Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Yanga Yatoka Droo na Wajerumani

NewsImages/6744146.jpg
Sunday, January 06, 2013 2:40 AM
Mabingwa wa kombe la Kagame, Yanga, ambao wanaendelea kujifua nchini Uturuki kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania, wametoka sare ya 1-1 na timu ya Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki.
Timu ya Young Africans Sports Club imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jumamosi jioni katika uwanja wa Adora Football pembeni kidogo ya mji wa Antalya.

Armini Bielefeld ilianza soka kwa kasi kwa lengo la kujipatia bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Yanga na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' ilikuwa kikwazo kwao kwani mashambulizi yao yaliishia mikononi mwake.

Ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu Young African iliweza kuonyesha soka safi katika kipindi cha kwanza hali iliyowashangaza wajerumani hao na kipindi cha pili kuamua kufanya mabadiliko ya kikosi kizima.

Viungo wa Yanga Frank Domayo, Haruna Niyonzima na Kabange Twite waliweza kutawala mchezo kwa dakika 45 zote za kipindi cha kwanza huku baadhi ya wajerumani waliokuwa wakishuhudia mchezo huo kushangazwa na kiwango cha timu ya Yanga

Hadi mapumziko timu zote zilikwenda mapumziko , Young Africans 0 - Arminia Bielefeld.

Kipindi cha pili Arminia Bielefeld iliamua kubadilisha kikosi chake chote cha wachezaji kwa lengo la kuingiza nguvu mpya ili waweze kuikabili kasi ya wachezaji wa Yanga ambao walionekana kuwa imara na bora zaidi.

Dakika ya 55 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Said Bahanuzi na David Luhende na nafasi zao kuchukuliwa na Jerson Tegete na Saimon Msuva.

Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 60 ya mchezo, akiunganisha pasi safi aliypewa na Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa Arminia Bielefeld na kumpa pasi Tegete ambaye aliukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao la kwanza.

Kuona hivyo wajerumani walikuja juu kusaka bao la kusawazisha, lakini bado ukuta wa Yanga uliendelea kuonekana kuwa makini lakini makosa ya mshika kibendera yaliipelekea Armini Bielefeld kupata bao la kusawazsiha dakika ya 81 kupitia kwa Eric Agyemang amabaye alikua ameotea.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Young Africans 1 - 1 Armini Bielefeld.

 
Na Tovuti ya Yanga    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: J_G    Sunday, January 06, 2013 03:38:28   
 
iyo timu ya wajeru wajelu-UBUGUVU ni ya daraja la ngapi?

si mbaya kucheza na jamii za wengine, sio kulla siqu afrika 2!

 
 
Mtoa Maoni: Abdulaziz    Sunday, January 06, 2013 12:13:18   
 
Africa kwa kweli kuna wachezaji wazuri unaweza kulinganisha na nchi za Europe ukiwacha nchi za Asia, kwa mfano Tanzania lazima wabadilike wazi binafsi club zao lazima twende na wakati, katika dunia ya leo mpira ni pesa na iwepo good administtration ndio club na nchi jina lake litapanda sio kila sisi sauti zetu zinasikika East Africa tu hatutowi wachezaji nje wala hatuwachi kupenda simba na yanga wakati ni nchi inao watu milioni 45 na mikoa zaidi 22 tubadilike tufute mifano ya wenzetu.
 
 
Mtoa Maoni: Mang    Monday, January 07, 2013 11:05:27   
 
UBUGUVU Yanga umewaona? Usilete chuki binafsi! mzungu ni mzungu, ukiona hadi anapata bao la offside ujue hiyo Yanga si ya kawaida ndio maana inastahiki kuongoza ligi ya TZ bila mpinzani! Simba ya Adeni Rage waache wachapane makonde msimbazi!!! hadi kieleweke!


 
 
Mtoa Maoni: Magore Magabo    Tuesday, January 08, 2013 06:09:15   
 
Mange shika adabu zako di merdo weee
 
 
Mtoa Maoni: pengo    Saturday, January 19, 2013 07:40:38   
 
hiyo timu ya ujerman ni ya daraja la 4 kwahiyo sio ajabu na ucheza na timu ya daraja la 4 na kujisifu mbona afrca cup wafanyi chochote tanzania mpri bado sana
 
 
       Jumla kuna maoni (9), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za michezo
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> MANJI atangaza kuachia ngazi Yanga
> Yanga na Simba Hakuna Mbabe 3-3
> LIVE VIDEO - TANZANIA - IVORY COAST High Quality
> Taifa Stars Yafa Kiume Morocco, Yalala 2-1
> Mechi ya Simba na Yanga Yaingiza Milioni 500
> VIDEO - Nyota wa Liverpool, Suarez Amng'ata Mkono Beki wa Chelsea
> Drogba Aitosa Chelsea na Kujiunga na Galatasaray
> VIDEO - Staili Mpya ya Kushangilia Goli Kwa Makalio
> Yanga Yawabamiza Wasauzi 3-2
> Yanga Yatoka Droo na Wajerumani
> Zanzibar Heroes ya futwa kwa utovu wa nidhamu
> KILIMANJARO STARS YATOLEWA CHALLENGE
> VIDEO - Jamaa Anayeipenda Yanga Kuliko Kitu Chochote
> Simba na Yanga Hakuna Mbabe, Zatoka Sare 1-1
> Kuiona Mechi ya Simba na Yanga ni 5000/=
> Simba Yashushiwa Kichapo cha Mabao 3-1 na Azam, Yatolewa Kombe la Kagame
> Yanga Yatinga Nusu Fainali Kombe la Kagame, Yaibanjua Mafunzo
> Simba Nayo Yabugizwa 2-0 na URA ya Uganda
> Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0
> Drogba Atimukia China, Kulipwa Kitita cha Nguvu
> Maximo Arudi Nchini Toka Brazili Kuifundisha Yanga
> Beki wa Simba Atimukia Yanga Kwa Milioni 30
> Chelsea Mabingwa Wapya wa Ulaya, Yaizamisha Bayern Munich
> Manchester City Yatawazwa Mabingwa wa Uingereza

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD