Kompyuta na Monitors, Laptop toka Triple B Computers, Email: triplebcomputers@gmail.com
   
 
Member's Login
Username
Password
Not a member? Sign Up
            Sign Out

 
 
Wakulima wa embe wasaidiwa milioni 126/-

NewsImages/1731346.jpg
Monday, April 13, 2009 8:17 AM
MFUKO wa Maendeleo ya Afrika (ADF) umetoa msada wa shilingi milioni 126 kwa Chama cha Wakulima wa Embe (AMAGRO) katika mikoa ya Tanga, Dar es Salam na Pwani.
Fedha hizo zilizotolewa na serikali ya Marekani, zinalenga kuimarisha uwezo wa chama hicho.

AMAGRO imekuwa ikihamasisha kilimo cha embe kwa ajili ya uchumi endelevu wa taifa.

Kulingana na taarifa ya Ubalozi wa Marekani Jijini Dar es Salaam, msaada huo utawanufaisha wakulima wadogo 65 wa zao hilo kwa ajili ya kuzalisha embe bora na kuuza nje ya nchi.

Lengo lingine la msaada huo ni kuiwezesha AMAGRO kuwa mzalishji wa embe zenye ubora wa kimataifa pamoja na mamzao mengine ya embe katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Tarifa hiyo ilieleza kuwa, msaada huo wa ADF utawasaidia wakulima wa embe kuanzisha mashamba ya mfano, kuwafundisha wafanyakazi na wakulima masuala ya uongozi, mifumo ya fedha, uendelezaji wa mipango ya biashara na mbinu z utafutaji wa masoko.

ADF ambalo ni shirika la serikali ya Marekani limekuwa likidhamiria kufungua fursa za kiuchumi barani Afrika.

Kwa sasa ADF inafanya kazi zake katika zaidi ya nchi ya 20 barani Afrika ambapo kwa zaidi ya miaka 25 iliyopita Shirika hilo limefadhili karibu miradi 1,500.

Kwa sasa shirika hilo linafadhili miradi 27 ya uwekezaji nchini yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2 ambapo hapa nchini shirika hilo limekuwa likifadhili miradi ya kiuchumi tangu mwaka 1986.

Katika hatua nyingine shirika hilo limetoa msaada kwa wakulima wa kakao wa Mbingu wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Wakulima hao wamepatiwa msaada wa dola za Marekani 99,000 kwa ajili ya kuwajengea wa uwezo wakulima wa zao hilo kupitia chama cvha wakulima wa Kakao Mbingu (MOCOA).

Msaada huo unalenga kuwawezesha wakulima hao kuendesha kilimo hai cha zao hilo kwa ajili ya kuuza nje ya nchi.

 
Suleiman Kipimo    
Mtumie Rafiki Yako
  Comments    Add your Comment

Mtoa Maoni: Maembe    Wednesday, June 24, 2009 12:41:58   
 
Nawapongeza wakulima waliopata msaada wa fedha ili kufanikisha ukulima wa maembe. Tatizo kubwa Tanzania ni ukosekanaji wa usafirishaji wa matunda kwenda ng'ambo. Upungufu wa ndege za mizigo na matatizo yanayoletekezwa na watumishi uwanja wa ndege n.k huchelewesha sana matunda kusafirishwa. Hatimaye matunda yote huharibika. Inabidi serikali kuchunguza na kutatua tatizo hili kabla mavuno hajaanza.
 
 
Mtoa Maoni: joyce Richard    Thursday, September 24, 2009 09:37:02   
 
Naweza kupata anuwani yao ili nipate mbegu za embe!
 
 
Mtoa Maoni: Alobadilijina    Wednesday, September 30, 2009 11:35:56   
 
Kulima si hoja, hoja kuuza na hasa kusafirisha hayo maembe. Tatizo kubwa saaaana hapa TZ ni vikwazo vilivyopo katika mbinu za usafirishaji mazao kwenda nchi za nje. Hasa matunda ambayo mara huoza yasiposafirishwa on-time.
Ukienda nchi za nje utakuta matunda kutoka Afrika ya kusini, toka Misri na Kenya lakini hamna hata mabuyu toka Tanzania!! Tuamke jamani.

 
 
Mtoa Maoni: Richard Membi    Thursday, December 10, 2009 12:02:58   
 
Mimi ni mmoja wa wakulima mdogo wa embe mkaazi wa mkoa wa Tanga. Ningependa sana nijiunge na hicho chama cha wakulima wa embe. Kwa hiyo kwa kupitia jukwaa hili naomba nifahamishwe utaratibu wa kujiunga
 
 
Mtoa Maoni: MacDonald Kiwia    Tuesday, December 29, 2009 07:04:38   
 
Nawapongeza sana AMAGRO kwa kuanzisha chama hicho, ukisoma moja ya malengo ya AMAGRO ni kuongeza wakulima wa embe wajiunge na chama, cha ajabu hakuna website yao, hakuna contacts popote, hakuna msaada wowote unaoweza kusaidia mwanachama mpya kujiunga.Nikiwa ni mmoja wa wenye nia ya kujiunga naomba kwa yeyote ajayejua jinsi ya kujiunga naomba anitumie taratibu za kujiunga na AMAGRO kwenye email yangu realmacd@yahoo.com

Natanguliza shukrani, aksante sana.

 
 
       Jumla kuna maoni (14), Soma maoni yote
Unakaribishwa kuchangia maoni yako
Jina Lako    *
Maoni Yako *
 
*** Unaruhusiwa kutuma maoni yako yoyote yale. Tafadhali tumia lugha nzuri, maoni yenye kukashifu watu na yasiyofaa kwa jamii hayataruhusiwa. ***

*** Maoni yanayotolewa hapa ni mawazo binafsi ya Mtoa Maoni
Nifahamishe.com Haihusiki na maoni yatakayotolewa ***
Habari zaidi za biashara na uchumi
> Benki ya Vijana kuzinduliwa
> Jishindie Milioni 3 Kila Siku na Vodacom
> Precision Air yaanza safari za Bukoba
> Precision Air yazindua nauli maalumu ya Sunrise
> Zain sasa ni Airtel
> Nokia Yatoa Simu Zinazochajiwa na Baiskeli
> TBL yapigwa faini kuvuruga ushindani wa kibiashara
> Gharama za huduma za simu zazidi kupungua
> Uzalishaji wa Bia Mpya TBL Wasimama Baada ya Mitambo Kuungua
> Ewura yashtua wabunge kwa kuwa na matumizi makubwa
> Zain yaja na Balckberry Pre Paid
> Wakulima wa embe wasaidiwa milioni 126/-
> BOT, NMB ijiunge na umoja switch kuondoa kero
> Soko la samaki laingiza bilioni mbili
> Serengeti Breweries yatunzwa tunzo ya dhahabu
> VIDEO - Dhahabu Zatumika Kununulia Mkate Zimbabwe
> ATM 'Yapagawa' na Kuwajaza Watu Mapesa Italia
> Wafanyabiashara Watakiwa Kujitangaza
> BET Yatoa Elimu Kwa Wajasiliamali Nchini
> Wengi hawajui kama simu za zamani zinaweza kutumika kutengeneza vitu vingine
> Mmea wa Mbuyu Unatakiwa Kuzalishwa Kwa Wingi- Wizara
> Arusha Thomson Safaris named among 2009 Best Adventure Travel Companies on Earth
> Mifuko ya Rambo kupigwa marufuku Tanzania
> Uuzaji wa Pamba Nje Marufuku
> Uzalishaji Korosho Utashuka

...Habari Zaidi

 

Advertisements
Tangaza Hapa Email: sales@nifahamishe.com
Habari Zilizosomwa Sana
Photo Gallery
Photo Album

 Huku si Kujitakia kifo?
Random Photo

 Kipindi na maliza mwng primary schl nikiwa na my dream
Habari Mpya Mpya
> Korea yasimamisha safari kuingia Kenya
> Marekani yaishambulia ISIS licha ya Onyo
> Waislamu Waanza Mfungo wa Ramadhan
> Kilichoinyima Siri ya Mtungi tuzo ya Afrika
> Ni Azam bingwa Bara 2013/2014
> BREAKING NEWS" Mzee Muhidin Gurumo hatunaye tena maishani"
> Muendelezo wa majina 201
> Majina ya watu 201 walioteuliwa na Rais
> Ukumbi wa Bunge la Katiba wakamilika
> Mgomo wa wafanyabiashara waingia siku ya tatu leo kupinga mashine EFD