com/
 
 
Mtoa Maoni: FLENK    Wednesday, December 25, 2013 06:59:33   
 
YANGA MNATISHA NIKO BUKOBA.WILAYA MLEBA
 
 
       Jumla kuna maoni (12), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za michezo
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> MANJI atangaza kuachia ngazi Yanga
> Yanga na Simba Hakuna Mbabe 3-3
> LIVE VIDEO - TANZANIA - IVORY COAST High Quality
> Taifa Stars Yafa Kiume Morocco, Yalala 2-1
> Mechi ya Simba na Yanga Yaingiza Milioni 500
> VIDEO - Nyota wa Liverpool, Suarez Amng'ata Mkono Beki wa Chelsea
> Drogba Aitosa Chelsea na Kujiunga na Galatasaray
> VIDEO - Staili Mpya ya Kushangilia Goli Kwa Makalio
> Yanga Yawabamiza Wasauzi 3-2
> Yanga Yatoka Droo na Wajerumani
> Zanzibar Heroes ya futwa kwa utovu wa nidhamu
> KILIMANJARO STARS YATOLEWA CHALLENGE
> VIDEO - Jamaa Anayeipenda Yanga Kuliko Kitu Chochote
> Simba na Yanga Hakuna Mbabe, Zatoka Sare 1-1
> Kuiona Mechi ya Simba na Yanga ni 5000/=
> Simba Yashushiwa Kichapo cha Mabao 3-1 na Azam, Yatolewa Kombe la Kagame
> Yanga Yatinga Nusu Fainali Kombe la Kagame, Yaibanjua Mafunzo
> Simba Nayo Yabugizwa 2-0 na URA ya Uganda
> Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0
> Drogba Atimukia China, Kulipwa Kitita cha Nguvu
> Maximo Arudi Nchini Toka Brazili Kuifundisha Yanga
> Beki wa Simba Atimukia Yanga Kwa Milioni 30
> Chelsea Mabingwa Wapya wa Ulaya, Yaizamisha Bayern Munich
> Manchester City Yatawazwa Mabingwa wa Uingereza

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD