Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Skendo la Ununuzi wa Rada ya Tanzania, BAE Yapigwa Faini Dola Milioni 450


Wakala wa ununuzi wa rada ya Tanzania, Shailesh Vithlani
Monday, February 08, 2010 3:16 AM
Skendo la ununuzi wa rada ya ulinzi ya Tanzania toka kwa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza limechukua sura nyingine nchini Uingereza kwa kampuni ya BAE kupigwa faini ya dola 450 kwa kukiri kutumia rushwa kukamilisha madili yake.
Kampuni ya BAE System iliyoiuzia rada ya ulinzi Tanzania imepigwa faini ya jumla ya dola Milioni 450 (Zaidi ya Tsh. Bilioni 580) kwa kutumia rushwa katika kukamilisha dili zake na Tanzania, Jamhuri ya Cheki, Hungary na Saudi Arabia.

Awali taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza iliipa mwezi mmoja BAE Systems kukiri makosa yake au kufikishwa mahakamani

Awali SFO iligundua kuwa mkataba wa ununuzi wa rada wa mwaka 1999, kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uingereza ya BAE Systems uligubikwa na rushwa kubwa.

Ununuzi wa rada hiyo ulifanikishwa na wakala Shailesh Vithlani ambaye aliifanya Tanzania itoe TSh bilioni 16 zaidi ya bei halisi katika ununuzi wa rada hiyo.

Vithlani inasemekana alipewa dola milioni 12 (zaidi ya TSh. bilioni 12) kama kamisheni ya kufanikisha dili hilo na inasemekana aligawana pesa hizo na maafisa saba wa ngazi za juu katika serikali ya Tanzania.

Vithlani alitoroka Tanzania miaka mitatu iliyopita akiwa nje kwa dhamana baada ya kufunguliwa mashtaka na alikamatwa mwaka jana nchini Uswizi alikokuwa akijificha.

Mbali na rushwa kutumika katika ununuzi wa rada ya Tanzania, BAE pia ilituhumiwa kutumia rushwa katika kukamilisha uuzaji wa ndege moja ya kijeshi kuiuzia nchi ya Afrika Kusini na uuzaji wa ndege nyingine ya kijeshi ambao haukufanikiwa kwa Jamhuri ya Cheki.

"Kampuni ya BAE inajutia yaliyotokea na inakubali kubeba mzigo kwa matatizo yaliyotokea", alisema mwenyekiti wa BAE, Dick Olver.

BAE ilikiri kuwa malipo ya kamisheni kwa mtekelezaji wa dili la rada ya Tanzania hayakuwekwa wazi kama ilivyotakiwa na kwasababu hiyo BAE imekubali kutoa paundi milioni 30 ambazo baadhi ya pesa hizo zitatumika kwaajili ya manufaa ya Tanzania.

Mkurugenzi wa SFO, Richard Alderman alielezea kufurahishwa kwake na makubaliano yaliyofikiwa na kuongeza kuwa huo ndio utakuwa mwisho wa uchunguzi wao kwa kampuni ya BAE.

 
Source: AFP    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Ubuguvu    Monday, February 08, 2010 07:30:36   
 
mimi sijui kilichotupata mpaka kununua rada ya ulinzi kwa pesa nyingi wakati nchi yetu inamatatizo mengi zaidi kuliko usalama wetu na nchi jirani tz sio kama nchi za mashiki ya kati madui wenyewe kwa wenyewe lakini sisi tatizo letu kubwa ujambazi rusha na ufisadi na haya rada haioni japokua wengi hawajui kama MOMS016 anataka majambazi na marelia yote yachunguzwe na rada nchi yetu inaitaji umeme wa kudu maji safi MINA apunzike kubeba maji na kichwg natamani ile sheria ukiwa rais wa tz hushit
 
 
Mtoa Maoni: KING    Monday, February 08, 2010 08:51:18   
 
@Pole sana mdau UBUGUVU kwa kutojua kilichotupata, ukweli ni kuwa tumekosa vipaumbele vya maana!

Hii ni geresha tu, hiyo fine analipwa nani? Kampuni baradhuri kuilipa serikali dharimu, ama? C la kufurahia hili manake tumeibiwa na katu hatupati chochote hapo, wanalipana wenyewe. Hii ingekuwa na maana japo kidogo kwetu Tz kama hayo mamilioni ya dola yangelipwa kwetu tulioibiwa. Hili ni changa la macho..........tumelambwa mkono kwa mara nyingine!

 
 
Mtoa Maoni: MINA    Monday, February 08, 2010 09:19:36   
 
mmh HII SASA KALI me ata sina la kuongea mana tuanapata habari mambo yalishapita na sidahani kama iansaidia nahisi hii ni danganya toto kama anavyosema KING. UBUGUVU sidhani kama taacha kubeba maji kichwani mana mwenyewe uanelewa ndio mana utaki kurudi... MOMSO16 NIMEKUMISS MCHUMBA Haaaaaa.. tajijuuu
 
 
Mtoa Maoni: idi issa    Monday, February 08, 2010 09:56:02   
 
tuanaongozwa na wanyama na sio binadamu huko tanzania jamani, kikwete na mkapa ni wabovu hasa
 
 
Mtoa Maoni: zhao    Monday, February 08, 2010 10:04:15   
 
duuu, haya basi gawaneni hizo pesa viongozi wa tz,zikioza tupeni ss kama wale samaki,viongozi wa tz mnataka na mna upenda ufahari kwa masilahi yenu,hamjali raia wala nn,lkn mtaendelea kupunwa daily nyinyi,kisha mnazulumu ndio god anawarudi.barabara zinamatundu kibaoo,mnatunywisha maji machafu lkn poa.TENGEZENI NCHI HAMNA CHA MANA KITAKACHOPELEKEA KUVAMIWA AU MNAUNDA SILAHA ZA NUCLEAR NDIO MNATAKA KUJILINDA?mashuduuu
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za Tanzania
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Polisi kwa kete 300 za bangi
> Tani za mtama usiofaa wakamatwa Zanzibar
> Jeshi la Polisi laimarisha ulinzi Kariakoo
> Tendwa atupilia mbali pingamizi la Chadema
> Aangua kilio baada ya kutapeliwa- Kar iakoo
> Sheria isipofata mkondo wake, nitaandaa maandamano-Baswalehe
> Darasa la 7 waanza mitihani leo
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Chadema yawasilisha pingamizi
> Wanafunzi waweweseka Tabata
> Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma yateketea
> Ramli ya Joseph ilisema hivi!
> 7 papohapo, wengine majeruhi ajalini- Mabibo
> Makahaba msipotoshe vazi hili!
> Sakata la kugombania maiti bado tata
> Mahakamani kwa kujipatia ngono kwa njia ya madawa ya kulevya
> Chadema yamuwekea pingamizi Kikwete

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake