Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Aliyedai Asizikwe Atafufuka Baada ya Siku Mbili Asababisha Balaa

NewsImages/6601474.jpg
Tuesday, September 18, 2012 4:25 AM
Mwanaume mmoja wa nchini Afrika Kusini ambaye alidai enzi za uhai wake kuwa atakapofariki asizikwe kwakuwa atafufuka baada ya siku mbili ameshindwa kufufuka baada ya kifo chake na maiti yake imekuwa kero kwa watu kutokana na harufu kali inayotoa.
Mwanaume huyo aliyekuwa mkazi wa Tsolo, Eastern Cape nchini Afrika Kusini aliwaagiza ndugu zake wakati wa uhai wake kuwa atakapofariki basi mwili wake usipelekwe monchwari kwakuwa atafufuka baada ya siku mbili.

Mwanaume huyo alifariki jumanne ya wiki iliyopita na ndugu zake walifuata maagizo yake kwa kuuweka mwili wake nyumbani kwake wakimsubiria arudi toka kuzimu akiwa hai tena.

Familia yake iliendelea kuutunza mwili wake huku wanajumuiya wa kanisa lake wakija kumuombea dua.

Baada ya siku mbili kupita ambazo alidai angefufuka maiti yake ilianza kuharibika na kutoa harufu kali iliyoanza kuwa kero kwa majirani.

Msemaji wa eneo hilo aliyetambulishwa kama Sizwe Kupelo aliwaambia waandishi wa habari kuwa majirani wameanza kulalamika harufu kali inayotoka kwenye nyumba yake.

"Limekuwa tatizo la kiafya sasa, watu wanaohofia kupata maambukizi", alisema Kupelo.

Timu ya maafisa wa afya na mapolisi walitarajiwa kuitembelea familia hiyo na kuishawishi iachane na mawazo ya kusubiria kufufuka kwa ndugu yao na hatimaye wauzike mwili wake kama inavyotakikana.

 
Nifahamishe.com    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: ubuguvu    Tuesday, September 18, 2012 08:07:50   
 
Afrika kusini wawashukuru sana hao wazungu maana kukosa wazungu sijui wengekua katika hali gani, hawa watu wana imani potofu sasa imani za kishirikina ndo zimejaa yule babu la Loliondo angekua kwao angekubiliana kwa mwezi mmoja tu
 
 
Mtoa Maoni: Pan Africanist    Tuesday, September 18, 2012 11:15:15   
 
Wewe unayesema 'wawashukuru wazungu' unamatatizo. baadala utoe comment nyingine unaongelea wazungu.Kwani wazngu wana tofaut gani na wewe.Sasa kwa taarifa zako, wazungu ndo washirikina namba moja.Uliza mtu yeyote ambaye amekaa kwao vya kutosha.
 
 
Mtoa Maoni: ubuguvu    Tuesday, September 18, 2012 18:54:16   
 
ww usijitie uzalendo wa kijampaka ukawa unapinga ukweli, uchawi wa kizungu unatofautiana na wakwetu wazungu hawana ushirikina ule wa kuauwa maalbino ili wawe matajiri, unajua afrika ya kusini imetumia shiling ngapi katika kombe la dunia ili washinde na mwisho wametoka raundi ya kwanza? Ww unakaa na wazungu walichoka kama ww ndo maana wanakua na fikra kama zako za kwa babu wa Loliondo
 
 
Mtoa Maoni: Mimi     Tuesday, September 18, 2012 19:56:28   
 
huyo ana mawazo kama ya mwanza Boy kudadeki akifa hata kaburini mwanza boy hatopelekwa! kwanza mwanza boy akifa kama kafa mbwa tu hana faida yeyote hapa duniani,wewe mwanzaBoy wa kuwakashifu waislam wewe! kama unaunga mkono ushoga si kivyako nenda na wewe basi ukaolewe huko uingereza usituletee za kuleta hapa! ***********mbavu zako! salam ziwafikie wale wote mashoga wa mwanza boy!
 
 
Mtoa Maoni: SEEKER-OF-TRUTH    Tuesday, September 18, 2012 20:04:26   
 
Ukweli ni kwamba hata wazungu kuna washirikina tena wabaya zaidi, ambao wanaabudu Sheitani. Na Freemasons wala hawajali kujulikana na hivi sasa wanaeneza ibada hio ya kishirikina. Na uchawi ulaya na Marekani ni fashion.
 
 
       Jumla kuna maoni (16), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za dunia
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Mbakaji Azimia Baada ya Kuambiwa Mwanamke Aliyembaka ni Muathirika
> Wanawake Waislamu Waowana Ndoa Ya Jinsia Moja.
> Wanawake Waislamu Waowana Ndoa Ya Jinsia Moja.
> Wazuiwa Chuo Kwa Nguo Waliyovaa
> 'Waislamu ni Waovu Waueni Wote'
> Jela Au Faini Kwa Kucheka Kwa Sauti Kubwa.
> Kijasho Chembamba Chamtoka Waziri Mkuu
> Wakulima Wapewa Mikopo Kupunguza Ujane
> Binti Wa Miaka 15 Atoroka kwa Mume kisa Mzee
> Gangnam Style Ina Asili ya Afrika
> Apiga picha za uchi kupinga katiba ya kiislam
> Mwanamke mnene washindwa kumpandisha kwenye Gari la wagonjwa
> Wafufua maiti na kuitembeza mitaani
> Mbunge wa bunge la ulaya ashitakiwa kwa kuwatukana waislamu
> Ajiua kwa Matamanio ya ngono ya mara kwa mara
> Wanawake waitisha mgomo wa ngono Italy
> Mwanafunzi azuiwa kwenda chooni afariki darasani
> Cobra ailazimisha ndege kutua Misri
> Obama Achaguliwa Tena Kuwa Rais wa Marekani
> Wamarekani Kumchagua Rais Wao Leo
> Mlinzi wa Obama Ajiua
> Aliyetangazwa Amekufa, Ahudhuria Mazishi Yake Mwenyewe
> VIDEO - Ukisikia Pombe si Maji....

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD