Kompyuta na Monitors, Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Chelsea Mabingwa Wapya wa Ulaya, Yaizamisha Bayern Munich

NewsImages/6426990.jpg
Chelsea ndio mabingwa wapya wa kombe la mabingwa wa ulaya
Sunday, May 20, 2012 1:58 AM
Kwa mara ya kwanza Chelsea imefanikiwa kulitwaa kombe la mabingwa wa ulaya kwa kuwalaza Bayern Munich kwa penalti ndani ya uwanja wao wa Allianz Arena jijini Munich katika mechi kali ya kusisimua ambayo imemfanya Drogba aingie kwenye historia ya watu watakaokumbukwa sana Chelsea.
Didier Drogba kwa mara nyingine tena amekuwa shujaa wa Chelsea kwa kuipatia timu yake goli la kuwasazisha dakika mbili kabla ya mechi kuisha katika mechi kali ya kusisimua ya dhidi ya Bayern Munich katika fainali ya kombe la mabingwa wa ulaya.

Bayern ambao walitawala zaidi mechi hiyo na kupoteza nafasi nyingi sana za magoli walipata goli kwenye dakika ya 83 mfungaji wao akiwa ni Thomas Mueller.

Wakati Bayern wakijiandaa kushangilia kombe hilo la mabingwa wa ulaya, Drogba alienda hewani kwenye dakika ya 88 na kuunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Juan Mata. Kipa wa Bayern alibaki akizubaa huku mpira ukijaa kwenye nyavu zake.

Mechi ilienda kwenye dakika 30 za ziada ambapo Bayern walipata penalti ambayo Arjen Robben alishindwa kuizamisha kwenye nyavu za Chelsea na kuifanya mechi hiyo hadi dakika 30 za ziada zinaisha hakuna mbabe kati yao. Mechi hiyo ilibidi iamuliwe kwa matuta ya penalti.

Bayern walikosa penalti mbili kati ya tano huku Chelsea wakizifumania nyavu mara nne. Penalti ya tano iliyoipa ubingwa Chelsea ilipigwa na Drogba ambaye alimpeleka kushoto golikipa wa Bayern, Manuel Neuer huku mpira ukizama kwenye nyavu za kulia.

Hili limekuwa kombe la kwanza la mabingwa wa ulaya katika historia ya Chelsea tangu mwaka 2001 ilipoanza kampeni za kulisaka kombe hili. Kwa upande wao Bayern wamefanikiwa kulitwaa kombe hili mara nne.

Wapenzi wa Chelsea nchini Uingereza watapata fursa ya kuliona kombe hilo leo mchana wakati litakapotembezwa kwenye basi la wazi litakalobeba wachezaji na kombe hilo na kuzunguka mitaa ya jiji la London.

 
Na Mohamed Kindindi, Uingereza    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: mpenda amani    Sunday, May 20, 2012 02:04:24   
 
Mungu mkubwa
 
 
Mtoa Maoni: LAUO    Sunday, May 20, 2012 12:51:41   
 
hongera sana vijana wa darajani ,maana mmedhirihisha hta baca mlipaswa kuwafunga.isotshe walicheza bila main coach
 
 
Mtoa Maoni: mimi     Sunday, May 20, 2012 13:31:31   
 
hongera chelsea kwa juhudi hizo! ila mwanza boy mtoto mambo safi siku hizi upo wapi? mwanza boy chakula cha wakubwa kuna kazi ya kutoa mbwa ktk banda na kazi ya kupara miwa,nimesikia unaziweza saana kazi hizo!
 
 
Mtoa Maoni: J_G aka    Sunday, May 20, 2012 13:48:32   
 
UBUGUVU kikongwe chako cha kudhungu kimefurahia ushindi?

 
 
Mtoa Maoni: Osama mtoto    Sunday, May 20, 2012 14:28:26   
 
Kweli kipofu kaona njia
 
 
       Jumla kuna maoni (14), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za michezo
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> MANJI atangaza kuachia ngazi Yanga
> Yanga na Simba Hakuna Mbabe 3-3
> LIVE VIDEO - TANZANIA - IVORY COAST High Quality
> Taifa Stars Yafa Kiume Morocco, Yalala 2-1
> Mechi ya Simba na Yanga Yaingiza Milioni 500
> VIDEO - Nyota wa Liverpool, Suarez Amng'ata Mkono Beki wa Chelsea
> Drogba Aitosa Chelsea na Kujiunga na Galatasaray
> VIDEO - Staili Mpya ya Kushangilia Goli Kwa Makalio
> Yanga Yawabamiza Wasauzi 3-2
> Yanga Yatoka Droo na Wajerumani
> Zanzibar Heroes ya futwa kwa utovu wa nidhamu
> KILIMANJARO STARS YATOLEWA CHALLENGE
> VIDEO - Jamaa Anayeipenda Yanga Kuliko Kitu Chochote
> Simba na Yanga Hakuna Mbabe, Zatoka Sare 1-1
> Kuiona Mechi ya Simba na Yanga ni 5000/=
> Simba Yashushiwa Kichapo cha Mabao 3-1 na Azam, Yatolewa Kombe la Kagame
> Yanga Yatinga Nusu Fainali Kombe la Kagame, Yaibanjua Mafunzo
> Simba Nayo Yabugizwa 2-0 na URA ya Uganda
> Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0
> Drogba Atimukia China, Kulipwa Kitita cha Nguvu
> Maximo Arudi Nchini Toka Brazili Kuifundisha Yanga
> Beki wa Simba Atimukia Yanga Kwa Milioni 30
> Chelsea Mabingwa Wapya wa Ulaya, Yaizamisha Bayern Munich
> Manchester City Yatawazwa Mabingwa wa Uingereza

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD