Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
VIDEO - Drogba Aizamisha Arsenal


Thomas Vermaelen wa Arsenal kushoto akiwania mpira na Didier Drogba wa Chelsea
Monday, February 08, 2010 2:26 AM
Nyota wa Ivory Coast, Didier Drogba ameendeleza rekodi yake nzuri ya kuwatungua Arsenal kwa kuifungia Chelsea mabao yote mawili katika kichapo cha mabao 2-0 walichowapa vijana wa Arsene Wenger na kulifanya pengo la pointi kati ya Chelsea na Arsenal kufikia pointi 9. VIDEO ya magoli yote katika mechi hii mwisho wa habari.
Matumaini ya Arsenal kutwaa kombe la ligi kuu ya Uingereza yamezidi kufifia baada ya kupokea kipigo cha pili mfululizo katika ligi ya Uingereza.

Wiki iliyopita Arsenal ilibamizwa 3-1 na mashetani wekundu wa mji wa Manchester, Manchester United na wiki hii imekubali kupokea kipigo kingine cha mabao 2-0 toka kwa Chelsea.

Drogba ambaye ana rekodi nzuri ya kuzifumania nyavu za Arsenal kila Arsenal inapokutana na Chelsea, ndiye aliyeifungia Chelsea mabao yote mawili katika ushindi wa leo katika uwanja wa Stamford Bridge.

Arsenal ilicheza vizuri zaidi kwenye kipindi cha pili na kulisakama sana lango la Chelsea lakini washambuliaji wake walishindwa kulipenya lango la Chelsea lililoongozwa na nahodha John Terry.

Kwa ushindi wa leo, Chelsea imejikita kileleni mwa ligi ya Uingereza ikiwazidi Manchester United wanaoshika nafasi ya pili kwa pointi mbili.

Chini ni VIDEO ya magoli yote katika mechi hii.


VIDEO - Chelsea 2-0 Arsenal





 
Na Mohamed Kindindi, Uingereza    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Nyoshi    Monday, February 08, 2010 03:22:21   
 
Arsenal hawana uwezo wa kupambana na vigogo watazionea timu ndogo tu akina stoke city na Hull City
 
 
Mtoa Maoni: KING    Monday, February 08, 2010 09:06:21   
 
Dah, Drogba kama vile alizaliwa kwenye viunga vya Highbury/Emirates.........kila siku yy kuwaua Arsenal. Anyway hii pia inanigusa manake mi mdau hapo ati, naona sasa msimu umefungwa rasmi kwetu wadau wa Emirates!
 
 
Mtoa Maoni: zhao    Monday, February 08, 2010 09:50:28   
 
DROGBA UAAAA NA BADO SHENZ TYPE,tunawangojea wahindi M UTD,tutawapiga cha bata kwao
 
 
Mtoa Maoni: Great Thinker    Monday, February 08, 2010 15:58:01   
 
Title race is not yet over. Let us wait and see.
 
 
      
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za michezo
> Ligi Kuu Bara Kuanza Jumamosi, Waamuzi Acheni Unazi
> Kenneth Asamoah Boateng: Mtambo mpya wa mabao Yanga
> 'Huu Ndiyo Uchawi Wangu' - Fuso
> Kaseja na Kado Wachuana Kuwania Jezi Namba 1
> Kocha Mpya Stars Aguswa na Kiwango cha Ngasa
> Nyota wa Uingereza Amhonga Kahaba Paundi 800 Kwa Usiku Mmoja
> Taifa Stars Kujipima Ubavu na Wamisri
> VIDEO - Ushangiliaji wa Goli Ambao Haujawahi Kutokea
> Baada ya Kubugizwa 6-0 Twiga Stars Yaja na Visingizio Kibao
> Ngassa Kizani Azam Fc
> Simba Yaiovateki Yanga na Kumsajili Gumbo
> Jeuri ya Wachina Bongo
> Kocha Wa Yanga Hataki Masihara
> Matumla Ajigamba Kumdunda Maugo
> Semenya Arudi Kwenye Riadha Kwa Ushindi
> VIDEO - Ajaribu Kuliiba Kombe la Dunia
> VIDEO - Hispania Wawa Mabingwa Wapya wa Dunia
> Wachezaji wa Hispania Waingizwa Mjini Afrika Kusini
> Sweta la Bluu Ndilo Linaloipa Ushindi Ujerumani
> Wawili Wauliwa Kenya Kwasababu ya Mechi ya Ghana
> Ghana Yawasononesha Waafrika
> Brazil Chariii!! Yatolewa Kombe la Dunia
> Ujerumani Yaicharanga Uingereza 4-1
> Ivory Coast Yaliaga Kombe la Dunia, Ghana Ndio Tegemeo Lililobaki
> Ghana Yaibeba Afrika, Algeria Yafungashwa Virago

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Namabengo Computer Repairing Services Call: 0762-486583 0r 0712-409641
Habari Zilizosomwa Sana
1 'Yesu Alikuwa ni Muathirika w...
Photo Gallery
Photo Album

 Ukisikia Wazazi bomu
Random Photo

 Ashakum
Habari Mpya Mpya
> 'Yesu Alikuwa ni Muathirika wa Ukimwi'
> PICHA - Mapenzi Yanaua..
> Askofu Awaponda Wanaomtukana Kikwete
> Siri ya Kimada Yafichuka
> Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo
> VIDEO - Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu
> Kampeni zachachamaa, wapinzani nao watoa ahadi
> JK aendelea kutoa ahadi
> Pingamizi la Chadema baada ya siku 5
> Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi