Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0

NewsImages/6499290.jpg
Hispania wamekuwa mabingwa wa mataifa ya ulaya kwa mara nyingine tena
Monday, July 02, 2012 2:03 AM
Hispania imekuwa nchi ya kwanza kutwaa makombe matatu makubwa duniani kwa mpigo baada kuibugiza Italia mabao 4-0 na kulitwaa tena kombe la mataifa ya ulaya.
Mabingwa wa ulaya na mabingwa wa dunia, Hispania au maarufu kwa jina la "La Roja" wamejiongezea taji jingine kwa kutwaa tena kombe la euro 2012.

Katika mechi hiyo ya fainali iliyochezwa nchini Ukraine, Hispania waliwafundisha soka Italia kwa pasi zao fupi fupi wakitawala sehemu kubwa ya mechi hiyo.

Licha ya vyombo vya habari kumbeza kocha wa Hispania kwa staili yake ya kuchezesha viungo sita bila ya mshambuliaji, staili yake hiyo ilisaidia kumzima nyota wa Italia, Andrea Pirlo na kumfanya Mario Balotelli kuwa msindikizaji uwanjani.

Magoli mawili ya Hispania kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa David Silva kwenye dakika ya 14 na beki Jordi Alba kwenye dakika ya 41 yalisaidia kuivunja nguvu Italia kabla ya Fernando Torres na Juan Mata kulipigilia jeneza la Italia misumari ya mwisho kwenye dakika za mwisho za kipindi cha pili.

Kwa ushindi huu Hispania imefanikiwa kuvunja rekodi nyingi za mashindano ya soka ya kimataifa.

Hispania imekuwa nchi ya kwanza kuweza kufanikiwa kuutetea ubingwa wake wa kombe la mataifa ya ulaya. Hispania pia imeweka historia ya kutwaa kombe la mataifa ya ulaya kwa idadi kubwa ya magoli kuliko mechi zote za fainali za Euro zilizowahi kuchezwa.

Hispania imekuwa nchi ya kwanza kutwaa makombe matatu makubwa kwa mfululizo baada ya kutwaa Euro 2008 na kombe la dunia 2010.

Fernando Torres amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli katika mechi mbili tofauti za fainali za kombe la mataifa ya ulaya.

 
Nifahamishe.com    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: (Nundaa)    Monday, July 02, 2012 08:06:42   
 
Wadau naomba mnisaidie, mimi navyofahamu mfungaji magoli mengi ni MARIO BALOTELI anayomagoli 4 na vipi ataambiwa amefunga magoli 3?
Italy Vs Ireland kafunga goli moja.
Italy Vs England kafunga goli moja kwa penati.
Italy Vs Germany kafunga magoli mawili.
Jee itakuwaje Fernando Tores achaguliwe mfungaji mwenye magoli mengi?
Nifahamishe.com na Wadau nisaidieni kuhusu ili swali langu.

 
 
Mtoa Maoni: zungut    Monday, July 02, 2012 13:00:13   
 
Goli la penalti halihisabiki kwani kafunga baada ya dakika 120.
 
 
Mtoa Maoni: (Nundaa)    Monday, July 02, 2012 14:18:51   
 
zungut: Kiswahili kwako nafikiri ni kigumu au hujafahamu namna ya kunifahamisha? Unasema goli la penalti halihesabiki na hapo hapo unakubali kuwa kafunga goli la penalti baada ya dakika 120, jee mbona limehesabika kuitoa England?
Au sheria za mpira wa miguu zimebadilika?
Hatubishani ila tunafahamishana na napenda kujua ili nifaidike na wenzetu wengine wafaidike kujifundisha ni muhimu na kuuliza si ujinga.
Asante sana mdau zungut.

 
 
Mtoa Maoni: Misha    Monday, July 02, 2012 15:45:34   
 
Nundaa ni hivi nikufahamishe
Goli la penalti mbali ya dakika dakika 90 za mchezo halihesabiki katika rekodi za idadi ya magoli linahesabika katika uamuzi wa mechi tu kujua nani kashinda tu

 
 
Mtoa Maoni: (Nundaa)    Tuesday, July 03, 2012 07:22:35   
 
Misha & zungut: Asanteni sana kwa kunifahamisha, kweli kuuliza sio ujinga ila ni kujifundusha, hivi sasa ndio nimefahamu Mwenyezi Mungu akuzidishieni kheri na baraka, amin.
 
 
       Jumla kuna maoni (9), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za michezo
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> MANJI atangaza kuachia ngazi Yanga
> Yanga na Simba Hakuna Mbabe 3-3
> LIVE VIDEO - TANZANIA - IVORY COAST High Quality
> Taifa Stars Yafa Kiume Morocco, Yalala 2-1
> Mechi ya Simba na Yanga Yaingiza Milioni 500
> VIDEO - Nyota wa Liverpool, Suarez Amng'ata Mkono Beki wa Chelsea
> Drogba Aitosa Chelsea na Kujiunga na Galatasaray
> VIDEO - Staili Mpya ya Kushangilia Goli Kwa Makalio
> Yanga Yawabamiza Wasauzi 3-2
> Yanga Yatoka Droo na Wajerumani
> Zanzibar Heroes ya futwa kwa utovu wa nidhamu
> KILIMANJARO STARS YATOLEWA CHALLENGE
> VIDEO - Jamaa Anayeipenda Yanga Kuliko Kitu Chochote
> Simba na Yanga Hakuna Mbabe, Zatoka Sare 1-1
> Kuiona Mechi ya Simba na Yanga ni 5000/=
> Simba Yashushiwa Kichapo cha Mabao 3-1 na Azam, Yatolewa Kombe la Kagame
> Yanga Yatinga Nusu Fainali Kombe la Kagame, Yaibanjua Mafunzo
> Simba Nayo Yabugizwa 2-0 na URA ya Uganda
> Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0
> Drogba Atimukia China, Kulipwa Kitita cha Nguvu
> Maximo Arudi Nchini Toka Brazili Kuifundisha Yanga
> Beki wa Simba Atimukia Yanga Kwa Milioni 30
> Chelsea Mabingwa Wapya wa Ulaya, Yaizamisha Bayern Munich
> Manchester City Yatawazwa Mabingwa wa Uingereza

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD