Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Mlinzi wa Obama Ajiua

NewsImages/6662206.jpg
Monday, November 05, 2012 2:37 AM
Mlinzi wa Rais wa Marekani, Barack Obama amejiua mwenyewe baada ya kufunguliwa kesi ya kulala na mpenzi wake hotelini wakati akiwa kazini nje ya nchi.
Mlinzi wa rais wa Marekani, Barack Obama amejiua mwenyewe wakati uchunguzi ukiendelea kutokana na kitendo chake cha kutotoa taarifa kuwa alilala na mpenzi wake ambaye si raia wa Marekani hotelini na hivyo kuvunja sheria za shirika la ujasusi la Marekani.

Mlinzi huyo wa Obama aliyetajwa kwa jina la Rafael Prieto mwenye umri wa miaka 47, alikuwa akichunguzwa kwa kushindwa kutoa taarifa kuwa alilala hotelini na mwanamke ambaye si raia wa Marekani wakati alipokuwa nchini Colombia kuandaa mazingira kabla ya ziara ya rais Obama nchini humo mwezi aprili mwaka huu.

Shirika la ujasusi la Marekani linawafanyia uchunguzi baadhi ya maafisa wake kufuatia skendo la maafisa wake kukodisha makahaba wakati walipokuwa kwenye ziara ya kikazi nchini Colombia mwanzoni mwa mwaka huu.

Kwa kawaida maafisa hao hutakiwa kutoa taarifa za mahusiano yao na wanawake ambao si raia wa Marekani ili kuhakikisha kuwa wanawake hao hawana madhara kwa usalama wa taifa la Marekani.

Rafael Prieto, alikuwa kwenye ndoa na mkewe raia wa Marekani aliyezaa naye watoto lakini alikuwa pia na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na mwanamke raia wa Mexico.

Uhusiano wake uligundulika baada ya afisa mwenzake aliyekuwa naye kwenye mji wa Cartagena nchini Colombia kuripoti mahusiano hayo kuwa yanavunja sheria za shirika la ujasusi la Marekani.

Shirika la ujasusi la Marekani, limeelezea kusikitishwa kwake na kifo cha afisa wake Rafael ambaye alikutwa amefariki ndani ya gari lake baada ya kujipulizia gesi ya sumu. Rafael amelitumikia shirika la ujasusi la Marekani kwa miaka 20.

Kufuatia skendo hilo la makahaba nchini Kolombia, shirika la ujasusi la Marekani limeongeza masharti magumu kwa maafisa wake kwa kuwapiga marufuku kunywa pombe na kuingiza raia wa kigeni hotelini wakati wakiwa kwenye safari za kikazi nje ya Marekani.

 
Nifahamishe.com    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: HUM HUM    Monday, November 05, 2012 03:10:14   
 
Nenda zako jahanam iko uko itakupokeya uzuri
 
 
Mtoa Maoni: JUDEX    Monday, November 05, 2012 06:23:09   
 
Enhee wenyewe wanaanza kujiua, hizo ni adhabu za Allah S.W zinaanza kuwapata!! na bado hapo watajiondoa hao mpaka watakwisha, nataka hizo sheria zizidi kuwa kali yani hata ukikohoa nje ya marekani ushtakiwe ndo itakuwa shega!!! lakini cha kusikitisha kwa nini kama ameamua kujiua asiondoke na wenzie kama watatu hivi ili akapunguza mzigo kwa Waislamu???
 
 
Mtoa Maoni: alobadilijina    Monday, November 05, 2012 20:53:16   
 
Licha ya kulala na mpenzi wake hotelini hata angelala naye juu ya mti pia ingekuwa ni hatia. kujiua mwenyewe pia ni hatia ila labda anjaribu kusitiri uchaguzi wa bosi wake.
 
 
Mtoa Maoni: SIKAFUNJE    Tuesday, November 06, 2012 10:00:16   
 
dini ya ALLAH inahamasisha watu wauwawe duuh hivyo ndo mnavyofundishwa hiyo n dini ya shetwaaanii bin iblisii,NAOMBA NIAMBIWE KAMA KUNA SHEHE MWENYE ELIMU HATA YA FORM 4 TZ.
 
 
Mtoa Maoni: Shelaina    Tuesday, November 06, 2012 10:10:04   
 
Mlinzi wa Barack Obama kujiua inahusianaje na kupunguza mzigo kwa waislamU???? Inaelekea wewe hata dini yenyewe huijui vizuri? Usizalilishe uislmu?

 
 
       Jumla kuna maoni (19), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za dunia
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Mbakaji Azimia Baada ya Kuambiwa Mwanamke Aliyembaka ni Muathirika
> Wanawake Waislamu Waowana Ndoa Ya Jinsia Moja.
> Wanawake Waislamu Waowana Ndoa Ya Jinsia Moja.
> Wazuiwa Chuo Kwa Nguo Waliyovaa
> 'Waislamu ni Waovu Waueni Wote'
> Jela Au Faini Kwa Kucheka Kwa Sauti Kubwa.
> Kijasho Chembamba Chamtoka Waziri Mkuu
> Wakulima Wapewa Mikopo Kupunguza Ujane
> Binti Wa Miaka 15 Atoroka kwa Mume kisa Mzee
> Gangnam Style Ina Asili ya Afrika
> Apiga picha za uchi kupinga katiba ya kiislam
> Mwanamke mnene washindwa kumpandisha kwenye Gari la wagonjwa
> Wafufua maiti na kuitembeza mitaani
> Mbunge wa bunge la ulaya ashitakiwa kwa kuwatukana waislamu
> Ajiua kwa Matamanio ya ngono ya mara kwa mara
> Wanawake waitisha mgomo wa ngono Italy
> Mwanafunzi azuiwa kwenda chooni afariki darasani
> Cobra ailazimisha ndege kutua Misri
> Obama Achaguliwa Tena Kuwa Rais wa Marekani
> Wamarekani Kumchagua Rais Wao Leo
> Mlinzi wa Obama Ajiua
> Aliyetangazwa Amekufa, Ahudhuria Mazishi Yake Mwenyewe
> VIDEO - Ukisikia Pombe si Maji....

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD