Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Uingereza Kuzibania Viza Za Wanafunzi


Monday, February 08, 2010 2:39 AM
Serikali ya Uingereza imetangaza mpango wake wa kupunguza idadi ya wanafunzi wanaopewa viza za kusoma nchini humo.
Serikali ya Uingereza imetangaza kuweka sheria na masharti magumu katika utolewaji wa viza za uanafunzi.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza, Alan Johnson amesema kuwa masharti magumu yameongezwa katika maombi ya viza za uanafunzi kwa wanafunzi toka nchi zote duniani.

Mojawapo ya masharti yaliyoongezwa katika uombaji wa viza za uanafunzi ni kwa mwanafunzi anayeomba viza kutakiwa awe anaongea kiingereza fasaha.

Miongoni mwa sheria ziliongezwa ni kama vile kuwazuia wanafunzi wenye viza za muda mfupi kuwaleta Uingereza jamaa zao kama vitegemezi (dependant) wao.

Sheria mpya zimewekwa kufuatia waziri mkuu wa Uingereza kutaka masharti ya utolewaji wa viza yaangaliwe upya kufuatia tukio la mwanafunzi wa Nigeria aliyemaliza masomo yake nchini Uingereza kujaribu kuilipua ndege ya Marekani bila mafanikio.

Sababu kubwa ya kuwekwa kwa sheria hizi ni kupunguza idadi ya wanafunzi toka barani Afrika na Asia ambao hujishughulisha zaidi na kufanya kazi kuliko masomo yao.

Awali mwaka mmoja uliopita Uingereza iliongeza ugumu katika utolewaji wa viza za wanafunzi kwa kuwataka wanafunzi watoe vithibitisho vya kuweza kujilipia ada yote ya masomo yao na pia kuwa na uwezo wa kifedha kukimu gharama za maisha yao nchini Uingereza.

Wiki iliyopita, Uingereza ilisimamisha kwa muda kupokea maombi ya viza za wanafunzi kutoka maeneo ya kaskazini mwa India, Nepal na Bangladesh. Hatua hiyo ilitokana na idadi kubwa kuliko kawaida ya maombi ya viza za uanafunzi toka maeneo hayo.

Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza imesema kuwa kutokana na masharti mapya ya utolewaji wa viza za wanafunzi, idadi ya wanafunzi watakaopewa viza itapungua sana lakini hata hivyo wizara hiyo ilikataa kutoa tathmini zao.

 
    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Mwanza boy    Monday, February 08, 2010 06:50:22   
 
UK njaa tupu! Heri nijikalie Mwanza ambabo maisha ni ya kuaminika zaidi. Wanaokimbilia nje nawahurumia saana! Maisha magumu sana huko. Mie nilimtemebelea shemeji yangu tukawa tunakula kwa kubahatisha. Kazi zenyewe wanazofanya ni za kijiiinga!!
 
 
Mtoa Maoni: Ubuguvu    Monday, February 08, 2010 08:04:03   
 
Mwanzaboy nakunga mkono kua maisha uk ni magumu lakini sio sawa na bongo na kugusu ndugu yako kutokua na kazi sio kigezo kua hakuna kazi sawa uk hakuna kazi za kuchajisha simu na kuuza ndo zamaji uk kila mtu ana umeme kwake sio kama tz mtu una simu nyumba unayokaa haina umeme wala maji kuifananisha uk na tz ni dhambi isiosameheka wabunge na mawaziri wa nchi mbali bali wanatamani kua raia tu uingereza then useme mwanza bora kuliko uk jana nilikua nangalia tv moja ya tz mtangazaji wa tv kacho
 
 
Mtoa Maoni: KING    Monday, February 08, 2010 09:02:08   
 
Hakuna la kulalamika hapo, wenye nchi wanalinda maslahi ya nchi zao. Cha msingi nasi ulimwengu wa tatu ni kujifunza nn tufanye kuboresha hali za maisha ktk nchi zetu ikiwamo kuboresha mazingira ya elimu bora na sio kila siku kulia kama mitoto kuomba ziwa wakati nyingi kati ya nchi zetu zinamiaka zaidi ya 30 ya uhuru. Mimi nachukulia maamuzi haya kama challenge kwetu ya kuwa wabunifu na kujitegemea zaidi, hata hz nchi zao tunazokimbilia wao walizijenga kwa jasho na damu.....nasi tufanye hv!
 
 
Mtoa Maoni: zhao    Monday, February 08, 2010 09:44:42   
 
na ss tz tunazuia kutoa viza kwa wadosi,wakonngo na wengine kibao sio,wakitaka viza waongee kiswahili fasaha
 
 
Mtoa Maoni: kaka    Monday, February 08, 2010 11:03:50   
 
yeah nadhani Serikali ya Tanzania umefika wakati wa kuweka masharti makari mno ya viza za TZ.maana sasa naona wageni wengi mno.Unajua kipindi cha nyuma maeneo kama Tandika,mbagala uwezi kumkuta mtu wa njano sasa hivi wamejaa kibao na wanafanya biashara za machinga.Kama yatawekwa masharti ya kuongea kiswahili fasaha ndugu zangu wa Asia watapungua sana kuja huku.maana wachache sana wataweza kuongea kiswahili kizuri.Serikali ya Uingereza inajisumbua tu.Wafuatilie maendeleo ya mwanafunzi.
 
 
       Jumla kuna maoni (11), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za dunia
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake
> Boti Zingine Mbili Zazama na Kuua Zaidi ya 200 Kongo
> Mwanamke Akamatwa Akijipigisha Punyeto Huku Akiendesha Gari
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Miaka 9 Jela Kwa Kuendesha Gari Huku Akiangalia Ngono
> Kama Siku ya Kufa Haijafika...
> Mapenzi Yanapozidi....
> 'Osama Bin Laden ni Kibaraka wa Marekani' - Fidel Castro
> Madaktari Watupiana Makonde Chumba cha Uzazi
> Mgahawa wa Nyama za Binadamu Wafunguliwa Ujerumani
> Rais wa Zamani wa Madagascar Ahukumiwa Kifungo cha Maisha
> Hali Hii Isifike Bongo..
> Kitabu cha Katuni za Kumkashifu Mtume Kutolewa Mwezi Ujao
> Mwarabu Ampigilia Misumari 24 Hausigeli Wake
> Nyota wa Muziki Aliyewaambukiza Watu Ukimwi Anusurika Kwenda Jela
> Miaka 20 Jela Kwa Kumtikisa Mtoto Wake Mchanga
> Wazikwa Hai Hadi Disemba...
> VIDEO - Magari 46 Yagongana, Watu 72 Wajeruhiwa

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
1 Kanisa Lasisitiza Kuchoma Mot...
2 VIDEO - Simba Alipomgeuza Asu...
3 Kelele za Kimahaba Zamponza
4 Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nch...
5 Kesi ya Rama yahamishiwa Maha...
6 Wanawake tumieni fursra hii
7 Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa...
8 Hatimaye Kanisa Laahirisha Ku...
9 Viagra Ya Saudi Arabia Yazua ...
10 VIDEO ya Salamu za EID MUBARA...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Duh pole sana
Habari Mpya Mpya
> VIDEO ya Salamu za EID MUBARAK Toka Nifahamishe.Com
> Hatimaye Kanisa Laahirisha Kuchoma Moto Quran
> Viagra Ya Saudi Arabia Yazua Mzozo
> Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha Chafu
> Kesi ya Rama yahamishiwa Mahakama Kuu
> Wanawake tumieni fursra hii
> Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza
> Kanisa Lasisitiza Kuchoma Moto Quran Jumamosi
> Kelele za Kimahaba Zamponza
> VIDEO - Simba Alipomgeuza Asusa Mkufunzi Wake