Kompyuta na Monitors, Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Aliyetangazwa Amekufa, Ahudhuria Mazishi Yake Mwenyewe

NewsImages/6652566.jpg
Gilberto Araujo
Thursday, October 25, 2012 1:55 AM
Mwanaume aliyehudhuria mazishi yake alisababisha kizaa zaa nchini Brazili na kupelekea baadhi ya ndugu zake kuzimia na wengine kumkimbia kwa hofu.
Muosha magari katika mji wa Alagoinhas nchini Brazili, Gilberto Araujo mwenye umri wa miaka 41, alisababisha mtafaruku mkubwa pale alipohudhuria mazishi ambayo yalikuwa kwaajili yake.

Mtafaruku huo ulitokea pale kaka yake Gilberto, Jose Marcos, alipotakiwa na polisi aende hospitali kuutambua mwili wa ndugu yake ambaye alitajwa kuwa ameuliwa kwa kupigwa risasi.

Jose aliutambua mwili huo na kusema ni kweli wa mdogo wake Gilberto na kuruhusiwa kuuchukua mwili huo kwaajili ya taratibu za mazishi.

Wakati taratibu za mazishi zikielekea ukingoni, Gilberto aliwahi nyumbani kwao baada ya kukutana na mtu aliyempa taarifa kuwa nyumbani kwao wanajua amefariki dunia na hivyo mazishi yanafanyika.

Baadhi ya watu kwenye mazishi walizimia na wengine walikimbia baada ya kumshuhudia aliyetajwa kuwa ni marehemu ametokea mbele yao akiwafuata.

Shemeji yake Gilberto akilielezea tukio hilo alisema kuwa mtafaruku ulianza pale habari zilipoanza kusambaa mtaani kuwa muosha magari ameuliwa kwa kupigwa risasi.

"Polisi walimuita mume wangu na kumuambia kuwa kaka yake ameuliwa kwa kupigwa risasi na mwili wake uko monchwari hivyo alitakiwa aende kuutambua", alisema mke huyo wa kaka yake.

Iligundulika baadae kuwa mtu halisi aliyeuliwa katika tukio hilo alikuwa ni Genivaldo Santos Gama.

"Kwa jinsi walivyokuwa wakifanana na wote walikuwa waosha magari ndio maana watu walidhani ni Gilberto ameuliwa", alisema mama yake Gilberto.

"Nina furaha sana, kitu gani ambacho mama anaweza kusema baada ya kuambiwa kuwa mtoto wake amefariki halafu baadae anamuona yuko hai", alisema mama yake Gilberto, bi Marina Santana.

 
Nifahamishe.com    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Faraja McHarris    Thursday, October 25, 2012 06:54:20   
 
Hajafa Gilbrerto yuko hai jamanie. Cha news kichwa.
 
 
Mtoa Maoni: kadwame    Thursday, October 25, 2012 18:38:47   
 
huo ndio mwisho wa dunia!!!
 
 
Mtoa Maoni: alobadilijina    Friday, October 26, 2012 20:45:39   
 
Hapo kuna fundisho.
Mtu anapokufa akililiwa haimaanishi kuwa anapendwa labda watu wanalia kwakua kwanini alichelewa kuondoka duniani. Maiti akifufuka hata siku moja watu hawatafurahi bali watamkimbia, watamnyanyampaa na mengine kama hayo. ama kweli dunia ni duara ukifikiri sana utahara!

 
 
Mtoa Maoni: MR. GROOM FOONG    Friday, November 02, 2012 08:57:50   
 
Jamani NIFAHAMISHE/COM muwe basi mnaletea wasomaji wa habari habari ambazo siko serious tafadhali. Basi tu!
 
 
Mtoa Maoni: j . j mpingo    Saturday, November 03, 2012 14:29:35   
 
mnapo weka habaari muweka habari za kweli nasio kudanganya watu hii sio jambo zuri ila tu nakuombeeni mue watu wakweli tu na munatoa wapi hizi habari za uongo .....
 
 
       Jumla kuna maoni (9), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za dunia
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Mbakaji Azimia Baada ya Kuambiwa Mwanamke Aliyembaka ni Muathirika
> Wanawake Waislamu Waowana Ndoa Ya Jinsia Moja.
> Wanawake Waislamu Waowana Ndoa Ya Jinsia Moja.
> Wazuiwa Chuo Kwa Nguo Waliyovaa
> 'Waislamu ni Waovu Waueni Wote'
> Jela Au Faini Kwa Kucheka Kwa Sauti Kubwa.
> Kijasho Chembamba Chamtoka Waziri Mkuu
> Wakulima Wapewa Mikopo Kupunguza Ujane
> Binti Wa Miaka 15 Atoroka kwa Mume kisa Mzee
> Gangnam Style Ina Asili ya Afrika
> Apiga picha za uchi kupinga katiba ya kiislam
> Mwanamke mnene washindwa kumpandisha kwenye Gari la wagonjwa
> Wafufua maiti na kuitembeza mitaani
> Mbunge wa bunge la ulaya ashitakiwa kwa kuwatukana waislamu
> Ajiua kwa Matamanio ya ngono ya mara kwa mara
> Wanawake waitisha mgomo wa ngono Italy
> Mwanafunzi azuiwa kwenda chooni afariki darasani
> Cobra ailazimisha ndege kutua Misri
> Obama Achaguliwa Tena Kuwa Rais wa Marekani
> Wamarekani Kumchagua Rais Wao Leo
> Mlinzi wa Obama Ajiua
> Aliyetangazwa Amekufa, Ahudhuria Mazishi Yake Mwenyewe
> VIDEO - Ukisikia Pombe si Maji....

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD