Kompyuta na Monitors, Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Maximo Arudi Nchini Toka Brazili Kuifundisha Yanga

NewsImages/6456874.jpg
Marcio Maximo anatua nchini kuinoa Yanga
Friday, June 08, 2012 7:58 PM
Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya soka, Taifa Stars, Marcio Maximo, anatarajiwa kutua nchini wiki ijayo kwa ajili ya kuingia mkataba wa kuifundisha Yanga.
Marcio Maximo, anatarajiwa kutua nchini wiki ijayo kuchukua mikoba ya kocha anayemaliza muda wake katika klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imeelezwa.

Kocha huyo anatarajia kuwasili nchini akiwa na Kocha msaidizi wa viungo, huku akiwa ameongozana na mkewe.

Maximo anatarajiwa kuanza kuifua Yanga kukiandaa kikosi cha timu hiyo kinachotarajia kushiriki michuano ya Kombe la Kagame.

Aidha imeelezwa kuwa mara tu baada ya kupokea maombi ya kukinoa kikosi hicho Maximo hakuwa na pingamizi lolote bali alikubaliana na maombi hayo moja kwa moja huku akitoa mapendekezo ya kuwasajili wachezaji awatakao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Katika mapendekezo hayo ya wachezaji aliowahitaji Maximo ni pamoja na Beki wa Simba, ambaye hadi sasa bado anazua gumzo na mtafaruku mkubwa baina ya klabu hizo mbili za watani wa jadi Simba na Yanga, Kelvin Yondani, pamoja na kipa Ali Mustapha 'Bartez'.

Chanzo cha habari hizi kutoka klabu hiyo ya Jangwani kimetonya kuwa baadhi ya wachezaji wengine waliokwishamwaga wino katika Klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ni pamoja na beki wa timu ya Kagera Sugar, David Luhende, mchezaji anayecheza soka la kulipwa na timu ya DC Motema Pembe, Mussa Hassan Mgosi, Owen Kasule kutoka Klabu ya Hoang Anh Gia Lai ya Vientnam, Middie Kagere kutoka timu ya Polisi Rwanda na mchezaji wa Tanzania anayecheza Soka la kulipwa nchini Canada Nizar Khalfan pamoja na Said Bahanuzi na Juma Abdul kutoka timu ya Mtibwa Sugar.

Aidha imeelezwa kuwa 'Bartez' tayari amekwisha saini mkataba na Yanga, huku Kipa namba tatu wa timu hiyo, Shaban Kado, akiachiwa kwa Mkopo kurejea katika kikosi cha timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.

 
Na Muhidini Sufiani    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: J_G aka    Friday, June 08, 2012 20:22:27   
 
Hivyo nani kasema km MXM ni kocha? Ama kweli mwendawazimu kupoa ni majaaliwa!!
Im out!!

JAMROCK sasa km umeamua kukenua mijino hii ndio hbr yenyewe!! si kwenye misiba!!!

 
 
Mtoa Maoni: J_G aka    Friday, June 08, 2012 20:23:30   
 
Oh nimekumbuka.. kaja KUMAlizia filamu zake alizoziacha kiporo kabla visa haijamalizika! KDDDK!
 
 
Mtoa Maoni: OSAMA MTOTO    Friday, June 08, 2012 21:09:29   
 
"Yanga xaxa kwisha" Kazi ipo YANGA wale waliokuja kusema Maxmo hafai walikuwa sio wa shabiki wa yanga? Ila ache ajekupunguza upinzani na simba mana si mnafahamu kuwa alikuwa akishinda sana ni droo so simba itakuwa ikuchuana na azamu
 
 
Mtoa Maoni: ubuguvu    Friday, June 08, 2012 22:54:07   
 
yanga kwa kupenda uwoza! Hawa yanga kwani kocha mzuri lazima awe mzungu ? Yule wa mwanzo hamjamlipz munaleta mzungu mwengine, jk yangu wenda kamleta yeye huyo
 
 
Mtoa Maoni: Mang    Saturday, June 09, 2012 03:11:43   
 
Tatizo la Yanga ni timu kuongozwa na viongozi wasio na moyo wa maendeleo ya timu! Kila kukicha migogoro na ahadi hewa! Kocha mzungu sio dawa. Dawa ni ari na moyo wa kuitumikia timu!
 
 
       Jumla kuna maoni (14), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za michezo
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> MANJI atangaza kuachia ngazi Yanga
> Yanga na Simba Hakuna Mbabe 3-3
> LIVE VIDEO - TANZANIA - IVORY COAST High Quality
> Taifa Stars Yafa Kiume Morocco, Yalala 2-1
> Mechi ya Simba na Yanga Yaingiza Milioni 500
> VIDEO - Nyota wa Liverpool, Suarez Amng'ata Mkono Beki wa Chelsea
> Drogba Aitosa Chelsea na Kujiunga na Galatasaray
> VIDEO - Staili Mpya ya Kushangilia Goli Kwa Makalio
> Yanga Yawabamiza Wasauzi 3-2
> Yanga Yatoka Droo na Wajerumani
> Zanzibar Heroes ya futwa kwa utovu wa nidhamu
> KILIMANJARO STARS YATOLEWA CHALLENGE
> VIDEO - Jamaa Anayeipenda Yanga Kuliko Kitu Chochote
> Simba na Yanga Hakuna Mbabe, Zatoka Sare 1-1
> Kuiona Mechi ya Simba na Yanga ni 5000/=
> Simba Yashushiwa Kichapo cha Mabao 3-1 na Azam, Yatolewa Kombe la Kagame
> Yanga Yatinga Nusu Fainali Kombe la Kagame, Yaibanjua Mafunzo
> Simba Nayo Yabugizwa 2-0 na URA ya Uganda
> Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0
> Drogba Atimukia China, Kulipwa Kitita cha Nguvu
> Maximo Arudi Nchini Toka Brazili Kuifundisha Yanga
> Beki wa Simba Atimukia Yanga Kwa Milioni 30
> Chelsea Mabingwa Wapya wa Ulaya, Yaizamisha Bayern Munich
> Manchester City Yatawazwa Mabingwa wa Uingereza

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD