|
|
|
Uzalishaji wa Bia Mpya TBL Wasimama Baada ya Mitambo Kuungua |

|
Thursday, July 30, 2009 11:38 AM
UZALISHAJI wa bia mpya ambayo haikufahamika jina lake utasimama kutokana na miundombinu kuharibika katika kiwanda cha bia cha TBL cha jijini Dar es Salam kuungua |
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Miradi kiwandani hapo, Bw.Phocas Laswai alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari ofisini kwake.
Laswai amesema kuwa, kutokana na miundombinu kuharibika walikuwa wanatarajia kuzalisha bia mpya na uzalishaji wa bia hiyo utasimama kutokana na sababu kubwa ya mitambo mipya ya kuzalishia bia iliyotoka nchini Ujetumani imeharibika.
Amesema mitambo hiyo imeungua na kuleta kusimamishwa kwa uzalishwaji wa bia kwa muda mfupi hadi hapo watakaporekebisha mitambo hiyo ama kupatikana mingine.
Pia amesema sababu nyingine itakayosababisha kusimamishwa kwa uzalishaji wa bia hiyo ni kutokana kwa kuungua chupa zaidi ya million 1.6 zilizotarajiwa kuhifadhia bia hizo.
Hivyo Phocas amesema kutachukua zaidi ya wiki moja kusimama zoezi la uzalishaji bia kiwandani hapo kutokana na uharibifu mkubwa uliotokea kiwandani hapo na kupelekea hasara ya mabilioni ya shilingi.
Katika moto huo uliotokea usiku wa kuamikia jana kumepelekea shenena nzima ya kuhifadhia makasha kuteketea na ilifahamika kuwa zaidi ya makasha laki mbili yaliteketea kwa moto huo |
|
|
Na Chondoma Shabani, Dar
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtoa Maoni:
kaka
Thursday, July 30, 2009 16:03:35
|
|
Mtoa Maoni:
ubuguvu
Thursday, July 30, 2009 23:25:03
|
|
Mtoa Maoni:
kaka
Friday, July 31, 2009 08:58:46
|
|
Mtoa Maoni:
moms016
Sunday, August 09, 2009 01:21:58
|
|
Mtoa Maoni:
jane
Thursday, September 10, 2009 23:43:53
|
|
|
|
|
|
Jumla kuna maoni (17), Soma maoni yote |
|
|
|
|
|
|
|
Habari zaidi za biashara na uchumi |
...Habari Zaidi
|
|
Advertisements

|
|
Habari Zilizosomwa Sana |
|
|
|
|
| Photo Gallery |
 |
|
|
 |
|
|
|
|
|
|
|