Kompyuta na Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Precision Air yazindua nauli maalumu ya Sunrise

NewsImages/5326102.jpg
Meneja masoko wa Precition Air Emillian Rwejuna kulia akiongea na waandishi wa habari kushoto Mkurugenzi wa biashara wa kampuni hiyo Phil Mwakitawa
Saturday, January 22, 2011 1:09 AM
Kampuni ya safari za ndege ya Precision leo imezindua nauli maalumu kwa wasafiri wa ndege wa kampuni hiyo kwenda na kutoka Visiwani Zanzibar.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Biashara - Phil Mwakitawa alisema; “Kwa muda wa miezi mitano ijayo abiria wetu kwenda na kutoka Zanzibar watalipa kiasi cha Shilingi za Tanzania 35,000 kwa safari moja na Shilingi za Kitanzania 60,000 kwa safari ya kwenda na kurudi.”

Pamoja na hayo, kampuni ya ndege ya Precision Air ilianzisha safari za ndege za mapema alfajiri mnamo mwezi Novemba mwaka jana ili kutoa nafuu hasa kwa wafanyabiashara kwa kuondoa usumbufu kwa abiria wake wanaosafiri katika njia hiyo.

Safari ya ndege ya mapema alfajiri kwenda Zanzibar inaondoka Jijini Dar es Salaam saa saba na nusu usiku wakati safari ile ya kutoka Zanzibar kwenda Jijini Dar es Salaam inaondoka Zanzibar saa nane na nusu usiku.

Kuongezwa kwa safari hiyo ya mapema alfajiri inafanya safari za ndege kwenda Zanzibar kufikia nne na zile za kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam kufikia saba.

“Kwa kuanzishwa kwa safari hii ya mapema alfajiri, kwa sasa ni rahisi kwa abiria kwenda Zanzibar kwa ndege mapema kabla ya shughuli za kibiashara hazijaanza, kuhudhuria miadi pamoja na wale wanaotaka kuwasili Jijini Dar es Salaam mapema”, alisema Mwakitawa.

Kampuni ya ndege ya Precision imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja wake kwa kutumia vifaa vyake vipya na vya kisasa katika soko la biashara ya ndege.

Mnamo mwaka 2006 Kampuni ya Ndege ya Precision na kampuni ya kutengeneza ndege ya ATR walisaini mkataba wa Dola milioni 129 kwa ajili ya ununuzi wa ndege saba mpya katika mpango wake wa kuboresha ndege zake. Ndege ya mwisho kutoka ATR iliwasili Jijini Dar es Salaam mwezi Septemba mwaka jana.

Mkataba huu wa kibiashara wa ndege hizi saba (2 ATR 42-500 na 5 ATR 72-500) uliiwezesha Precision Air kutunukiwa kwa zawadi mbili za kimataifa.

Mwezi Aprili 2009, Jarida la Air Finance liliuzawadia mkataba huu kuwa Mkataba wa kibiashara bora zaidi kwa Afrika katika mwaka 2008. Mkopo wa ndege za ATR ulikuwa umeishazawadiwa Desemba mwaka juzi na Gazeti la Usafirishaji Jane’s Finance, kama “Mkopo mkubwa wa mwaka Afrika wa ndege 2008.”

Kuletwa kwa ndege hiyo ya mwisho mwezi Septemba imefanya kampuni hii ya ndege kuwa na jumla ya ndege kumi, saba kati ya hizo ni mpya kabisa. Kampuni ya Precision Air pia inatumia ndege moja aina ya Boeing 737.

Kampuni hii ya ndege ina mtandao mkubwa wa safari za anga ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara.

Kampuni ya Precisionair pia hufanya safari zake za anga katika miji ya Nairobi na Mombasa nchini Kenya na Entebbe nchini Uganda.

 
Na kalimanzila, Dar    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Ubuguvu    Saturday, January 22, 2011 05:12:32   
 
Kwa maana hiyo anataka kutwambia airport ya dar ni 24 hrs siku hizi haifungwi? Maana mimi nilipokuwa tz mwaka jana mwishoni kufika Saa saba ya usiku uwanja umefungwa kila upandi ninaotazama nakutana na visanduku vya misada lkn kutokana kuwa bore pale uwanjani sikuwa na nguvu ya kusoma vyote wanaomba nini lkn nadhani hakikosi kisandu cha bili ya umeme wa airport.
 
 
Mtoa Maoni: mark.mushi    Saturday, January 22, 2011 12:30:50   
 
boing 737?mimi nafikiri boing 747 kumbe ako 737,ubuguvu wa2mie ndege bwana.....wamechoka hawo apo airport wanapiga mizinga2,moms016nitafutie demu bikira basi uko ulipo?maananamsaka kweli yani...nawasifu kwa nauli ya35elifu kwenda zenji,aya sasa wale ambao amjawai kupanda ndege changamkeni jamani mtakufa amjaipanda mtaishia kuziona2kwa macho,ila nauli ya 35 usalama upo?bora boti ya bakhressa?apo yangu ni klm,swiss,air france nikijaga bongo,klm kama nikishukia moshi kilimanjaro,aka kia,fcebok
 
 
Mtoa Maoni: Semenya    Saturday, January 22, 2011 14:14:56   
 
Hahhaaaa!! UBUGUVU wewe hasaa hujatulia mwanawani unakandia nchi yetu saaaaana!! Anyway angalau nitapata kwenda kumtembelea shogangu MOMSO a.k.a KAVUVI kwa masaa machache nikishakula pweza narudi zangu Dar.
 
 
Mtoa Maoni: Mang    Saturday, January 22, 2011 16:17:30   
 
Hongera Shirika la Precisionair!
 
 
Mtoa Maoni: pili    Sunday, January 22, 2012 16:29:14   
 
MARK MUSHI
Sasa kwa nini huleti hiyo yako 747 utupe URODA!

 
 
       Jumla kuna maoni (21), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za biashara na uchumi
> Benki ya Vijana kuzinduliwa
> Jishindie Milioni 3 Kila Siku na Vodacom
> Precision Air yaanza safari za Bukoba
> Precision Air yazindua nauli maalumu ya Sunrise
> Zain sasa ni Airtel
> Nokia Yatoa Simu Zinazochajiwa na Baiskeli
> TBL yapigwa faini kuvuruga ushindani wa kibiashara
> Gharama za huduma za simu zazidi kupungua
> Uzalishaji wa Bia Mpya TBL Wasimama Baada ya Mitambo Kuungua
> Ewura yashtua wabunge kwa kuwa na matumizi makubwa
> Zain yaja na Balckberry Pre Paid
> Wakulima wa embe wasaidiwa milioni 126/-
> BOT, NMB ijiunge na umoja switch kuondoa kero
> Soko la samaki laingiza bilioni mbili
> Serengeti Breweries yatunzwa tunzo ya dhahabu
> VIDEO - Dhahabu Zatumika Kununulia Mkate Zimbabwe
> ATM 'Yapagawa' na Kuwajaza Watu Mapesa Italia
> Wafanyabiashara Watakiwa Kujitangaza
> BET Yatoa Elimu Kwa Wajasiliamali Nchini
> Wengi hawajui kama simu za zamani zinaweza kutumika kutengeneza vitu vingine
> Mmea wa Mbuyu Unatakiwa Kuzalishwa Kwa Wingi- Wizara
> Arusha Thomson Safaris named among 2009 Best Adventure Travel Companies on Earth
> Mifuko ya Rambo kupigwa marufuku Tanzania
> Uuzaji wa Pamba Nje Marufuku
> Uzalishaji Korosho Utashuka

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Je unahitaji kompyuta zenye ubora wa kimataifa toka Uingereza?: Namba za simu Uingereza 00447404851682 Namba za simu Tanzania: 00255783054508 au 00255762486583
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD