Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Aliyetengeneza Filamu ya Kumkashifu Mtume Ajificha na Familia Yake

NewsImages/6602438.jpg
Nakoula Basseley Nakoula a.k.a. Sam Bacile akiwa na mmoja wa wasanii wake Anna Gurji.
Tuesday, September 18, 2012 4:56 AM
Wakati maandamano ya kuipinga filamu ya kumashifu mtume (s.a.w) yakizidi kupamba moto katika nchi mbalimbali duniani, mtengenezaji wa filamu hiyo pamoja na familia yake ameingia mafichoni kunusuru maisha yake.
Nakoula Basseley Nakoula, ambaye ni tapeli mwenye kujipa majina mbalimbali mwenye umri wa miaka 55 ambaye alihukumiwa kwenda jela miezi 21 nchini Marekani kwa makosa mbalimbali ya utapeli mwaka 2010, ameingia mafichoni pamoja na familia yake baada ya maandamano ya kuipinga filamu aliyoitengenza kuzidi kupamba moto.

Nakoula alijiita jina la Sam Bacile wakati wa utengenezaji wa filamu ya "The Innocence of Muslims" ambayo trela lake liliwekwa kwenye YouTube na video zake zikimuonyesha mtu aliyeigiza kama mtume Muhammad, akifanya mapenzi, akibaka na akiamuru kuuliwa kwa watu.

Nakoula aka Sam Bacile hajaonekana tangu jumamosi baada ya polisi kwenda nyumbani kwake kumhoji na familia yake ya watu wanne nayo jana jumatatu iliihama nyumba yao na kwenda mafichoni kujiunga na Nakoula.

Polisi wa Los Angeles waliwasili majira ya alfajiri kabla jua halijachomoza na walimchukua mke wa Nakoula na watoto wake watatu na kuwasindikiza kwenye maficho ya siri ambako Nakoula amejificha.

Familia yake ilizificha sura zao wakati wakisindikwa na polisi toka kwenye nyumba yao iliyozungukwa na waandishi wa habari wengi waliokuwa wakikesha mbele ya nyumba hiyo.

"Waliona kuwa watakuwa salama sehemu ambayo wataweza kutoka nje na kuishi maisha ya kawaida", alisema msemaji wa polisi na kuongeza "Tulichokifanya sisi ni kuwachukua na kuwapeleka sehemu ambayo Nakoula amejificha".

Nakoula aliwahi kutupwa jela miaka miwili iliyopita kutokana na utapeli wa cheki za watu kwa kutumia majina mbalimbali feki. Alikaa jela mwaka mmoja kabla ya kutolewa kwa masharti kumalizia kifungo chake uraiani.

Vyombo vya habari vya Marekani vimekuwa vikiripoti kuwa kujihusisha kwake kutengeneza filamu hiyo kunaweza kukawa kumevunja masharti aliyopewa hivyo anaweza kurudishwa jela.

 
Nifahamishe.com    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: mvumilivu    Tuesday, September 18, 2012 05:36:01   
 
hilo si suluhisho, Obama kama kiongozi wa nchi angelieka fatwa, mtu yeyote atakae fanya jambo ambalo linaweza kugharimu maisha ya watu, basi hukumu yake iwe kifo, ili kupunguza matatizo duniani, ila kuwaficha ni kuwapa hifadhi kama mlivompa Sulayman Rushid, hivyo sifikirii kua hilo ni suluhisho bali ni uharibifu wa dunia, Marekani ni kama kiooo ch ulimwengu, nyinyi kapigwa picha za uchi mke wa mjukuu wa mfalme tu magazeti na T.v zote zinapiga kelel, na karibu magazeti yatashtakiwa.
 
 
Mtoa Maoni: Dada    Tuesday, September 18, 2012 07:17:54   
 
Imeonyeshwa kwenye TV za nchi za nje kuwa cnn wamemkamata na sura yake kufunikwa na kitambaa na kavaa kofia, leo vipi Nifahamishe mnasema yupo mafichoni? haiwezekani
Mwache aipate ajue iko siku kifo chake kitakuwa kibaya tu kama zinavyomwagika damu za watu hivi sasa. malipo duniani akhera huenda husabu. kila anaemtendea mwenzake ubaya>>>>>> AJUE iko siku yake

 
 
Mtoa Maoni: ubuguvu    Tuesday, September 18, 2012 07:36:49   
 
marekani ilisema wao hawahusiki na hiyo film na wote walioshiriki watachukuliwa hatua sasa hiyo ndo hatua kuwapeleka mafichoni, hapa cha msingi ni kuongeza kuua balozi mwengine wa marekani popote pale
 
 
Mtoa Maoni: Juma    Tuesday, September 18, 2012 09:17:14   
 
Wewe Dada hapa ndio Nifahamishe.com unapata habari motomoto sasa nenda tena CNN utapata habari kama hii usiwe mvivu wa kufikiri kuwa mambo yanabadilika kila sekunde
 
 
Mtoa Maoni: ASHRAF YASSER    Tuesday, September 18, 2012 14:01:30   
 
Dunia inaelekea mwisho na hizi ndio dalili zenyewe yatupasa tujue nini cha kufanya kuelekea siku ya hukumu kwani kiama ndo tayari
 
 
       Jumla kuna maoni (34), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za dunia
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Mbakaji Azimia Baada ya Kuambiwa Mwanamke Aliyembaka ni Muathirika
> Wanawake Waislamu Waowana Ndoa Ya Jinsia Moja.
> Wanawake Waislamu Waowana Ndoa Ya Jinsia Moja.
> Wazuiwa Chuo Kwa Nguo Waliyovaa
> 'Waislamu ni Waovu Waueni Wote'
> Jela Au Faini Kwa Kucheka Kwa Sauti Kubwa.
> Kijasho Chembamba Chamtoka Waziri Mkuu
> Wakulima Wapewa Mikopo Kupunguza Ujane
> Binti Wa Miaka 15 Atoroka kwa Mume kisa Mzee
> Gangnam Style Ina Asili ya Afrika
> Apiga picha za uchi kupinga katiba ya kiislam
> Mwanamke mnene washindwa kumpandisha kwenye Gari la wagonjwa
> Wafufua maiti na kuitembeza mitaani
> Mbunge wa bunge la ulaya ashitakiwa kwa kuwatukana waislamu
> Ajiua kwa Matamanio ya ngono ya mara kwa mara
> Wanawake waitisha mgomo wa ngono Italy
> Mwanafunzi azuiwa kwenda chooni afariki darasani
> Cobra ailazimisha ndege kutua Misri
> Obama Achaguliwa Tena Kuwa Rais wa Marekani
> Wamarekani Kumchagua Rais Wao Leo
> Mlinzi wa Obama Ajiua
> Aliyetangazwa Amekufa, Ahudhuria Mazishi Yake Mwenyewe
> VIDEO - Ukisikia Pombe si Maji....

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD