Kompyuta na Monitors, Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Chelsea Yaibanjua Barcelona, Yatinga Fainali

NewsImages/6373970.jpg
Fernando Torres akilizamisha jahazi la Barcelona kwa goli safi lililoifanya Chelsea itoke sare ya 2-2 na Barcelona
Wednesday, April 25, 2012 2:05 AM
Ikicheza pungufu wachezaji 10 kwa takribani lisaa limoja, Chelsea wameweza kufanya kilichoonekana hakiwezekani kwa kuibwaga Barcelona na kuitupa nje ya mashindano ya kombe la mabingwa wa ulaya.
Timu ya Chelsea ya Uingereza imeweza kufanya kile ambacho watu wengi waliona hakiwezekani.

Chelsea imeweza kuitupa nje ya mashindano Barcelona ya Hispania kwa jumla ya magoli 3-2 baada ya kutoka sare ya 2-2 kwenye mechi kali ya kusisimua kwenye uwanja wa Nou Camp jijini Barcelona.

Chelsea ingawa ilicheza staili ya kujihami zaidi ikilundika wachezaji wake wote ndani ya 18, ilifanikiwa kuiminya Barcelona na kutinga fainali ya kombe la mabingwa wa ulaya ambapo fainali itachezwa mjini Munich Ujerumani mnamo tarehe 19 mwezi ujao.

Chelsea itapambana na mshindi wa mtange wa kukata na shoka leo kati ya Real Madrid na Bayern Munich.

Katika mechi na Barcelona, nahodha wa Chelsea John Terry alitupwa nje ya uwanja baada ya kupigwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mshambuliaji wa Barcelona, Alexis Sanchez ambaye alikuwa hana mpira.

Baada ya mechi, John Terry alikri kosa lake na aliwaomba msamaha wachezaji wenzake na washabiki wa Chelsea akisema kuwa amewaangusha kwa kitendo chake cha kumchezea rafu Sanchez huku akiwa hana mpira.

Katika mechi hiyo ambapo Lionel Messi alikosa penalti kwa kugongesha mwamba, magoli ya Chelsea yalifungwa na Ramires kwenye dakika ya 45 na Fernando Torres kwenye dakika ya 90.

Barcelona ndiyo iliyotangulia kuliona lango la Chelsea kwa mabao yaliyofungwa na Busquets kwenye dakika ya 35 na Iniesta kwenye dakika ya 43.

Akizungumza baada ya mechi, kocha wa Chelsea, Roberto Di Matteo aliwapongeza sana wachezaji wake kwa ujasiri na jinsi walivyojituma na kuipigania Chelsea.

Di Matteo pia alisema kuwa John Terry pia ni binadamu hivyo anaweza kufanya makosa.

"Unauliza nina hasira naye?, hapana sijamkasirikia, sisi sote ni binadamu hivyo wakati mwingine tunakosea", alisema Di Matteo alipoulizwa kuhusiana na kadi nyekundu ya John Terry.

 
Na Mohamed Kindindi, Uingereza    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: ukweli    Wednesday, April 25, 2012 06:05:38   
 
barcelona wachezaji wamishaa zeeka sasa wanatakiwa kubadiliswa imechoka
 
 
Mtoa Maoni: JUDEX    Wednesday, April 25, 2012 06:44:15   
 
Mimi na mapira NISAHAULIWE, kwa upande wangu ushindi wa chelsea ulikuwa ni maudhi sana! nashangaa mtaani zogo za magoma mpaka alfajiri, hapa nina ucngz kibao! mitaa ya uswahilini watu wana maudhi kweli, sawa timu imeshinda lakini msiwakere watu waliolala! mlitakiwa msherehekee KIMYAKIMYA hadi asubuhi.
 
 
Mtoa Maoni: Fikiri michael    Wednesday, April 25, 2012 07:33:23   
 
Timu zote zipo sawa mi sioni iliochoka
 
 
Mtoa Maoni: kadwame    Wednesday, April 25, 2012 10:22:40   
 
oya judex pole sana ndugu yangu kwa kufungwa chelsea timu kubwa
 
 
Mtoa Maoni: J_G aka    Wednesday, April 25, 2012 11:41:52   
 
Yanga na chelsii nani mkali? KDDDK!!
 
 
       Jumla kuna maoni (9), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za michezo
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> MANJI atangaza kuachia ngazi Yanga
> Yanga na Simba Hakuna Mbabe 3-3
> LIVE VIDEO - TANZANIA - IVORY COAST High Quality
> Taifa Stars Yafa Kiume Morocco, Yalala 2-1
> Mechi ya Simba na Yanga Yaingiza Milioni 500
> VIDEO - Nyota wa Liverpool, Suarez Amng'ata Mkono Beki wa Chelsea
> Drogba Aitosa Chelsea na Kujiunga na Galatasaray
> VIDEO - Staili Mpya ya Kushangilia Goli Kwa Makalio
> Yanga Yawabamiza Wasauzi 3-2
> Yanga Yatoka Droo na Wajerumani
> Zanzibar Heroes ya futwa kwa utovu wa nidhamu
> KILIMANJARO STARS YATOLEWA CHALLENGE
> VIDEO - Jamaa Anayeipenda Yanga Kuliko Kitu Chochote
> Simba na Yanga Hakuna Mbabe, Zatoka Sare 1-1
> Kuiona Mechi ya Simba na Yanga ni 5000/=
> Simba Yashushiwa Kichapo cha Mabao 3-1 na Azam, Yatolewa Kombe la Kagame
> Yanga Yatinga Nusu Fainali Kombe la Kagame, Yaibanjua Mafunzo
> Simba Nayo Yabugizwa 2-0 na URA ya Uganda
> Hispania Ndio Mabingwa Wa Ulaya, Waibugiza Italia 4-0
> Drogba Atimukia China, Kulipwa Kitita cha Nguvu
> Maximo Arudi Nchini Toka Brazili Kuifundisha Yanga
> Beki wa Simba Atimukia Yanga Kwa Milioni 30
> Chelsea Mabingwa Wapya wa Ulaya, Yaizamisha Bayern Munich
> Manchester City Yatawazwa Mabingwa wa Uingereza

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD