Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Manchester City Yatawazwa Mabingwa wa Uingereza

NewsImages/6410602.jpg
Manchester City wamekuwa mabingwa wapya wa Uingereza
Monday, May 14, 2012 2:39 AM
Magoli mawili yaliyofungwa kwenye dakika mbili za mwisho yalitosha kuifanya Manchester City itawazwe kuwa mabingwa wa Uingereza msimu huu na kuwavua ubingwa watani wao wa jadi, Manchester United.
Manchester City wamekuwa mabingwa wa Uingereza baada ya miaka 44 kwa kuichapa timu ya QPR kwa magoli 3-2 katika mechi kali ya aina yake iliyohitimisha msimu huu wa ligi ya Uingereza.

Mara ya mwisho Manchester City kutwaa ubingwa ilikuwa ni mwaka 1968.

Magoli mawili yaliyofungwa ndani ya dakika mbili za mwisho za majeruhi, yaliifanya Manchester City ifanye kisichowekana kionekane rahisi na kuwavua ubingwa wapinzani wao wakubwa, majirani zao Manchester United.

Manchester City iliingia dakika 90 ikiwa nyuma kwa mabao 2-1 lakini kona yao ya 18 walioipata kwenye mechi hii ilizaa matunda kwa mshambuliaji wao Edin Dzeko kuiunganisha kwa kichwa kilichojaa kwenye nyavu za Queens Park Rangers iliyokuwa ikipigania isishuke daraja.

Dakika moja baadae, Sergio Aguero aliifungia Manchester City goli lililoipa Man City ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 44.

Shamra shamra za goli hilo la Aguero ziliwanyamazisha washabiki wa Manchester United ambao walidhani wamechukua kombe baada ya mechi yao na Sunderland kumalizika wakiwa wameshinda 1-0 huku katika mechi ya Man City, QPR walikuwa wamelazimisha sare ya 2-2 hadi dakika za majeruhi.

Manchester City imechukua ubingwa kwa tofauti kubwa ya magoli manane kulinganisha na Manchester United pamoja na kwamba wamelingana kwa pointi 89.

Arsenal imemaliza ikiwa nafasi ya tatu wakati Tottenham Hotspur inashika nafasi ya nne huku Chelsea ikimaliza nafasi ya sita na Liverpool nafasi ya nane.

Timu zilizoshuka daraja ni Wolverhampton Wanderers, Blackburn Rovers na Bolton Wanderers.

 
Na Mohamed Kindindi, Uingereza    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: J_G aka    Monday, May 14, 2012 10:30:22   
 
UBUGUVU tajijuu,
 
 
Mtoa Maoni: Khatib Haji Dau    Monday, May 14, 2012 12:23:40   
 
Aliyejuu hushuka na wa chini hupanda.Manchester City juu,juu, juu zaidi.
 
 
Mtoa Maoni: mimi    Monday, May 14, 2012 14:16:26   
 
hawa jamaa mwaka huu walistahili huu ubingwa! Man U wamecheza wenyewe walikuwa vantage ya point 8 wanakuja kukumbuka shuka wakati kumekucha! mwanza boy chakula cha wakubwa!, unatoa mbwa ktk banda. mwanza boy chokoraa
 
 
Mtoa Maoni: Boniventura    Tuesday, May 15, 2012 14:46:21   
 
Asiyekubali kushindwa si mshindani. Big up kwa sana Man City. Mmejituma sana msimu huu na mmevuna kabisa mlichopanda.
 
 
Mtoa Maoni: BnkTQZQUyQ    Tuesday, June 19, 2012 11:55:25   
 
I see, I spposue that would have to be the case.
 
 
       Jumla kuna maoni (6), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za michezo
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> MANJI atangaza kuachia ngazi Yanga
> Yanga na Simba Hakuna Mbabe 3-3
> LIVE VIDEO - TANZANIA - IVORY COAST High Quality
> Taifa Stars Yafa Kiume Morocco, Yalala 2-1
> Mechi ya Simba na Yanga Yaingiza Milioni 500
> VIDEO - Nyota wa Liverpool, Suarez Amng'ata Mkono Beki wa Chelsea
> Drogba Aitosa Chelsea na Kujiunga na Galatasaray
> VIDEO - Staili Mpya ya Kushangilia Goli Kwa Makalio
> Yanga Yawabamiza Wasauzi 3-2
> Yanga Yatoka Droo na Wajerumani
> Zanzibar Heroes ya futwa kwa utovu wa nidhamu
> KILIMANJARO STARS YATOLEWA CHALLENGE
> VIDEO - Jamaa Anayeipenda Yanga Kuliko Kitu Chochote
> Simba na Yanga Hakuna Mbabe, Zatoka Sare 1-1
> Kuiona Mechi ya Simba na Yanga ni 5000/=
> Simba Yashushiwa Kichapo cha Mabao 3-1 na Azam, Yatolewa Kombe la Kagame
> Yanga Yatinga Nusu Fainali Kombe la Kagame, Yaibanjua Mafunzo
> Simba Nayo Yabugizwa 2-0 na URA ya Uganda
> Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0
> Drogba Atimukia China, Kulipwa Kitita cha Nguvu
> Maximo Arudi Nchini Toka Brazili Kuifundisha Yanga
> Beki wa Simba Atimukia Yanga Kwa Milioni 30
> Chelsea Mabingwa Wapya wa Ulaya, Yaizamisha Bayern Munich
> Manchester City Yatawazwa Mabingwa wa Uingereza

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD