|
Precision Air yaanza safari za Bukoba |

Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air, Alfonse Kioko akielezea uzinduzi wa safari za Bukoba |
Wednesday, February 02, 2011 3:17 AM
Kampuni ya shirika la ndege la Precision Air limezindua rasmi safari za ndege kwenda Bukoba. |
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Alfonse Kioko alisema kuwa wanayo furaha kubwa ya kuwafahamisha wateja wetu kuwa tunaaza tena safari za kwenda Bukoba kuanzia tarehe 12 mwezi huu wa pili baada ya kusitisha safari hizo kwa zaidi ya mwaka sasa.
Uzinduzi wa safari hizo unafuatia kumalizika kwa ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Bukoba uliofanywa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.
"Huduma ya safari itakuwepo kila siku kutoka Dar es Salaam kupitia Mwanza na kutoka Bukoba kwenda maeneo tofauti katika mtandao wetu," alisema Kioko.
"Tunaanza na bei ya Tshs. 454,000 kwa safari ya kwenda na kurudi," aliongeza Kioko.
Katika safari za Bukoba, Precision Air itatumia ndege aina ya ATR42-500 iliyopewa jina la Bukoba kama ishara ya shukrani kwa watu wa mkoa huo. |
|
Na Kalimanzila, Dar
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
Mang
Wednesday, March 16, 2011 13:18:36
|
|
Mtoa Maoni:
joyce rwehumbiz
Thursday, June 02, 2011 12:25:29
|
|
Mtoa Maoni:
saleh
Monday, August 08, 2011 13:38:28
|
|
Mtoa Maoni:
ayoub stambuli
Wednesday, September 07, 2011 19:30:22
|
|
Mtoa Maoni:
anita
Monday, September 26, 2011 15:22:42
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (27), Soma maoni yote |
|
|
|
Habari zaidi za biashara na uchumi |
...Habari Zaidi
|
|
|