Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Simba Yaibugiza Yanga 5-0

NewsImages/6392286.jpg
Wachezaji wa Simba wakishangilia ubingwa
Monday, May 07, 2012 2:27 AM
Aungurumapo Simba nani husimama?
Simba imesherehekea kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kuwabugiza wapinzani wao timu ya Yanga mabao 5-0 katika mechi kali ya kusimumua iliyofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao matatu ya zawadi ya penati kutoka kwa mwamuzi Hashim Abdallah yamesheheresha ubingwa wa Simba wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Timu hiyo kutoka mitaa ya Uhuru na Msimbazi iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya watani wake wa jadi, Yanga ambao mashabiki wake walitabiri kipigo hicho kabla kutokana na migogoro isiyokwisha na kususia kuja kuona mechi hiyo kama ilivyo kawaida.

Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi, ndiye aliyeanza kuona lango la Yanga, alipoifungia Simba goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza dakika ya kwanza na sekunde ya 10 muda mchache tu baada ya mpira kuanza, bao ambalo lilidumu hadi zilipomalizika dakika 45 za kipindi cha kwanza huku Yanga wakionekana kutawala mchezo huo kipindi chote na kufufua matumaini kwa mashabiki wake ambao wengi walihisi bao la kwanza lilikuwa ni la bahati tu.

Kipindi cha Pili kilipoanza Dakika ya 53, Beki wa Yanga Shadrack Nsajigwa alimchezea vibaya Emanuel Okwi katika eneo la hatari na kusababisha penati iliyowekwa kimiani na Felix Sunzu.

Dakika ya 62, Emmanuel Okwi aliwatoka mabeki wa Yanga na kumchungulia Kipa wa Yanga, Said Mohamed, na kuandika bao la 3 na mnamo Dakika ya 66 Emmanuel Okwi kwa mara nyingine tena alichezewa vibaya eneo la hatari na beki, Goy Taita na kusababisha penati iliyopigwa na kipa wa Simba Juma Kaseja.

Dakika ya 70, Emmanuela Okwi tena aliwekwa chini na kuzaa penati iliyopigwa na Patrick Mafisango na kuandika bao la 5 ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo.

Baada ya mchezo huo Simba walikabidhiwa Kombe na kutawazwa kuwa mshindi mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Msimu wa 2012.

MATOKEO YA MICHEZO MINGINE YA KUMALIZIA LIGI ILIYOCHEZWA LEO NI : -
Coast Union ya Tanga 1 Toto African ya Mwanza 0
Villa Squard 2 Ruvu Shooting 1
Azam Fc 2 Kagera Sugar 1
Moro Utd 0 Mtibwa Sugar 1
Polisi Dodoma 0 JKT Oljoro 1

Kwa matokeo hayo sasa timu za Villa Squard, Polisi Dodoma na Moro United zitakuwa zimeshuka Daraja msimu huu.

 
Na Muhidini Sufiani    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Jamrock    Monday, May 07, 2012 08:31:31   
 
TEH TEH TEH,YANGA KWELI MMEGALAGAZWA MPAKA BASI,NI BORA MUACHE MPIRA,MKAUZE MITUMBA TU,TEH TEH TEH
 
 
Mtoa Maoni: ilaka    Monday, May 07, 2012 08:36:42   
 
hahaha! nais tri.
 
 
Mtoa Maoni: J_G aka    Monday, May 07, 2012 08:37:15   
 
JAMROCK tajijuuu! KDDDK! hoi bin taaban! UBUGUVU hongela!! KDDDK too!
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za michezo
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> MANJI atangaza kuachia ngazi Yanga
> Yanga na Simba Hakuna Mbabe 3-3
> LIVE VIDEO - TANZANIA - IVORY COAST High Quality
> Taifa Stars Yafa Kiume Morocco, Yalala 2-1
> Mechi ya Simba na Yanga Yaingiza Milioni 500
> VIDEO - Nyota wa Liverpool, Suarez Amng'ata Mkono Beki wa Chelsea
> Drogba Aitosa Chelsea na Kujiunga na Galatasaray
> VIDEO - Staili Mpya ya Kushangilia Goli Kwa Makalio
> Yanga Yawabamiza Wasauzi 3-2
> Yanga Yatoka Droo na Wajerumani
> Zanzibar Heroes ya futwa kwa utovu wa nidhamu
> KILIMANJARO STARS YATOLEWA CHALLENGE
> VIDEO - Jamaa Anayeipenda Yanga Kuliko Kitu Chochote
> Simba na Yanga Hakuna Mbabe, Zatoka Sare 1-1
> Kuiona Mechi ya Simba na Yanga ni 5000/=
> Simba Yashushiwa Kichapo cha Mabao 3-1 na Azam, Yatolewa Kombe la Kagame
> Yanga Yatinga Nusu Fainali Kombe la Kagame, Yaibanjua Mafunzo
> Simba Nayo Yabugizwa 2-0 na URA ya Uganda
> Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0
> Drogba Atimukia China, Kulipwa Kitita cha Nguvu
> Maximo Arudi Nchini Toka Brazili Kuifundisha Yanga
> Beki wa Simba Atimukia Yanga Kwa Milioni 30
> Chelsea Mabingwa Wapya wa Ulaya, Yaizamisha Bayern Munich
> Manchester City Yatawazwa Mabingwa wa Uingereza

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD