Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Simba Yalowa Sudan, Yafungwa 9-8 Kwa Penalti

NewsImages/6409638.jpg
Monday, May 14, 2012 1:59 AM
Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC imetupwa nje ya michuano ya kombe la shirikisho Africa CAF kwa mikwaju ya penalti 9-8 na timu ya Al Ahly Shandy ya Sudan baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kwenye dakika 90 za mechi hiyo ya marudiano.
Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba wameshindwa kuunguruma nchini Sudan na kukubali kipigo cha mabao 3-0 toka kwa Al Ahly Shandy na baadae kutolewa kwa mikwaju ya penalti 9-8.

Simba iliingia kwenye mechi hiyo ikiwa na ushindi wa mabao 3-0 iliupata kwenye mechi ya awali iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Simba, Emanuel Okwi alifunikwa kwenye mechi hiyo na alishindwa kabisa kuonyesha cheche zake kama ilivyokuwa kwenye mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.

Simba iliweza kujilinda kwenye kipindi cha kwanza na haikuruhusu washambuliaji wa Al Ahly Shandy kuliona lango lake. Timu zote mbili zilienda mapumziko zikiwa 0-0.

Katika kipindi cha pili, Simba ilikubali kuruhusu magoli mawili ya haraka kwenye dakika ya kwanza na ya tatu ya kipindi cha pili.

Katika dakika ya 59 makosa ya Victor Costa yalipelekea mshambuliaji wa Al Ahly Shandy, Farid Mohammed kuipatia timu yake goli la tatu lililoizamisha kabisa vijana hao wa mtaa wa Msimbazi.

Mechi hiyo ilimalizika Simba ikiwa imelala 3-0 na mechi hiyo ikabidi iingie kwenye hatua ya mikwaju ya penalti.

Penalti 10 zilipigwa ambapo Simba walikosa penalti mbili zilizopigwa na Patrick Mutesa Mafisango na Juma Kaseja. Kaseja pia aliokoa penalti moja ya Al Ahly Shandy.

Kwa kipigo hicho, Simba imeliaga kombe hilo na kuiacha Al Ahly Shandy ikisonga mbele.

 
Nifahamishe.com    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: J_G aka    Monday, May 14, 2012 02:38:21   
 
Ah.. nilikuwepo!!
 
 
Mtoa Maoni: Jamrock    Monday, May 14, 2012 04:10:31   
 
TEH TEH TEH,UBUGUVU UPO HAPO?TEH TEH TEH
 
 
Mtoa Maoni: JHN    Monday, May 14, 2012 05:27:07   
 
IVO Tz mnawaza nini kataka football? Cup gani mtachukuwa na mchezo wenu sio wa kiwango cha ju na wachezaji wana lipwa pesa za kununuwa madaf kariako!!!! labda mwanza boy awe coach wa simba na yanga na baadaye awe wa taifa stars mtapata half cup.
 
 
Mtoa Maoni: Herbert .Natai    Monday, May 14, 2012 08:23:18   
 
Mkubali matokeo huo ndio mpira wetu
 
 
Mtoa Maoni: MZEE MKWANDA    Monday, May 14, 2012 14:17:26   
 
HAWA WACHEZAJI WA SIMBA WALIKUWA WAMELEGEA SANA KWENYE MECHI HII YA SUDAN.
NYINYI MSHASHINDA MABAO-3 NYUMBANI ILIBIDI WAKAZANE SIO KULEGELEA MPIRA WA MIGUU SIO LELEMAMA AU MKWAJU NGOMA INABIDI UKAZE MSHIPA.
NA AFADHALI WAMETOLEWA KWENYE RAUDI HII KWENYE RAUNDI ZA MBELE MNGEWAONEA HURUMA MAANA WANGEKUTANA NA VIDUME WA TIMU KAMA MAZEMBE AU ZAMALEK/AHLY NDIO WANGETUTIA AIBU ZAIDI KWA MAGOLI WATAKAYOFUNGWA.
SIMBA/YANGA WATAMBE HAPA HAPA AFRICA YA MASHARIKI TUU.
 
 
       Jumla kuna maoni (15), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za michezo
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> MANJI atangaza kuachia ngazi Yanga
> Yanga na Simba Hakuna Mbabe 3-3
> LIVE VIDEO - TANZANIA - IVORY COAST High Quality
> Taifa Stars Yafa Kiume Morocco, Yalala 2-1
> Mechi ya Simba na Yanga Yaingiza Milioni 500
> VIDEO - Nyota wa Liverpool, Suarez Amng'ata Mkono Beki wa Chelsea
> Drogba Aitosa Chelsea na Kujiunga na Galatasaray
> VIDEO - Staili Mpya ya Kushangilia Goli Kwa Makalio
> Yanga Yawabamiza Wasauzi 3-2
> Yanga Yatoka Droo na Wajerumani
> Zanzibar Heroes ya futwa kwa utovu wa nidhamu
> KILIMANJARO STARS YATOLEWA CHALLENGE
> VIDEO - Jamaa Anayeipenda Yanga Kuliko Kitu Chochote
> Simba na Yanga Hakuna Mbabe, Zatoka Sare 1-1
> Kuiona Mechi ya Simba na Yanga ni 5000/=
> Simba Yashushiwa Kichapo cha Mabao 3-1 na Azam, Yatolewa Kombe la Kagame
> Yanga Yatinga Nusu Fainali Kombe la Kagame, Yaibanjua Mafunzo
> Simba Nayo Yabugizwa 2-0 na URA ya Uganda
> Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0
> Drogba Atimukia China, Kulipwa Kitita cha Nguvu
> Maximo Arudi Nchini Toka Brazili Kuifundisha Yanga
> Beki wa Simba Atimukia Yanga Kwa Milioni 30
> Chelsea Mabingwa Wapya wa Ulaya, Yaizamisha Bayern Munich
> Manchester City Yatawazwa Mabingwa wa Uingereza

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD