|
|
|
John Terry Anyang'anywa Unahodha Baada ya Kumtia Mimba Shemeji Yake |

John Terry |
Friday, February 05, 2010 9:50 PM
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uingereza, Fabio Capello amemnyang'anya unahodha John Terry kufuatia skendo lake la kumtia mimba mpenzi wa mchezaji mwenzake na kisha kuitoa mimba hiyo. |
Skendo la John Terry kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wa mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Uingereza limefikia hatua nyingine kwa kocha wa Uingereza kumvua unahodha John Terry.
John Terry ambaye ana mke na watoto wawili anashutumiwa kumzunguka rafiki yake Wayne Bridge ambaye walicheza pamoja Chelsea na kutembea na mpenzi wake mrembo wa Ufaransa, Vanessa Perroncel.
Mbali ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Vanessa ambaye amezaa mtoto mmoja na Wayne Bridge, Terry anadaiwa kumtia mimba Vanessa na kisha kuitoa mimba hiyo ili siri ya uhusiano wao isifichuke.
Terry alianza uhusiano na Vanessa mwaka jana baada ya Wayne Bridge kuhama Chelsea ya London na kuhamia mjini Manchester kuichezea Manchester City.
John Terry anacheza nafasi ya kati ya ulinzi katika timu ya taifa ya Uingereza wakati Wayne Bridge naye yumo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza akicheza kama beki wa kushoto.
Akiliongelea suala hilo leo mchana, kocha wa Uingereza raia wa Italia, Fabio Capello alisema kuwa ili kuikoa timu ya taifa ya Uingereza isifanye vibaya kwenye kombe la dunia, ameona ni bora amnyang'anye unahodha John Terry.
Vyombo vya habari vya Uingereza vililishikilia bango skendo la Terry na kutaka anyang'anywe unahodha lakini chama cha soka cha Uingereza kilisema kuwa uamuzi wa mwisho atautoa Capello.
Capello ameamua kumchagua Rio Ferdinand kuwa nahodha mpya wakati Steven Gerrard atakuwa nahodha msaidizi. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
zhao
Friday, February 05, 2010 22:55:18
|
|
Mtoa Maoni:
Semenya
Friday, February 05, 2010 23:30:37
|
|
Mtoa Maoni:
Great Thinker
Saturday, February 06, 2010 01:00:51
|
|
Mtoa Maoni:
Mutalemwa
Saturday, February 06, 2010 17:40:55
|
|
Mtoa Maoni:
KING
Saturday, February 06, 2010 19:53:46
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (6), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
Habari zaidi za michezo |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|